Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Nimeelewa mkuu, hapa bila shaka ni kweli atakuwa na shida ambayo kwa namna moja ama nyingine inamfanya kuchanganyikiwa hii ni kutokana na uhalisia wa maisha pengine anayoishi. Kiufupi mm nikiwa mmoja ya wahitimu wa mwaka huo chuo mojawapo mkoani kilimanjalo katika taaluma ya elimu-sanaa, nimejifunza vingi sana hasa kupitia wenzangu ambao wamemaliza lakn kwa kiasi fulani walikuwa wanategemea ajira kama mm. Hawakuona umuhimu wa kujishughurisha kwasababu tu ajira za ualimu zilikuwa za kuchaguliwa kama wanafunzi. Baada ya utaratibu kubadilika wengi walijikuta wanakata tamaa. Badala ya ama kuchukua hatua ili mazingira yalete matokeo wengine wakaamua kukata tamaa jumla. Kwa huyo dada kuna kitu nimekiona kilichofanya au sababisha ashindwe ama kuanzisha hiyo biashara kwa makusudi au ni nje ya uwezo wake. Kwanza: Hajiamini, hii ni kwasababu kiwangu cha pesa alichosema hapo na mahitaji yake kwa ujumla ilikuwa ngumu kuanzisha kwani mtaji ni kidogo sana afadhari angesema 150tsh. Lkn uamuzi aliochukuwa wa kutaka kuolewa sio sahihi kwani hilo ni tatizo jingine wanaume saizi tunataka mdada ambaye naye amejiongeza na ana kitu/vitu hatuoi mtu awe mzigo bali mchango. Anyway akipata kusoma ujumbe huu aje pm nimcouncel maana wahutimu wa shahada hatutakiwi kufikilia kurahisi hivyo.
Mkuu kwa hiyo unataka kusema labda ana shida ya kisaikolojia na sio kwamba anafanya makusudi? ok nawe fanya utafiti kama ukiridhisha kwamba si makusudi, uone namna ya kumsaidia.
 
Mtaje tu Mkuu ili tukomeshe matapeli humu. Ila check na MODS kwanza kama hili halikiuki sheria zao. Kama kuna hii sheria ya kutowataja matapeli basi inabidi ibadilishwe haraka sana.

Hee, wakuu naomba nimtaje, nilikuwa sijapitia profile yake, sasa nimejiwa na wazo la kiipitia, naona aana kila dalili ya kupiga watu wengine. Naona hivi karibuni kaja na uzi wa kutafuta mume, bila saka atataka atumiwe sehemu ya mahari, au wachumba wamtumie hela kidogo ya kupunguza ukali wa maisha.
cc BAK CHIKIRA MTABARI
 
Mtaje tu Mkuu ili tukomeshe matapeli humu. Ila check na MODS kwanza kama hili halikiuki sheria zao. Kama kuna hii sheria ya kutowataja matapeli basi inabidi ibadilishwe haraka sana.
Kuwataja ni halali ilimradi uthibitishe tu mkuu.

Ila ukishindwa kuthibitisha umekiuka sheria.
 
Mkuu kwa hiyo unataka kusema labda ana shida ya kisaikolojia na sio kwamba anafanya makusudi? ok nawe fanya utafiti kama ukiridhisha kwamba si makusudi, uone namna ya kumsaidia.
Yani hapo anaweza kufanya makusudi au dishi limecheza, au yote kwa pamoja. Ila naungana na ww kuwa mwanaume atakae kuwa tayari ni lazima afanye utafiti ndipo ajiridhishe kuwa anafaa kumuoa huyo bint vinginevyo isije ikawa tabu maana shida yake kubwa ni kumpata mtu wa kumtatulia matatizo
 
dah! aiseee
 
Yan watu wa namna hio hata watoto wao waende shule inayofundisha vip hakuna ni zero halafu siku zote hata ukoo wao mzima hauna neema ni laana tupu.
 
Hata humu inawezekana yumo kesha badili jina mkuu ila utapa mara elfu zaidi alizochukua mkuu
 
Dah pole sana mkuu.
Watu kama hao wanapunguza kuaminika kwa wengine wenye nia ya dhati.
 
Hongera kwa moyo huo ni wachache wanaoweza fanya hvo
 
Wakuu,

Kuna mwana jf alijitokeza humu akiomba wana jf tumsaidie mtaji kidogo aanzishe biashara baada ya kumaliza chuo, kukosa ajira na kushindwa kuanzisha mradi wowote kutokana na kukosa mtaji.

Kutokana na alivyokuwa anajieleza, na kwa kuwa mara nyingi nimekuwa nikihamasisha kuwa tujenge utamaduni wa kisaidiana, nilijikuta nikishawishika kumsaidia mtaji. Hata hivyo, kwa makusudi, sikumpatia kiasi chote alichokiwa akihitaji, bali nilimpatia kama 80% na kumueleza kuwa aanze kidogo kidogo halafu mbele ya safari tuone maaendeleo ya biashara kwanza. Lengo langu lilikuwa ni ili nimsome kwanza na kimuelewa ni mtu wa namna gani na yuko commited kiasi gani.

Basi nikamtumia hiyo hela na akanieleza kuwa kashafungua biashara na inaendelea vizuri kwa kuwa bado ni ndogo. Kwa kuwa alieleza kuwa yeye yuko dsm na mimi niko mkoani, nilimueleza kuwa, nitakapokuja dsm, ningeenda kuona biashara yake inavyoendelea.

Baada ya muda, nikaenda dsm, nilikuwa na mambo mengi na muda kidogo wa kukaa dsm lakini nikaona pia ingekuwa vyema nikamuona na kuhakikisha kama kweli alianzisha biashara.

Nilipofika dsm, nikampigia kumjulisha kuwa niko dsm na ningependa kumtembelea.Akanielekeza biashara ilipo ila nilipotaka kwenda akawa anatoa dharura mbali mbali. Muda wangu ukaisha nikaondoka dar.

Mara ya pili nilivyorudi dar, bikampigia tena, akaniambia niende mpaka eneo flani, nikifika hapo nimjulishe maana biashara yake ilipo nikaribu na hapo.

Nikaenda mpaka aliponielekeza, nilipofika ilikuwa ni jioni hivi kwenye saa kumi na mbili na robo.Nilivyomueleza kuwa nimefika, akaniambia nilikuwa nimechelewa, hivyo nisingeza kumuona na anashindwa kuelewa ni kwa sababu gani nilichelewa kiasi hicho.

Nikashikwa na hasira, lakini nikakumbuka moja ya vitu vyenye hasara tu na visivyona faida ni hasira.Nikakumbuka madhara ya hasira kwenye afya ya binadamu, nikageuka kulia na kushoto, nikatabasamu. Mbele kama hatua tano hivi nikaona duka, nikasogea hadi dukani, nikaagiza pepsi yenye ubaridi karibu kuganda. Nikaimiminia mdomoni karibu nusu.Ingawa nilishaelezwa kuwa kiafya kuwa pepsi si nzuri, nilipata burudani iliyokaribiana na ile iliyomfanya wakili mashuhuri ajiuzulu nafasi zake zote. Nikachukua boda na kutoweka eneo lile.

Lengo kuu la kwenda kumuona mwana jf huyo, lilikuwa ni kuhakikisha kuwa kama kweli ameanzisha biashara na yuko serious, nifanye mpango wa kumuongezea kamtaji kwa vile ambavyoingewezekana. Haina maana kuwa nina uwezo mkubwa, bali lengo ni katika jitihada tu za kuungana mkono kwa kuwa sisi sote ni binadamu na ni vizuri kusaidiana.Lakini mpaka naandika uzi huu, sijamuona muhusika wala sijaona biashara iliyoanzishwa na kuzinguliwa nimezinguliwa vile vile.

My take.
Kuna watanzania wanaishi kwenye hali ngumu sana ya kimaisha kutokana na kutokujitambua na ujinga, wengine kwa sababu ya kiburi na dharau.Hawa wataendelea hivyo hivyo tu hamna namna ya kuwatoa hapo mpaka wenyewe waamue tu kubadilika. Hata hivyo kuna wengine wamekwama kama sehemu ya mitihani ya maisha na tukisaidiana wanaweza kuwa watu waliofanikiwa sana.Hata hivyo changamoto kubwa ni kwenye kujua yupi ni yupi.

Naomba kuwasilisha.
bora ungenipa Mimi tu .
 
Kuna watu akili zao huwa zinawza pesa bila kujua jinsi ya kuendeleza hizo pesa.
 
Watu kama huyo ndio wanapelekea watu kuwa ni mioyo ya barafu.
 
mhhhh jamani sasa hili si janga
 
Nishapigwa laki 8 zangu huku nilimkopesha mtu hata simjui amalizie ada zake za mwisho wa mwaka kwa lengo kwamba akipangiwa kitu cha kazi (ni mwalimu ataanza nilipa 50.000 kwa mwezi) mpaka atakapomaliza, tena nikamwambia akiajiriwa afanya kazi miezi 6 kwanza ajijenge ndo aanze nilipa. Nikaja ona jina lake kapangiwa kitu kanambia yupo poa, SIKUWAHI KUMSIKIA TENA TENA TENA TENA!!!!! NIMESEMAGA SITASAIDIA MTU TENA labda yule nayemwona pale anakufa njaa nimpe chakula halafu nilale mbele.

Ninafanya biashara, sasa kuna jamaa alikuwa fresh from school, akalia sana katoka Kigoma hana hata pakukaa na kupata kazi mpaka awe na wa kumshika mkono. Nikampa kazi hapo kwenye biashara yangu. Baada ya kujua biashara na kuniibia akaanza ya kwake, na kujaribu ongea na wateja wangu ahame nao kwa bei nafuu na quality ile ile (maana nilimfundisha kila kitu akawa ndo mbadala wangu nikisafiri), HILI NI funzo la pili. USISAIDIE MTU hawafai kabisa.
ndugu uttoh unapo msaidia mtu lazima hujue ethics za watu wew ni wa kaskazin ukampa muha duka unategemea nin mi nadhani kama kuna kazi mpe lakini isihusishe pesa wala kukuingilia katika dili zako
 
Back
Top Bottom