Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Kuna rafiki yangu alikuja gheto usiku (Nilikua bado nasoma kachuo flani hv)
Akasema nimsaidie nafasi alale na mizigo yake. (Microscope &Others lugage)
Mm nikampa nafasi tukalala kama marafiki tuliozoeana , asubuhi nikamuacha gheto nikaenda class kurudi nakuta kanikomba hela yote ta matumizi, kaweka supeblack kwenye mafuta ya kupaka, kanyoa minywele ya sirini akatapakaza bafuni na hakutoa, akachukua walet na kitambulisho cha mpiga kura, akachukua laini yangu akakopa 5000 aisee niliumia sana..
Nikajiuliza hv kumsaidia ndio imekua kosa?
Bila principal nilikua namuweka ndani kwa muda akanyee ndoo.
.
.
.
Kudhurumiwa hela ndio usiseme sasa simkopi mtu yoyote tena nishakataa labda nimpe yote tu.
Dah, aiseee inaudhi sana brother!
 
Una moyo wa kipekee broo
Mm mwenyewe nishasema kumsaidia mtu mwisho chakula tu..
Watu wanaboa kinoma nikikumbuka niliyofanyiwa basi tu..
Tafakari upya, kumsaidia mtu sawa na wewe unapokuwa unahitaji msaada usaidiwe,.
Duniani hakuna mkamilifu kila mmoja ana mapungufu yake na kwa jinsi yake anahitaji msaada.
 
me wameshanichosha kabisaa nimeamua kukomaa pekeangu tuu. vijana wetu hawapendi kujishughulisha kabisa,wao ni kuvaa jeans,kubeti na ushabiki wa mambo.
 
Huyo anatakiwa kutengwa kabisa na jamii ya kitanzania, kama ingefaa namba yake ya simu na jina lake vingewekwa hapa inawezekana ni tapeli anawaumiza watu huko aliko
 
Mungu amekuelewa mkuu atakujaza zaidi kwa sabab umejaza watu,heko zako ..
 
Naomba nisisitize tena, sikutapeliwa maana sikukopesha mtu, na wala sisikitiki kupoteza hela maana sikwenda kwa ajili ya kurudishiwa.
Cc Islam005[/QUOTE]

Nimekuelewa sana Mkuu, nimewaza tu huyu dada atajisikiaje baada ya kusoma uzi wako ingawa kiukweli kakosea.
 
Naomba nisisitize tena, sikutapeliwa maana sikukopesha mtu, na wala sisikitiki kupoteza hela maana sikwenda kwa ajili ya kurudishiwa.
Cc Islam005

Nimekuelewa sana Mkuu, nimewaza tu huyu dada atajisikiaje baada ya kusoma uzi wako ingawa kiukweli kakosea.[/QUOTE]
Ajirekibishe asonge mbele
 
Mbona mm muha ila sipo hivyo...
unajua waha mnaharibiwa sana na wakimbizi kutoka congo na burundi na wafikapo bongo hujifunza kiswahili na wakiulizwa nyumbani wapi wanasema kigoma na kabila ni muha lakini nyuma ya pazia ni vilo vikubwa sana jamaa wanawake wa uko wana mdomo hatali na wanapenda mali niliwahi mshuhudia rafik yangu mmja kisa wameachana mwanamke alimtumia ndugu zake na walimfyatulia risasi ya mguu kisa nyumba haloo mlioa waha kuweni makini wengine si watanzania
 
Wakuu,

Kuna mwana jf alijitokeza humu akiomba wana jf tumsaidie mtaji kidogo aanzishe biashara baada ya kumaliza chuo, kukosa ajira na kushindwa kuanzisha mradi wowote kutokana na kukosa mtaji.

Kutokana na alivyokuwa anajieleza, na kwa kuwa mara nyingi nimekuwa nikihamasisha kuwa tujenge utamaduni wa kisaidiana, nilijikuta nikishawishika kumsaidia mtaji. Hata hivyo, kwa makusudi, sikumpatia kiasi chote alichokiwa akihitaji, bali nilimpatia kama 80% na kumueleza kuwa aanze kidogo kidogo halafu mbele ya safari tuone maaendeleo ya biashara kwanza. Lengo langu lilikuwa ni ili nimsome kwanza na kimuelewa ni mtu wa namna gani na yuko commited kiasi gani.

Basi nikamtumia hiyo hela na akanieleza kuwa kashafungua biashara na inaendelea vizuri kwa kuwa bado ni ndogo. Kwa kuwa alieleza kuwa yeye yuko dsm na mimi niko mkoani, nilimueleza kuwa, nitakapokuja dsm, ningeenda kuona biashara yake inavyoendelea.

Baada ya muda, nikaenda dsm, nilikuwa na mambo mengi na muda kidogo wa kukaa dsm lakini nikaona pia ingekuwa vyema nikamuona na kuhakikisha kama kweli alianzisha biashara.

Nilipofika dsm, nikampigia kumjulisha kuwa niko dsm na ningependa kumtembelea.Akanielekeza biashara ilipo ila nilipotaka kwenda akawa anatoa dharura mbali mbali. Muda wangu ukaisha nikaondoka dar.

Mara ya pili nilivyorudi dar, bikampigia tena, akaniambia niende mpaka eneo flani, nikifika hapo nimjulishe maana biashara yake ilipo nikaribu na hapo.

Nikaenda mpaka aliponielekeza, nilipofika ilikuwa ni jioni hivi kwenye saa kumi na mbili na robo.Nilivyomueleza kuwa nimefika, akaniambia nilikuwa nimechelewa, hivyo nisingeza kumuona na anashindwa kuelewa ni kwa sababu gani nilichelewa kiasi hicho.

Nikashikwa na hasira, lakini nikakumbuka moja ya vitu vyenye hasara tu na visivyona faida ni hasira.Nikakumbuka madhara ya hasira kwenye afya ya binadamu, nikageuka kulia na kushoto, nikatabasamu. Mbele kama hatua tano hivi nikaona duka, nikasogea hadi dukani, nikaagiza pepsi yenye ubaridi karibu kuganda. Nikaimiminia mdomoni karibu nusu.Ingawa nilishaelezwa kuwa kiafya kuwa pepsi si nzuri, nilipata burudani iliyokaribiana na ile iliyomfanya wakili mashuhuri ajiuzulu nafasi zake zote. Nikachukua boda na kutoweka eneo lile.

Lengo kuu la kwenda kumuona mwana jf huyo, lilikuwa ni kuhakikisha kuwa kama kweli ameanzisha biashara na yuko serious, nifanye mpango wa kumuongezea kamtaji kwa vile ambavyoingewezekana. Haina maana kuwa nina uwezo mkubwa, bali lengo ni katika jitihada tu za kuungana mkono kwa kuwa sisi sote ni binadamu na ni vizuri kusaidiana.Lakini mpaka naandika uzi huu, sijamuona muhusika wala sijaona biashara iliyoanzishwa na kuzinguliwa nimezinguliwa vile vile.

My take.
Kuna watanzania wanaishi kwenye hali ngumu sana ya kimaisha kutokana na kutokujitambua na ujinga, wengine kwa sababu ya kiburi na dharau.Hawa wataendelea hivyo hivyo tu hamna namna ya kuwatoa hapo mpaka wenyewe waamue tu kubadilika. Hata hivyo kuna wengine wamekwama kama sehemu ya mitihani ya maisha na tukisaidiana wanaweza kuwa watu waliofanikiwa sana.Hata hivyo changamoto kubwa ni kwenye kujua yupi ni yupi.

Naomba kuwasilisha.
Weka ID yake japo tumpe za uso kidogo, mjinga kabisa huyo!!

Wengine wanakufa kwa kukosa watu wa kuwasaidia yeye anafanya ujinga!!
 
Pole kwake ipo cku atajutia hy nafasi maana ujanja ukizidi unakuwa ni ujinga, hongera sana kk kwa kuwa na moyo wa kusaidia vijana, person like you are in short supply in this world.
 
Huyo yupo kwenye kundi la WANA RAMBIRAMBI
 
Nimeamin unaweza mchukia mtu bila kumjua, Aisee hilo jamaa nimelichukia km funza.
 
Back
Top Bottom