Mrejesho: Najuta kuoa mwanamke mlokole

Jul 29, 2015
20
197
Wakuu amani iwe kwenu,

Kwa muktasari tu ni kwamba mimi na mke wangu tulikua na ugomvi kufikia hatua ya kutengana kwa karibu 2 month, hii ilitokana na wife kutojali familia na kushinda kanisani 24/7 ukatokea ugomvi mkubwa na hatimae tukatengana.

Mrejesho wenyewe:

Baada ya miezi miwili wife alinifuata kazini, ilikua siku ya Ijumaa iliyopita na kuniangukia akiomba msamaha kwamba arudi nyumbani kwangu, Hakusema kwamba ataacha matendo ya awali, bali aliniacha kwenye dilemma kwa kusema tu ananipenda hawezi kuishi bila mimi(wengi mnajua Maneno ya msamaha yanavyokua)
Nikamwambia sijaridhika maana """ umeomba msamaha ila hujatakamka how do we move on from here in relation to ur church which is the course of our problems """ Nikamwambia arudi atafakari upya aje tena na msimamo kuhusu suala hilo

Jumamosi nilipotoka kwenye mazoezi (bonanza la kila wiki) Mtaani, nilishangaa kumkuta wife Duka la Jirani karibu na Geti letu akiwa na mtoto na house girl wetu wakiwa na mabegi na mizigo yao, nikawapokea tukaingia ndani, nikamuuliza kulikoni umekuja wakati tulikua bado katika mashauriano, akasema yeye haitaji maongezi zaidi, ameshakata shauri kwamba anahitaji familia yake na mji wake na kwamba ameshakata shauri anaachana na kanisa hilo na tutaanza kuabudu wote kule nakoabudu mimi, hivyo nikawa sina budi kumsamehe.

Na kesho yake ilikua Jumapili alianza rasmi kuabudu nami katika kanisa letu ambalo lipo Jirani kabisa na tunapoishi, ni mwendo wa dakika 15 kwa kutembea na alipokelewa vizuri.

Shida iliyopo tu ni wazazi wake, maana hata hiyo Jumamosi aliyokuja, walikua wamemzuia kwa nguvu zote na Maneno ya laana juu akaamua kuondoka hivyo hivyo kuja, Sababu ya wao kumzuia ni kwamba hawataki ahame hilo kanisa na aliwaambia wazi kwamba kama atarudi kwangu atahama hilo kanisa ambalo ratiba zake ndio chanzo cha ugomvi wetu
wao wamemwambia hawaoni tatizo katka ratiba za hilo kanisa, maadam wanamwamini Mungu na wanakesha wakimuabudu Mungu hivyo hakuna binadam wa kuwazuia.

Nawashukuru wote ambao mlikuja inbox kwa ufumbuzi zaidi wa pamoja, hili tatizo limekwisha, nimeona ni jinsi gani Jf ikitumika vizuri inaweza kuwa na matokeo mazuri, na wengine wote nawashakuru pia.

Hata hivyo mwanzo Nilimruhusu wife kuendelea na kanisa lake ilimradi tu azingatie ratiba na muda, na kukesha kusiwepo kabisa isipokua mkesha wa Christmas, New year na Pasaka, lakini amekataa hilo kwa kuwa kwa vyovyote wazazi wake watakataa wazo hilo kwa sasa waumini wenzie wanamuona kama muasi, wametuma watu kuja kuzungumza nae, wamemwambia asimfuate mwanadam anavyotaka bali amfuate Mungu.

Kuhusu kurudi kwa Rachel, nimefuta mpango huo, nilipojaribu kumfuatilia nikaambiwa kuna jamaa moja limeshamuoa, hata hivyo nilitamka kwa hasira tamko hilo.

Nafuta kauli zote mbaya kuhusu ulokole, nilipotoka kutamka hivyo, ilikua ni hasira pia, nimegundua kumbe kuishi bila mke ni kazi nzito, ni miezi miwili tu lakini ni kama mwaka, pamoja na mapungufu yao kumbe umuhimu wa akina mama ni mkubwa mno, mnisamehe akina mama kwa kumpiga mwanamke mwenzenu, i had no choice, i was at a point of no return that's why i did it, i do apologize.

Mungu awabariki tuzidi kuombeana
 
Maamuzi mazuri , my take muda mungine usijumuishe be specific
 
''Nafuta kauli zote mbaya kuhusu ulokole, nilipotoka kutamka hivyo, ilikua ni hasira pia,
mnisamehe akina mama kwa kumpiga mwanamke mwenzenu, I do apologize''

Thank you very much. Umeonesha ukomavu na uungwana sana.
All the best Bro.
 
Huyo ni chaguo lako, huyo ni chaguo lako,huyo ni chaguo lako...hata kama ni mfupi,Mnene...huyo ni chaguo lako......

Siku zote umlindee,siku zote muombee ,Nyumba yenu iwe baraka,muwatunze watoto wenu.......Alulululululu......duhh!!! Nilikuwa nimenogewa na wimbo ile mbaya...

Hongera sana Reveland patterson kila la heri, nawatakia ndoa njema yenye furaha, amani na Upendo Tele.......siku zote usisahau haya maneno kwa mkeo NAKUPENDA, ASANTE na NISAMEHE.
 
Last edited by a moderator:
Reveland patterson

huyo ni mmoja wa mwanamke mwenye akili ya kujiendesha mwenyewe na hakika nakuomba umpe upendo wa hali ya juu. Ni wanawake wachache waliopo katika nchi yetu. Ni mmoja wa mwanamke anayejua kujirudi na kujitambuwa kuwa amekosea, ni mmoja wa wanawake ambao anajua thamani ya ndoa.

Mwanzo alikuwa hajitambuwi kwa kuwa aliruhusu akili yake kutawaliwa na wapita njia ila baadae amejitathimi yeye kama yeye bila kusikiliza wazo la kichwa cha mpita njia na kutambuwa kuwa ni yeye pekee wa kutatua tatizo la kimahusiano yake na siyo mama yake, dada yake, au kaka yake.

Anajua thamani ya ndoa na anajua hofu ya mungu. Hongera kwa kupata mwanamke mwema. Hao ndo tunaowaita mwanamke mwema.

Nakuomba usije kumpiga tena muonyeshe kuwa yaliyopita si ndwele mgange yajao, na kamwe usiyarudie kinywani mwako.

Mungu atakubariki na kukuongoza katika maisha uliyoyaanza na huyo rechal lilikuwa ni wazo la shetani wa ufarakano..
 
Last edited by a moderator:
Milima na mabonde ya maisha.

Mungu awaongoze katika maamuzi ya busara na mshikamano wa familia yenu.
 
Wee jamaa umepata mke aisee dah na pia nakusifu kwa msimamo hili ndo tunatakiwa tuwe nalo mwanaue lazima uwe na maamuzi na kuyasimamia bila hivyo uwanaume haoto kwepo
 
Safi,kwenye biblia wanasema wenye nguvu wataurithi ufalme wa mungu.Umenifurahisha pale ulipotumia nguvu kumpa kipigo cha nguvu.Usingetumia nguvu,wangekuchezea.BIG UP!Pia hao sio walokole wa kweli,neno la Mungu linasema enyi wake watiini waume zenu!Alifanya makosa kuwatii wa2 wengine.WANAUME WENGINE WAIGE MFANO HUU,VINGINEVYO WANAWAKE WATAWAKALIA VICHWANI.Mwanaume lazima uongoze familia,sio kuongozwa!SAFI SANA.
 
Reveland patterson

Hongera kaka we kweli mwanaume shujaa na Mungu atakusimamia.

Dua la kuku halimpati mwewe kama Mungu mwenyewe alisema mtu atamuacha baba ba mama na ataandamana na mumewe/ mkewe iweje leo aruhusu laana? Hilo kanisa la mkeo halimjui Mungu wala maandiko yake. Kanisa gani linavunja ndoa za watu?

Nampongeza pia mkeo kwa kuuona umuhimu na thamani ya ndoa yake. Yeye na wewe ni mwili mmoja hao wazazi muwaombee tu wala msiwachukie.

Nawatakia maisha mema chunga usichepuke Rachel kitu gani bwana?
 
Last edited by a moderator:
Na biblia iansema Mwanamke/mwanaume atawaacha wazazi wake na kuungana na mumewe/mkewe nao watakuwa mwili mmoja,na katika hilo sidhani kama wazazi wanapaswa kuamua maisha ya binti yao aliyeolewa tayari,wanachopaswa ni kushauri na inaweza kubaliwa au la,na sidhani kama ulokole unaruhusiwa kuvunja ndoa,kwani huko naona ilikuwa ni kukuvunjia ndoa,
Ila hongera kwa kuwa na msimamo thabiti ambao wanaume wote tunapaswa kuwa nao.
 
Back
Top Bottom