Michael Ngusa
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 1,637
- 458
Ndugu zangu,
Kwanza mfahamu kwamba natumia Kinokia cha Tsh 15,000 (true) kusoma jumbe zenu, na kila baada ya muda flani ninalzimika kupanda gari kutoka Misheni hadi Mtongani kwenda kuwajibu Internet Cafe.
Bila jumbe za kutia moyo humu ndani mimi leo nisingekuwepo. Nimekuwa nikisoma jumbe zenu huku nikibubujikwa na kujihurumia sana. Hadi jana saa 4 usiku, nilipokuwa nikiendelea kusoma jumbe za wanaJF, mke wangu alinipigia simu kunijulia hali (hatujaongea tangu aende kwao), nikafuta machozi ili niongee katika hali ya kawaida. Hakugundua lolote, basi...tukatakiana usiku mwema.
Leo saa 9 mchana nikiwa najiandaa kwenda kwa baba mdogo huko Kitunda (ndio mtu wa mwisho ninaweza kulazimisha kwenda kufia mlangoni kwake), nikapokea simu ya mwanaJF, tukaongea, nikamweleza hali ilivyo, basi tukaagana. Baada ya dakika 2, Tsh 100,000 ikaingia kwenye simu! KIDOGO NIANGUKE.
Nikampigia kumshukuru sana, pia akasema niandike namba yangu. Ni Tigo: 0653 257566. Basi nimeahirisha kwenda kwa Bamdogo niko Mtongani ninaandika. Hadi jioni tena, wacha nirudi nyumbani.
UPDATE 2:
Ndugu asanteni sana. Nimepokea msaada wa Tsh laki 1 ingine kutoka kwa mwanaJF ambaye na yeye anaishi nje ila ametumia mwenyeji aliye hapa Dar. Wakikubali nitawajulisha ID zao. Ila kikubwa ni shkrani za dhati kwa jumbe zenu na fedha zenu.
Asubuhi ya leo pia niliitwa na Afisa Jeshi mmoja ambae ni mwanaJF, nikamtembelea hapo kambini, kanitia moyo, kanipa chakula na nimepata tumaini. MBARIKIWE NDUGU ZANGU.