Wewe kijana ACHA KABISA HIZO HASIRA ZAKO. ACHA !! Unajitesa bure mwisho utapata vidonda vya tumbo. Usimfanyie lolote. Kama alikuwa amepata ajali akafa kama yule bibi arusi mtarajiwa wa Mbeya ungefanyaje? Ungejiua? No girl friend is worth so much of your feelings. Hakuna rafiki wa kike yeyote anayestahili akuumize nafsi kiasi hicho. Kama ni wasichana wako kibao- hata humu Jf wapo wengi tu hawana mtu. Sasa wewe unajifanya unataka kulipa kisasi ili iweje? Wewe unataka kusema hujawahi kumfanyia mtu mwingine ubaya? Kama kila uliyemfanyia ubaya angekulipa kisasi ungewepo hapo ulipo leo? Kama unataka kumkomoa, kwa kuwa nguo zake hizo unazo, fanya ifuatavyo (kumtisha tu lakini). Tafuta rafiki yako mmoja ili afanye ku-act kama yeye ni mganga. Then tafuta kibuyu, na kitambaa cheusi na kingine cheupe (au hata bedsheet jeupe), huyo mwenzako (mganga feki) ajifunge. Ashike hicho kibuyu azunguke hizo nguo za huyo dada akisema maneno ya kiganga-kiganga, na hapo hapo achome hizo nguo. Hakikisha unapiga video ya tukio zima halafu umtumie huyo dada. Mwambie kwa jinsi alivyokutesa umemwendea kwa mganga. Kila litakalompata atafikiri ni wewe kumbe hujamfanyia lolote mbali na kuchoma hizo nguo zake. Hawezi kujua kwamba ume-act tu. Akikuomba radhi msamehe