Mrejesho: Nimerejea kazini baada ya sekeseke langu kupata utatuzi

officialBossmtoto

JF-Expert Member
Jul 1, 2019
369
1,178
Kama mnakumbuka kisa kilichonikumba mpaka kupelekea kujifukuzisha kazi huku nikiacha msako wa kunitafuta ukiendelea basi leo nina furaha kuwaletea mrejesho. Tamaa imeniponza, nimeamua kujiachisha kazi

Sitaki kuzungumza sana maisha pale Morogoro, ila kiukweli changamoto zilikuwa nyingi. Nilianza kulala kituoni siku mbili nikiuza simu nikapata pesa kidogo nikapanga kwenye magetto ya uchochoroni. Mengi nilipitia ila nilikuwa nafatilia kwa karibu hali ya usalama wangu huku Dar.

Nilipata msaada kutoka kwa Jamaa mmoja huku JF (jina kapuni) ambae aliniunganisha na Mabinti wawili ambao wao walinihakikishia kwamba yule dada atarejesha ile pesa.

Nilipata hata jeuri ya kumsaka boss kwa namba mpya na nikamuahidi kabla ya mwezi wa pili kuisha hela yake yote itarejea nitaweka na faida.

Kweli tarehe 20/02/2023 nilipigiwa sim nikadaka abood nikaja Dar. Wale mabinti wakaniambia niwape account wakaniwekea 7,000,000 alafu wakaniambia tumekuwekea yote wewe angalia utatuonaje kwa kazi yetu.

Nilipata wasiwasi kidogo kutaka kujua wamemfanyaje yule dada, wakasema ni mzima na hawajamgusa popote ila hatakaa arudie. Niliomba niwape milioni moja sababu ndo kwanza naanza mapambano upya, wakakubali ila nikawaahidi baada ya miezi miwili nitawapa tena milioni nyingine.

Jamaa wa humu Jukwaani naye nikampa shukrani ya laki tano. Boss nilimpelekea hela Cash akanirejesha kazini. Kesho jumatatu naanza rasmi mapambano.

Nafuraha isio kifani. Japo sina hata shilingi ila nitayaweza yote. Hapa nimeongea na mwanangu amenijenga 20.000 ya kuanzia week.

NIMEIJUA NGUVU YA MMU, WALE WAOMBA USHAURI MSIKATE TAMAA
 
Jf is a good place ukikutana na watu wazuri Kuna Kila watu Humu my friend hongeraa sana brooo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Asante sana broo. Alafu the guy aliikataa sana hela. Ilibidi nimuombe kuonana nae na alipokuja nilikuja na hela kwenye bahasha nikamwambia, kaka ichukue tu hata uipeleke yote kanisani kama huna kazi nayo.

Hii ni shukrani yangu kwako.
 
Kama mnakumbuka kisa kilichonikumba mpaka kupelekea kujifukuzisha kazi huku nikiacha msako wa kunitafuta ukiendelea basi leo nina furaha kuwaletea mrejesho.
Kula like yangu....siku zingine usipende kwenda kupiga show kwenye nyumba ya MWANAMKE... Mpk pale utakapo kua assured na usalama wako....

Ukikwama nauli unaweza nichek....hatuto tangazana hata buku5 nikikutumia sio mbaya...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom