Mrejesho: Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mrejesho: Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Baada ya muda/miaka kadhaa baadae mdogo wako ataendelea kuwasiliana na shemeji yake kuhusu mtoto kwani ni mzazi mwenzie na huenda taratiibu wakaendeleza mahusiano yao japo kwa siri kwa tiketi ya kuwa ni mzazi mwenzie.

Nikupongeze sana kwa kumsamehe mdogo wako ila haikuwa na haja ya kumtahadharisha kuendelea na shemeji yake (ni km vile unampa kiapo/ laana imfikie) kwa lengo la kuwa ni dhambi kubwa sana atakapokuja kufanya hivyo baadae hata km ulishampa talaka.

Mapema baada ya kukamilisha zoezi la talaka tambua mwenye nafasi kubwa ya kuwasiliana na mwanaume huyo ni mdogo wako, sio km shemeji yake bali ni mzazi mwenzie kwa maendeleo na malezi ya mtoto wao.

In a long run kwa miaka kadhaa baadae jifunze na utambue mapema wazazi hao watakuwa na mawasiliano mazuri na wataweka tofauti zao pembeni kwa malezi bora ya mtoto wao wa damu, kwani mtoto anahitaji malezi ya baba na mama pia katika maradhi, shida na furaha.
 
Siku hizi ukioa au ukiolewa badala ya kujiletea faraja na raha za maisha kwa kumpata mwenzio...kinyume chake unajiletea mahangaiko na mateso kwenye maisha yako......

Badala ya ndoa kuwa baraka na neema zimekuwa ni chem chem ya mabalaa na mafarakano kwenye maisha yako....

Siku hizi ukioa au kuolewa ni kama unajiweka karibu maradhi ya moyo na visukari visivyo na sababu.....au hata kifo kabisa.....

Siku hizi ndoa baada ya kujenga undugu wa karibu kwa kuunganisha familia mbili badala yake zinakuwa chanzo cha uadui baina ya familia mbili......

NDOA ZIMEKUWA NDOANO......
una akiiiiili!!!
hats off
 
Wee acha tu! Sidhani kama naweza taka mwanaume tena
acha hiyo habar wewe!!
chaaaa!!!
jipe nafasi ya kuishi tena!!
maisha yetu ya jana hayatuhukumu tuishi kesho yetu hivyo!!
Love Live Laugh at veeeeery of ur best!!!
Ilikuwa ndoa njema ulifurahia imeenda mrama,umeumia fine but umeshafanya maamuzi haitakuwepo tena,grab the opportunity wen it comes,it surely does!!
woooih eti sitataka mwanaume tena!!!
 
Habari zenu wadau wa MMU,

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru mods na members wenzangu wote kwa mawazo, ushauri na michango yenu katika thread niliyoleta huku kipindi cha nyuma yenye kichwa kisemacho "mume wangu amempa mimba mdogo wangu"

Nimepata muda wa kutosha kutafakari michango ya mawazo yenu namna ya kumaliza tatizo hili na MUNGU amekuwa upande wangu na nimefanikiwa kufikia muafaka.

Jana ndo ilikuwa siku ya kukutana tena kwenye kikao pamoja na wazazi wa pande zote mbili na safari hii tukihusisha na wachungaji wetu na tulikaa na kufikia muafaka kama ifuatavyo;

Katika kusikiliza maelezo ya pande zote mbili yaani kutoka kwangu na kwa watuhumiwa, mume wangu aliamua kujibu vibaya kikao baada ya kuona anaandamwa na maswali ambayo haya kumfurahisha.

Nasikitika kusema alidiriki kujibu kuwa kama kosa limeshatokea waamue haraka yeye ana mambo ya muhimu ya kufanya kuliko hili.

Akaenda mbali zaidi kuwa hata wao wanajiona ni watakatifu kumuandama na maswali wana nyumba ndogo kibao sema ni kwa vile hawaja kamatwa. Pamoja nahayo akaongeza kuwa hajawahi jutia kosa lake kwani yule si dada yake wala hana ukoo nae kwahiyo ilikuwa ni sawa tu.

Wazazi wake walijaribu kumkatisha asiendelee kuzungumza lkn hakujali akapaza sauti zaid hapo ikabidi wamuache tu aongee mpaka amalize, aliongea mengi na magumu sana sina ujasiri wa kuyaandika hapa kwakuwa hayatamkiki kwa mtu mwenye akili timamu.

Baada ya kumsikiliza kikao kiliniuliza nasemaje kuhusu ndoa yangu.

Sikuwa na la zaidi, niliwaambia kwakuwa kwake ni jambo la kawaida sana na mimi kwangu si la kawaida nisingeweza kuendelea kuishi na mtu mwenye mtazamo tofauti.

Wachungaji walisema wao hawana mamlaka ya kuvunja ndoa ya kikristo lakini kwakuwa mwanaume ameongea maneno yenye dharau inaonesha hana moyo wa toba na angeendelea na uzinzi hivyo wanaungana na mimi katika maamuzi yangu.
Walinishauri nifuate taratibu za kisheria kuvunja ndoa.

Kwa upande wa mdogo wangu yeye alishanifuata zaidi ya Mara kumi kuniomba msamaha, sikuona sababu ya kutomsamehe nilimsamehe na jana niliuthibitisha msamaha wangu katika kikao lakini nilimtahadharisha kutoendelea na shemeji yake nae hakupingana nami katika hilo.

Mwanaume ameanza vitisho kwamba nijiandae kupambana.
Binafsi siogopi nipo tayari kupambana lakini sipo tayari kuendelea kuishi na mwanaume fedhuli kama yeye.

Hapo ndipo tulipo fikia na najiandaa kutafuta talaka kisheria.

Asanteni sana naamini hili limepita imebaki utekelezaji wa utenguzi wa ndoa.

Nakaribisha michango yenu ya mawazo..

Pia niwashukuru kwa kampani yenu katika kipindi kigumu

Upo single?
 
kwenye maelezo ya jamaa akusema kuwa wewe ni gogo kitandani na mdogo wako ni mtamu mno!!!!?

Kama alisema neno hili au linalofanana na hili basi jamaa hana makosa ila wewe ndio ulimkosea mshkaji
 
Je ktk kikao hicho ulikuwa tayari kumpa second chance au ulitaka kutoa tu maamuzi yako ya kuachana?
Kila la kheri, mungu akuongoze kwenye maisha mpya unayoenda kuyaanza kwani haikuwa dhamira yako.
Kwa upande wa vitisho anavyovitoa, inabidi kuwa makini naye maana siku hizi binadam wamebadilika sana.
 
Hakuna mtu aliyewahi kuja hapa kutupatia mazuri ya ndoa yake. Kila mtu anakuja kusema mabaya. Nikimaanisha mijadala inatoka kwa wAtu wa aina moja, mawazo mamoja, na mwishowe hizi hadithi zinakuwa sio za kweli na kufikirika ili kufufanya tutoe povu tu hapa. Ain't buying this story, it's too monotonous (common) hapa forum.
 
Duh.ngoja nipite. Japo sikusoma hiyo ya kwanza,ila mmmh! Neno moja tu POLE!huyo mumeo na mdogo wako wameleta laana na dosari kubwa katika familia .haitakaa ifutike.POLE TU NDUGU.
 
Sasa hapa umesaidia nini ndugu? wakati mapambano bado yanaendelea according to wewe mwenyewe...kweli nyie mnamconfront mtu kwa maswali mnategemea asikasirike na afight ili kulinda EGO yake? Na hao wachungaji nao badala wakushawishi uwe na moyo wa kusamehe kama Yesu wenu aliyewaokoa same people waliomdhihaki na kumtesa.. Wao wanashauri muachane..

Hivi siku hizi huko college za theology hawasomi psychology?
 
Muache aende lea,nenda mahakamani kalimalize,huyo ni looser ndio mana anaamua kupambana anapokosea sio kutubu,muache afanye anayotaka,na hivyo ndivyo alivyo hukua unamjua wewe sasa ndio unamjua vizuri
 
  • Thanks
Reactions: nao
Leah pole sana. Endelea kusimama na Mungu na usiogope vitisho. Wanaume wengine ni mitihani. Muse no na huruma jamani. Na alaaniwe mwanaume Huyu. Unamfungulia zipu Shemeji yako? Mabalaa yatamfuata sana. Ajiandae.
 
Hakuna mtu aliyewahi kuja hapa kutupatia mazuri ya ndoa yake. Kila mtu anakuja kusema mabaya. Nikimaanisha mijadala inatoka kwa wAtu wa aina moja, mawazo mamoja, na mwishowe hizi hadithi zinakuwa sio za kweli na kufikirika ili kufufanya tutoe povu tu hapa. Ain't buying this story, it's too monotonous (common) hapa forum.
Mh,mbona misijawahi kuleta baya langu?usikrem,mwanaume mtu na mwanamke mtu
 
Sasa hapa umesaidia nini ndugu? wakati mapambano bado yanaendelea according to wewe mwenyewe...kweli nyie mnamconfront mtu kwa maswali mnategemea asikasirike na afight ili kulinda EGO yake? Na hao wachungaji nao badala wakushawishi uwe na moyo wa kusamehe kama Yesu wenu aliyewaokoa same people waliomdhihaki na kumtesa.. Wao wanashauri muachane..

Hivi siku hizi huko college za theology hawasomi psychology?
Hata angesamehe yangerudi?kusamehe haimaanishi kurudiana kama mwenzie hataki?
 
Sasa hapa umesaidia nini ndugu? wakati mapambano bado yanaendelea according to wewe mwenyewe...kweli nyie mnamconfront mtu kwa maswali mnategemea asikasirike na afight ili kulinda EGO yake? Na hao wachungaji nao badala wakushawishi uwe na moyo wa kusamehe kama Yesu wenu aliyewaokoa same people waliomdhihaki na kumtesa.. Wao wanashauri muachane..

Hivi siku hizi huko college za theology hawasomi psychology?
Hivi umesoma vizuri hayo maelezo ya Leah lakini? Mme Alitakikana awe mpole aombe msamaha kwa kilealichofanya yeye ndo kwanza anasema shemeji yake hakuwa Dada yake Na alichokifanya haoni kama ni kosa.
Wewe kwako ni sahihi shemejio, Mme wa Dada yako mkubwa kumpa mimba mdogo wako wa mwisho harafu asiombe msamaha Na aseme alikua sahihi kabisa,hebu tafakari,
 
Back
Top Bottom