Mrejesho: Najuta kuoa mwanamke mlokole

Mrejesho: Najuta kuoa mwanamke mlokole

Uje humu tena baada ya mwaka utupe mrejesho. Pengine sasa utakuja na Habari Nyingine! Mh! labda michepuko yenu imeleta balaa Mkaachana tena!
 
Hongera.
Msahau yaliyopita mjenge familia Bora na Mungu awasimamie.
 
Safi,kwenye biblia wanasema wenye nguvu wataurithi ufalme wa mungu.Umenifurahisha pale ulipotumia nguvu kumpa kipigo cha nguvu.Usingetumia nguvu,wangekuchezea.BIG UP!Pia hao sio walokole wa kweli,neno la Mungu linasema enyi wake watiini waume zenu!Alifanya makosa kuwatii wa2 wengine.WANAUME WENGINE WAIGE MFANO HUU,VINGINEVYO WANAWAKE WATAWAKALIA VICHWANI.Mwanaume lazima uongoze familia,sio kuongozwa!SAFI SANA.
Nimecheka sana!
 
Huyo mwanamke Ana upendo wa dhati ....ni mihim Lila mmoja kwa dhati kumuacha baba yake na mama yake
 
Safi sana mkuu. Huyo mkeo bila ya kipigo heshima isingekuwepo.yani asingejulikana mwanamke wala mwanaume wote sawa. Huyo kajifunza sana tu. Kingine kawaza kuhusu future yake bila wewe itakuwaje?
Move on na maisha mapya bro!
 
Mkuu Reveland patterson hongera sana kwa kufanikiwa kumshinda shetani. Hongera kwa busara kubwa uliyoionyesha kwenye hili.
Nadhani misukosuko toka kwa wazazi imepungua kwa kiasi kikubwa toka mkeo alipoamua kufanya maamuzi yake binafsi ya kuthamini ndoa yake zaidi.
Mara nyingi wazazi wengi wa upande wa wanawake huwa wana hulka ya kuwapenda watoto wao sana kiasi cha kusahau ama kupuuzia mambo ya msingi sana Na mwishowe hupelekea mitafaruku kwenye familia za watoto wao. Bado kuna umuhimu wa kuendelea kuwa karibu nae mkeo hususani kwenye maisha yake ya kilokole. Nimegundua mkeo anahitaji maarifa zaidi ya neno la Mungu kuliko kushinda kanisani. Na hili linabaki kuwa jukumu lako kwa kiasi kikubwa sana. Wanaume tumepewa kuwa wasimamizi wa Nyumba zetu Na kuwa makuhani wa familia zetu. Hivyo basi jipange upate maarifa zaidi ya neno la Mungu ili ukawe Mwalimu wa mkeo kwanza kabla hajawa mwanafunzi huko nje wa Mwalimu mwingine. Ukifanikiwa kufanya hili basi utafanikiwa kwa asilimia 100 kumfanya mkeo akuamini Hata katika maamuzi yako. Nawapongezeni sana kwa makubaliano mliyofikia nadhani ni mfano wa kuigwa. Naungana na share kuhusu kuendelea kutuletea mrejesho ili tujue mnaendeleaje once in a long while.
Nasisitiza tena. Jikiteni wote katika kumtafuta Mungu zaidi kwa sababu mkeo ana kiu kubwa Na hofu ya Mungu ingawa anaonekana maamuzi mengi aliyafanya kwa shinikizo toka kwa wazazi. Wewe waweza kuwa nguzo yake kwenye hilo.
Make her feel loved, safe, protected and admired. You too can play that game.
Aisee Mungu awalinde sana Na kuwabariki
 
Last edited by a moderator:
Mkeo anaenda kuwa mke kitu chema.
Woi amekutana na mwalimu mzuri. Sasa utafurahia maisha
 
Wakuu amani iwe kwenu,

Kwa muktasari tu ni kwamba mimi na mke wangu tulikua na ugomvi kufikia hatua ya kutengana kwa karibu 2 month, hii ilitokana na wife kutojali familia na kushinda kanisani 24/7 ukatokea ugomvi mkubwa na hatimae tukatengana.

Mrejesho wenyewe:

Baada ya miezi miwili wife alinifuata kazini, ilikua siku ya Ijumaa iliyopita na kuniangukia akiomba msamaha kwamba arudi nyumbani kwangu, Hakusema kwamba ataacha matendo ya awali, bali aliniacha kwenye dilemma kwa kusema tu ananipenda hawezi kuishi bila mimi(wengi mnajua Maneno ya msamaha yanavyokua)
Nikamwambia sijaridhika maana """ umeomba msamaha ila hujatakamka how do we move on from here in relation to ur church which is the course of our problems """ Nikamwambia arudi atafakari upya aje tena na msimamo kuhusu suala hilo

Jumamosi nilipotoka kwenye mazoezi (bonanza la kila wiki) Mtaani, nilishangaa kumkuta wife Duka la Jirani karibu na Geti letu akiwa na mtoto na house girl wetu wakiwa na mabegi na mizigo yao, nikawapokea tukaingia ndani, nikamuuliza kulikoni umekuja wakati tulikua bado katika mashauriano, akasema yeye haitaji maongezi zaidi, ameshakata shauri kwamba anahitaji familia yake na mji wake na kwamba ameshakata shauri anaachana na kanisa hilo na tutaanza kuabudu wote kule nakoabudu mimi, hivyo nikawa sina budi kumsamehe.

Na kesho yake ilikua Jumapili alianza rasmi kuabudu nami katika kanisa letu ambalo lipo Jirani kabisa na tunapoishi, ni mwendo wa dakika 15 kwa kutembea na alipokelewa vizuri.

Shida iliyopo tu ni wazazi wake, maana hata hiyo Jumamosi aliyokuja, walikua wamemzuia kwa nguvu zote na Maneno ya laana juu akaamua kuondoka hivyo hivyo kuja, Sababu ya wao kumzuia ni kwamba hawataki ahame hilo kanisa na aliwaambia wazi kwamba kama atarudi kwangu atahama hilo kanisa ambalo ratiba zake ndio chanzo cha ugomvi wetu
wao wamemwambia hawaoni tatizo katka ratiba za hilo kanisa, maadam wanamwamini Mungu na wanakesha wakimuabudu Mungu hivyo hakuna binadam wa kuwazuia.

Nawashukuru wote ambao mlikuja inbox kwa ufumbuzi zaidi wa pamoja, hili tatizo limekwisha, nimeona ni jinsi gani Jf ikitumika vizuri inaweza kuwa na matokeo mazuri, na wengine wote nawashakuru pia.

Hata hivyo mwanzo Nilimruhusu wife kuendelea na kanisa lake ilimradi tu azingatie ratiba na muda, na kukesha kusiwepo kabisa isipokua mkesha wa Christmas, New year na Pasaka, lakini amekataa hilo kwa kuwa kwa vyovyote wazazi wake watakataa wazo hilo kwa sasa waumini wenzie wanamuona kama muasi, wametuma watu kuja kuzungumza nae, wamemwambia asimfuate mwanadam anavyotaka bali amfuate Mungu.

Kuhusu kurudi kwa Rachel, nimefuta mpango huo, nilipojaribu kumfuatilia nikaambiwa kuna jamaa moja limeshamuoa, hata hivyo nilitamka kwa hasira tamko hilo.

Nafuta kauli zote mbaya kuhusu ulokole, nilipotoka kutamka hivyo, ilikua ni hasira pia, nimegundua kumbe kuishi bila mke ni kazi nzito, ni miezi miwili tu lakini ni kama mwaka, pamoja na mapungufu yao kumbe umuhimu wa akina mama ni mkubwa mno, mnisamehe akina mama kwa kumpiga mwanamke mwenzenu, i had no choice, i was at a point of no return that's why i did it, i do apologize.

Mungu awabariki tuzidi kuombeana

Wanawake wa kilokole ni pasua kichwa
 
Mwanamke ataamuacha baba yake na Mama yake na ataishi na mume wake na hao watakua mwili mmoja! Mkeo anahekima ya kimungu..ingawa wapi watasema mjinga kujitebga na wazazi..ila alilllifanya ni la kimungu zaidi! Mpende mlinde na mshikamane maana nyie ni mwili mmoja Kama neno linasema!

Msishangilie ushindi mkajisahau, shetani bado atawapinga..muwe wenye msimamo hata kufa!
 
Mungu akubariki mkuu, sometimes viongozi wa dini wanasababisha watu wamkosee Mungu, kukesha kanisani siku nzima na kuach familia wala sio fundisho la kibiblia na zaidi sana utamkosea Mungu kwa kushindwa kuitelekeza familia hasa watoto ambayo Mungu amekupa.
Kama ametambua makosa yake ishi naye vizuri tu, wenzake watamwita muasi lakini uzidikumtia moyo asijione mkosaji.nafurahi sana kusikia walioachana sasa wamerudiana... congrats na Mungu aibariki familia yako bro.
 
Back
Top Bottom