Mrejesho: Nimemrudisha mke na mtoto ukweni baada ya kukosa kazi kwa miezi 3

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,637
457
Ndugu zangu,
Kwanza mfahamu kwamba natumia Kinokia cha Tsh 15,000 (true) kusoma jumbe zenu, na kila baada ya muda flani ninalzimika kupanda gari kutoka Misheni hadi Mtongani kwenda kuwajibu Internet Cafe.

Bila jumbe za kutia moyo humu ndani mimi leo nisingekuwepo. Nimekuwa nikisoma jumbe zenu huku nikibubujikwa na kujihurumia sana. Hadi jana saa 4 usiku, nilipokuwa nikiendelea kusoma jumbe za wanaJF, mke wangu alinipigia simu kunijulia hali (hatujaongea tangu aende kwao), nikafuta machozi ili niongee katika hali ya kawaida. Hakugundua lolote, basi...tukatakiana usiku mwema.

Leo saa 9 mchana nikiwa najiandaa kwenda kwa baba mdogo huko Kitunda (ndio mtu wa mwisho ninaweza kulazimisha kwenda kufia mlangoni kwake), nikapokea simu ya mwanaJF, tukaongea, nikamweleza hali ilivyo, basi tukaagana. Baada ya dakika 2, Tsh 100,000 ikaingia kwenye simu! KIDOGO NIANGUKE.

Nikampigia kumshukuru sana, pia akasema niandike namba yangu. Ni Tigo: 0653 257566. Basi nimeahirisha kwenda kwa Bamdogo niko Mtongani ninaandika. Hadi jioni tena, wacha nirudi nyumbani.

UPDATE 2:
Ndugu asanteni sana. Nimepokea msaada wa Tsh laki 1 ingine kutoka kwa mwanaJF ambaye na yeye anaishi nje ila ametumia mwenyeji aliye hapa Dar. Wakikubali nitawajulisha ID zao. Ila kikubwa ni shkrani za dhati kwa jumbe zenu na fedha zenu.

Asubuhi ya leo pia niliitwa na Afisa Jeshi mmoja ambae ni mwanaJF, nikamtembelea hapo kambini, kanitia moyo, kanipa chakula na nimepata tumaini. MBARIKIWE NDUGU ZANGU.
 
Ndugu zangu,
Kwanza mfahamu kwamba natumia Kinokia cha Tsh 15,000 (true) kusoma jumbe zenu, na kila baada ya muda flani ninalzimika kupanda gari kutoka Misheni hadi Mtongani kwenda kuwajibu Internet Cafe.

Bila jumbe za kutia moyo humu ndani mimi leo nisingekuwepo. Nimekuwa nikisoma jumbe zenu huku nikibubujikwa na kujihurumia sana. Hadi jana saa 4 usiku, nilipokuwa nikiendelea kusoma jumbe za wanaJF, mke wangu alinipigia simu kunijulia hali (hatujaongea tangu aende kwao), nikafuta machozi ili niongee katika hali ya kawaida. Hakugundua lolote, basi...tukatakiana usiku mwema.

Leo saa 9 mchana nikiwa najiandaa kwenda kwa baba mdogo huko Kitunda (ndio mtu wa mwisho ninaweza kulazimisha kwenda kufia mlangoni kwake), nikapokea simu ya mwanaJF, tukaongea, nikamweleza hali ilivyo, basi tukaagana. Baada ya dakika 2, Tsh 100,000 ikaingia kwenye simu! KIDOGO NIANGUKE.

Nikampigia kumshukuru sana, pia akasema niandike namba yangu. Ni Tigo: 0653 257566. Basi nimeahirisha kwenda kwa Bamdogo niko Mtongani ninaandika. Hadi jioni tena, wacha nirudi nyumbani.
Jamani Mungu ampe heri nyingi huyo maana jf, Mungu akutangulie pia
 
Nyingine iko hivi,unapata kazi halafu unaoa kisha unapata mtoto,ghafla unaachishwa kazi,maisha yanakuwa magumu,unashindwa kulisha familia,inabidi mke arudi kwao hadi upate ajira.Inatia huruma sana.
 
Daaah kaka MUNGU wetu awe nawe katika mahangaiko ya maisha usikate tamaa mkuu.
 
najua umezimis bia na totoz, but hyo pesa jitahd ui2mie vzur kaka
 
Kwa nini usifanye biashara hata ya kuuza maji ya kandoro au sigara ambazo mtaji wake ni kama 30000 hivi?? Tatizo mmekariri kuajiliwa
 
hope hiyo hela utaitumia kuanzishia biashara na sio kwa kula.all the best
 
Kila mtu amepewa uwezo wa kupata RIZIKI,wapo wa kuongea tu,kuandika,kulima,kutumia nguvu za mwilini,kufuga nk,si vyote unaweza fanya.
 
Katika JamiiForums kuna watu wana huruma sana, shida za watu wanazichulia kama zao!
 
Back
Top Bottom