Mrejesho: Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mrejesho: Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Kwanini umuzuie mdogowako kama wewe unaachika? Au wivu unakusumbua? Naona dalilizote za kurudi kwa mumeo! Na urudi acha ujinga utaumia na wivu tu
 
Hivi umesoma vizuri hayo maelezo ya Leah lakini? Mme Alitakikana awe mpole aombe msamaha kwa kilealichofanya yeye ndo kwanza anasema shemeji yake hakuwa Dada yake Na alichokifanya haoni kama ni kosa.
Wewe kwako ni sahihi shemejio, Mme wa Dada yako mkubwa kumpa mimba mdogo wako wa mwisho harafu asiombe msamaha Na aseme alikua sahihi kabisa,hebu tafakari,
Nmemsoma toka Uzi wake wa kwanza.. Nkamuelewa.. Mumewe kweli alikosea.. Lakini, kwa kadiri ya maelezo ya huyu bibie.. Naona walikuwa wanamuuliza jamaa maswali mengi mno kum-confront ili jamaa a-behave namna wao wanataka... Kitu ambacho si sahihi... Sio kila mtu anaweza kujiweka chini mbele ya Umati.. Bi dada alishaombwa msamaha personally,sasa ya nini tena kuja kudhalilishana mbele ya crew kuuubwa ya mara wachungaji na sijui wazee wa kanisa ambao mume anajua wana nyumba ndogo zao..???
Nadhani huyu bibie angetakiwa afanye selection nzuri ya watu ambao wana ushawishi kwa mumewe kama alitaka kuombwa msamaha mbele ya kadamnasi.
 
Pole sis, usiombe yakukute mume anauma kupita maelezo,lakini inapobidi MUACHE AENDE.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Kutoa mimba ni mauaji ya kiumbe kisicho kuwa na hatia, isitoshe ni kinyume na sheria za nchini pia ni dhambi mbele za Mungu. Kwahiyo hatatoa
Kwanini umeweza kumsamehe mdogo wako na Mme wako hukumsamehe toka mwanzo? Lazima angeongea hivyo kwa kua haikuwa na namna wote mnajua kosa ni nini na hukuonesha ushirikiano wa kumsamehe toka mwanzo. Which means kuna roho ulionesha kwa mdogo wako na kwake zina utofauti. Je Kati ya yeye na mdogo wako Nani mwenye makosa Kati ya mdogo wako na mmeo? Na je Nani anastahili kusamehewa? Mwisho una makosa kumleta mdogo wako kukaa hapo kwenu kwa mda mrefu. Kingine mnapaswa kujiuliza je alimbaka? Kama sio basi mdogo wako alileta ushawishi na wote wana kosa moja na wanapaswa kusamehewa, Walimwengu walisema ukitaka kujua utamu wa Ngoma uicheze. Hio ndio ndoa Dada yangu msamehe ganga mbele ndoa ni zaidi ya uijuavyo cha msingi ni uvumilivu zaidi ya uvumilivu hamna ndoa.
 
Nmemsoma toka Uzi wake wa kwanza.. Nkamuelewa.. Mumewe kweli alikosea.. Lakini, kwa kadiri ya maelezo ya huyu bibie.. Naona walikuwa wanamuuliza jamaa maswali mengi mno kum-confront ili jamaa a-behave namna wao wanataka... Kitu ambacho si sahihi... Sio kila mtu anaweza kujiweka chini mbele ya Umati.. Bi dada alishaombwa msamaha personally,sasa ya nini tena kuja kudhalilishana mbele ya crew kuuubwa ya mara wachungaji na sijui wazee wa kanisa ambao mume anajua wana nyumba ndogo zao..???
Nadhani huyu bibie angetakiwa afanye selection nzuri ya watu ambao wana ushawishi kwa mumewe kama alitaka kuombwa msamaha mbele ya kadamnasi.
Basi kama uliufatilia Uzi toka mwanzo nafikiri pia hukuuelewa,Huu jamaa hajawahi kuomba msamaha toka mwanzo,
Pili watu walioalikwa ni wazazi wa pande zote mbili yaani wazazi wake Na mwanaume,mwanamke, Na wachungaji waliofungisha ndoa yao ni Nani tena unafikiri angeweza kumshawishi huyu MTU??
Iwapo wazazi wake,Na wazazi wa mkewe pia walezi wake wa rohoni kawavunjia heshima kwakuwambia hata wao wana nyumba ndogo pengine unafikiri huyu bwana yuko sawasawa?
Hapana usimtete kwa kua ni mwanaume huyu akili yake haiko sawasawa angekua mwingine toka mwanzo wa hii inshu angekua ni mtu wakujutia kile alichofanya kwa kuomba msamaha kwa idadi isihesabika.
Ona mdogo mtu pamoja Na huo uovu aliomtendea dadake lakini tunaambiwa kamfuata dadake zaidi ya Mara kumi kwenda kuomba msamaha Huu ndo ungwana hata mtu una shawishika kusamehe.
 
leah2;
Nadhani wewe ni mtu wa maamuzi ya haraka haraka sana. Uliamua kusitisha kuzaa ili usome kwanza huku ukijua wazi kuwa upo kwenye ndoa. Sidhani wazo la kuendeleza kisomo alilitoa mumeo bali ni wewe mwenyewe. Mumeo alikuridhia japo shingo upande alipopata ka mwanya akamtumia mdogo wako ili aone kiumbe chake (mtoto).
Uamuzi wa pili ni kumkaribisha mdogo wako kwako mahali ulijua wazi kuwa kuna mwanamume, unaye lala naye kila siku. Hukuwaza kuwa, yawezekana akaamua kufanya kautafiti kuwa, hivi huyu mdogo mtu ni mtamu ka dadake? Ukadhani unakaa na malaika Gabriel ndani asiye na tamaa. Matokeo umeyaona.
Uamuzi mwingine mbaya ni kuwaleta jopo la watu ambao woote ulijua kuwa wapo upande wako ili kuja kukuhalalishia hiyo talaka unayofurahia kuwa utaitoa hivi karibuni.
Sawa kabisa, lakini naomba nikuambie; Tuliza munkari. Hao uliosema ati uliwaleta wachungaji, hawawezi kuihalalisha talaka yako. Ni neno la Mungu kuwa; Aliowaunganisha Mungu, mwanadamu, (Leah2) asiwatenganishe. Usiifurahie talaka, hiyo ni Passport ya kuingia kuzimu kwa Mkristo awaye yote. Hakuna talaka.
Sasa, tulia kabisa, rudi kwa Mungu wako, mlilie hata akusikie, akupe roho ya kusamehe, watume watu wema wamwendee huyo mumeo, wamweleweshe tu atapata akili mpya aone kosa lake, atubu, amrudie Mungu. Ndoa yako iliingia tu doa, usiikate nguo ati kwa sababu imeingia doa. Kumbuka nguo ni hiyo moja tu unayo.
Ati unasema, Sidhani ka nitamtamani tena mwanamume. Usitamani mwanamume mwingine, mtamani mumeo. Hata kama hatarudi mapema, mwombe kuwa, ukijisikia hamu saana usitumie "Midoli ya kichina/japan", mwombe uende alipo akutoe ham kidogo. Hutakuwa umezini bali ni mumeo tu mpaka kufa. Huu ndo ukweli japo shubiri. Kama ulikimbilia ndoa ya kikristo hayo ndo maukweli yake. Hakuna talaka bali lolote utakalo tenda, ni zinaa tuuu. Si mimi, ni Mungu kasema. Kwa kheriiiii kubali au kataa hii ndo kweli japo shubiri mesaa tuuu
Chukua like mia! Kuna sehemu kuna kosa kubwa kafanya huyu mdada!
 
Kwanini umeweza kumsamehe mdogo wako na Mme wako hukumsamehe toka mwanzo? Lazima angeongea hivyo kwa kua haikuwa na namna wote mnajua kosa ni nini na hukuonesha ushirikiano wa kumsamehe toka mwanzo. Which means kuna roho ulionesha kwa mdogo wako na kwake zina utofauti. Je Kati ya yeye na mdogo wako Nani mwenye makosa Kati ya mdogo wako na mmeo? Na je Nani anastahili kusamehewa? Mwisho una makosa kumleta mdogo wako kukaa hapo kwenu kwa mda mrefu. Kingine mnapaswa kujiuliza je alimbaka? Kama sio basi mdogo wako alileta ushawishi na wote wana kosa moja na wanapaswa kusamehewa, Walimwengu walisema ukitaka kujua utamu wa Ngoma uicheze. Hio ndio ndoa Dada yangu msamehe ganga mbele ndoa ni zaidi ya uijuavyo cha msingi ni uvumilivu zaidi ya uvumilivu hamna ndoa.
Mdogo mtu kaomba msamaha zaidi ya Mara kumi, Mme hajaomba hata Mara moja anasema Yule shemeji hakua dadake hivyo yeye anaona kawaida kwa alichofanya sasa kwanini aendelee kuishi Na mtu wa namna hii?
Pole sis, usiombe yakukute mume anauma kupita maelezo,lakini inapobidi MUACHE AENDE.
 
Pole kwa mapito hayo. Endelea kumuombea tu maana naona dhahiri nguvu za kipepo zikitenda kazi hapo. Kama amekutisha usiache ku report hilo Police pia.
 
Sasa mkuu, kulikuwa na haja gani ya kuweka kikao? Mi nadhani ajenda kuu ilikuwa usuluhishi ili ndoa ilindwe!! au?
Usuluhishi si lazima uulizwe kama hautorudia makosa ? sasa kama ameleta jeuri mbele ya wazazi wao wote unafikiri likitokea tatizo watakimbilia wapi ?
 
  • Thanks
Reactions: nao
Ninaogopa kumkosoa maana anatukana ukimwambia upande wa pili wa shilingi asikokupenda! Ngoja nikuonyeshe mwanga kidogo. Aligoma kuzaa wakati umri unakwenda na wanaume wa kisasa wanataka kuzaa mapema ili uwe na control ya watoto katika kuwatafutia fedha za kusoma ukiwa kijana. Alimleta dogo asiye na uwezo wa kiuchumi! Hili ni shida kubwa hasa kama mahitaji ya huyu dogo yalitimizwa na jamaa. Akawaacha wawe karibu eti mtu na shemeji yake! (Newton's third law of motion?). Ukaribu huo ungekuwa hivyo kwa dogo wa kiume? Sasa anafanya kosa lingine kubwa kuliko la kwanza.

Eti anaamua kuacha ndoa! Eti amemuonya mdogo wake aachane naye na amekubaliwa! Hana mtoto na huyo jamaa na dogo ndo anazaa mtoto ambaye baba yake mzazi ni jamaa! Ngoja nisubiri mrejesho!

Lakini pia kwa historia ya hii hadithi inaonyesha huyu dada anapenda ligi. Alikataa kuzaa, asome kwanza! Ameleta hoja ya upande mmoja hapa! Anaamua kuwakusanya wanaomuunga mkono na wanaoongea kinachomfurahisha! Ameamua kuacha mji! Amemuonya mdogo wake asiendelee wakati ndo anategemea mtoto! Sasa huyo mtoto atalelewa na nani??? Anatukana watu wanaotofautiana naye! Huyu dada huyu!!!!!!!
 
Mdogo mtu kaomba msamaha zaidi ya Mara kumi, Mme hajaomba hata Mara moja anasema Yule shemeji hakua dadake hivyo yeye anaona kawaida kwa alichofanya sasa kwanini aendelee kuishi Na mtu wa namna hii?
There is some thing hidden behind Dada yangu. Issue ya kusikiliza upande mmoja ni ngumu kujua siwezi jua bt akili inagoma kuwa upande wa pili haukuomba samahani navyoelewa uliomba sema haukupewa nafasi. And then hio samahani aliyo ipa base ni ile ya ukingoni wakati washajua kosa lipo wapi na kila kitu kinajulikana. BT ungekuwa tumepata maelezo ya pande zote mbili tungejua.
 
Back
Top Bottom