Mrejesho: Najuta kuoa mwanamke mlokole

Mrejesho: Najuta kuoa mwanamke mlokole

Hongera na Mungu azidi kuwasimamia na kuwaongoza katika ndoa yenu
 
Tatizo siyo ulokole, tatizo ni mafundisho potofu ya viongozi wao!
Mke wangu ni mlokole upuuzi wa namna ile hana. Pia kanisa linalopuuza taasisi ya ndoa ni la kukimbia haraka. Hakuna familia (ndoa) hakuna kanisa, sasa unajengaje kanisa kwa kubomoa ndoa?
 
Huyo ni chaguo lako, huyo ni chaguo lako,huyo ni chaguo lako...hata kama ni mfupi,Mnene...huyo ni chaguo lako......

Siku zote umlindee,siku zote muombee ,Nyumba yenu iwe baraka,muwatunze watoto wenu.......Alulululululu......duhh!!! Nilikuwa nimenogewa na wimbo ile mbaya...

Hongera sana Reveland patterson kila la heri, nawatakia ndoa njema yenye furaha, amani na Upendo Tele.......siku zote usisahau haya maneno kwa mkeo NAKUPENDA, ASANTE na NISAMEHE.

Aaaaaaahhhhaaaaa...kumbe umo eeehheee... aaahhaaa.. nimefurahi dear ulivyoimba . Thanks.
 
Last edited by a moderator:
Kusamehe ni kutekeleza maagizo ya Yesu Kristo kwetu sisi waamini. Ubarikiwe sana na ushibishwe Rohoni soma Waefeso 4:31-32
 
Hongera sana umefanya maamuzi ya kiume nakuhakikishia huyo mwanamke kuanzia sasa atakuheshimu kwa jambo utakalomkataza. Ila hawa viumbe wana maudhi sana kwa hiyo usisahau kumkata kata kidogo makofi pale sauti yake itakapozidi
 
Kwahiyo ukamkubalia arudi ukichukulia ni miezi 2 ulikuwa unajikumbusha jinsi gani usela ulivyomgumu,hebu tupe kidogo raha uliyopata siku ile ya kwanza aliporudi!Uligundua kumbe sometimes shetani ukimuendekeza anaweza kukulaza njaa mpaka unajikuta unamkumbuka mkeo ila kujishusha kumwambia arudi unaona noma!anyway hayo ndio mambo ya ndoa upande mmoja mtamu na mwingine mchungu.
 
Hongera kwa maamuzi magumu ila akileta tena ujinga tandika mpaka atakaposhika adabu. Usimwamini 100%
 
👏👏👏👏👏👏👏
 
Reveland patterson

%
kwangu mimi ulokole ni janga katika maisha ya ndoa nilishamwacha mke kwa ajili hiyo na sitaki hata kukaa jirani na mlokole wanafiki wakubwa baadhi yao wa kweli ni 2
 
Last edited by a moderator:
Hongera mkuu kwa maamuzi yenye busara na yaliyoangalia upande chanya wa family na jamii kwa ujumla.
Lakini naomba nikupe ANGALIZO,kichaa hakiponi.USIMWAMINI MOJA KWA MOJA NA ISHI NAYE KWA AKILI.
 
Back
Top Bottom