Mrejesho: Nipo njia panda

Mrejesho: Nipo njia panda

10 years? Too long, hata kwaka mmoja hapiti inakuwaga jeuri tu huu mda kampata jamaa na wanawake wanaakiri za kuonyesha kipya ni bora zaidi.

Tatizo huyo Ex wa demu(first boyfriend) yeye mwenyewe kamrudia huyo demu wake kama mchepuko tu. Sasa demu kishatowa jeuri kwa jamaa baadae demu ataleta story yake humu tu. Kwa hisia zangu inaonekana huyo demu yumo humu Jamiiforum ndio maana alikuwa anaongea na confidence ya kumfanya jamaa mchepuko wake.
 
Tatizo bwana LA sisi wanaume ni hili. Baada ya haya yoteeeee kesho au kesho kutwa atakuja na kusema alifanya mistake na kwamba umsamehe. After all this pain utakubali na mtarudiana.

Nimecheka sana Leo. Kuna mtu kanitumia picha ya dala dala imeandikwa ;

Moyo kazi yake ni kusukuma damu kupenda ni kiherehere.

All I am saying ni kwamba mambo kama haya hutokea ili uone unaedhania ndiye sie. Huwa ni fundisho lakini mwisho wa siku utakuta anakuja kwako anajiliza anaomba msamaha na atalala hapo kwako na zaidi utamdo kavu kavu. Wanaume sisi. Ahhhhh

Hatari sana!
 
Achana nae mpotezee tu komaa na kazi upate hela maisha yaende!
 
Move on boy ....achana naye..tafuta mwingne uzuri ni kwamba wapo wengii tu me mwanzoni sikuhamin kama nitakuja mpata mwingne kama yule but leo hii nimempata zaid ake na wala sina shaka kwenye hilo


Ahsante mkuu,pia shukrani kwa ushauri wako
 
Nimeskia hasira ila ndo hivyo tena. Hivi wasichana tuna matatizo gani? Kwa nn kabla hujawa na no less usivunje mahusiano ya nyuma? Kwa nn?

Jamani mahusiano nayapenda ila sijawahi muumiza mtu.kiasi hiki,? Mwaka na nusu? Tuwe na huruma sometimes.




Shukrani sana dadang,
 
Pole sana

Hili lilikuwa halina sababu ya kuja kuomba ushauri, wewe ungeomba tukufariji maana hapo una option moja tu ambayo ni kuachana naye,hiyo ya kuwa mchepuko sio option maana inazidi kuonyesha ni kiasi gani huyo mwanamke hafai.

Kuwa mwanaume piga moyo konde, usimwambie chochote kile endelea na maisha yako. Muda unaponya maumivu, with time u be will fine

NB: usiishi ukitarajia kuwa Mungu atamlipizia au kumuombea Mabaya kwenye huo uhusiano wake maana inaweza isitokee hivyo. Shukuru Mungu kakuepusha na balaa maana humo hamna mke.


shukrani sana kwa ushauri wako mkuu
 
Pole sana.
Kiukweli utakuwa umeumia sana.

TAMBUA MAMBO HAYA.
1/Wasichana wengi sana(Hususani Wanachuo) hujenga uhusiano mpya kila wanapotendwa na wapenzi wao lakini hurudia tena uhusiano wao wa zamani mambo yakitulia. Na hicho ndicho kilichokukuta wewe. The earlier one always is stronger in relationship. Dada amerudi kule alikuanzia kupenda kabla ya wewe kumpata. It is very natural! Na usishangae kabisa mambo yakiharibika tena kule, dada akataka kurudi kwako tena.

2/Mshukuru sana Mungu kwa huyo msichana kukwambia wazi wazi kuwa kwa sasa ana mtu wake na hakuhitaji tena wewe. Tofauti na hapo angekuficha halafu ungeendelea kudanganywa kila siku. Lakini ukichunga vizuri unaweza ukagundua kuwa huenda kabla ya sasa, wakati dada yupo na wewe, bado alikuwa anaendelea na uhusiano na huyo jamaa kisirisiri.

3/Usijaribu kabisa kufikiria kuwa mchepuko wake. It is dangerous kabisa. Kuna alot of issue zinaweza kukupata kama utakubali hilo. Zipo issue za Magonjwa, Mimba za kubambikiwa au kutegewa, Kufumaniwa, kuaibishwa na hata kuharibu mahusiano yako mapya kwa mwingine huko mbele ya safari.

4/Kwa sasa fanya haya na utavuka vyema kabisa.
-Kata kabisa mawasiliano na huyo Dada.
-Kuwa karibu sana na Mwenyezi Mungu.
-Kuwa karibu na Jamii(Ndugu, Marafiki, Majirani, Wafanyakazi wenzako nk) jaribu kushirikiana nao, kufurahi pamoja nao.
-Keep busy na kufanyakazi, mazoezi, watch movies nk.
-Tulia kabisa katika issue za mahusiano(It will take few month for that a least 3-6month) lengo ni kuiponya kwanza nafsi yako before kuchukua hatua bora za kumtafuta mwingine.

5/Kamwe usijaribu kabisa kufanya haya.
-Kuishi maisha ya Upweke.
-Kutaka kulipiza kisasi.
-Kujifariji kwa kunywa Pombe, kufanya ngono nk.
-Kukata tamaa ya Maisha.
-Kuendelea kujutia upendo uliokuwa nao kwa huyo dada. Take it as lesson rather than a mistake.
-Kutafuta mchepuko.






Ahsante sana,pia shukrani sana kwa ushauri wako uliotukuka mkuu...Mungu akubariki sana
 
NB: usiishi ukitarajia kuwa Mungu atamlipizia au kumuombea Mabaya kwenye huo uhusiano wake maana inaweza isitokee hivyo. Shukuru Mungu kakuepusha na balaa maana humo hamna mke.

I wish kila mtu angeelewa ulichokiongea. Many times tunatamani kweli wale wote waliotukosea Mungu awaadhibu, awafedheheshe ndo roho zetu zitulie. So unakuta mtu kaumizwa, instead of kujikung'uta ma vumbi asonge mbele, yupo busy kumuombea adui yake mabaya. Kwa hiyo hutoendelea, utabaki na sononeko tu, una uchungu mwenyewe. Afu adui yako anavyofanikiwa ndo unazidi kufa ndani kwa ndani. Hakuna kitu kizuri kama kumuombea mema adui yako. Afu sometimes kuna Vitu tusingejifunza kama tusingetendwa. Tushukuru hata kwa maumivu coz lazima kuna kitu positive tunajifunza
 
Mala zote hua hawafiki mbali hurudi na kukuta milango imefungwa,mimi nilisomesha mwanamke from diploma to degree nikiwa nae Ndani hapa jijini Mwanza,alipomaliza na kuajiliwa na serekali ndipo kivumbi kilipoanza,siwezi kuyasema yote hapa ila ilikua ni wakati mgumu hujawahi ona,na mwisho wa siku mimi nikiwa kazini nje ya jiji,niliporudi ijumaa kwa ajili ya week end nyumbani nilikuta kuna nguo zangu tu ndani ktk nyumba ya kupanga,kama mwanaume amini usiamini sikuumia nikajua huyu ni MUNGU kaniepusha na mengi,nikabeba zile begi na kuishia Hotel then nikasonga mbele na maisha,sasa ni miaka mitatu na nimeoa mwanamke mzuri kwangu kuliko alivyokua,hapa nina taklibani msg zake hazipungui hamsini akijutia maamuzi yake na anapita kwa marafiki zangu akiwasihi waniombe nimsamehe.kwa kipindi nisichokua nae nilipooa mke mwingine ktk miaka miwili sasa njia zangu zimekua za baraka hata kutoka kwenye maisha ya kupanga na kua na nyumba yangu na maendeleo mengine,wanaume wote wenye hekima hupenda wanawake watulivu na wasikivu,ndipo baraka za MUNGU huingia ndani ya nyumba,wanawake wameharibiwa na ile hali ya kujiona wamesoma na wanaweza kuendesha maisha zaidi hata ya baadhi ya wanaume,lakini mwanaume atabaki kua mwanaume,kamwe uumbaji wa MUNGU hautabadilika,nikutoe hofu kijana mtoa mada usibabaike muache aende zake na siku akirudi kamwe usimkaribishe,waweza karibisha kifo.wanawake kwa sasa ni wengi kama mchanga,anaemchezea mwanaume hajitambui tu,hua hawaoni mbele wako kama watoto.


Pole sana kwa yalo kutokea mkuu,naamin nawe ulipitia kipind kigumu sana.pia shukran sana kwa ushauri wako
 
Aisee mdau pole sana..shit happens..wengi wameshatoa ushauri mzuri wa nini unatakiwa kufanya...you are still young kuwa mchepuko..tena at your age inatakiwa uwe una plan ya maisha yako hii ikiwa mwanamke utakayekuja ishi naye huko mbele...usipoteze muda kufikiria kiasi cha investment ulichofanya kwake..kama ni pesa assume umeibiwa au umepoteza...time heals..ili uweze kuheal fasta kuwa busy na mambo yako ya msingi..then ili uweze kuwa huru zaidi epusha mawasiliano nae maana unaweza kwazika...ni ngumu lkn inakubidi ufanye hivyo...unaweza kuwa ulimpenda sana lkn kumbuka yeye sio mama yako...ukilitambua hilo then u can overcome it..jipe time kabla ya kuingia kwenye mahusiano mengine...unaweza ruka moto ukakanyaga miiba jus kwa kutokuwa careful...zaidi nakupa pole na moyo wa ujasiri katika kutekeleza haya mashauri tuliyokupa..




Ahsante mkuu,pia shukrani sana kwa ushauri wako
 
Mshukuru sana Mungu wako kwa sababu amekuwa muungwana hadi akakueleza. Siyo jambo rahisi kwa pande zote.

Kazi yako sasa ni moja tu. Kumsahau na kusonga mbele. Ila kwa uzoefu atakutafuta ndani ya miaka isiyozidi 10. Sijui kwa nini huwa tunasahau kuwa "mkataa pema pabaya panamwita.



Ahsante sana..pia shukrani kwa ushauri wako
 
Back
Top Bottom