Mrejesho: Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mrejesho: Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Vp mtoto atakayezaliwa atamwita nani? Je akiwa anamwangalia atakuwa na furaha ya moyo juu yake?[emoji57] [emoji19]
Mtoto kosa lake nini? Siwezi kumtenda uovu malaika asiyekuwa na hatia
 
Dogo nimemsamehe kweli, na nilimshauri asijerudisha mahusiano tena..na yeye alikili kutorudia na wazazi wakampa kiapo na kumlisha yamini ikitokea amerudia atapatwa na laana.

Pia niliamua kuendelea kuishi nae kama awali mpaka atakapo pata kazi nakujitgemea..nipo tayari kumudumia mtoto pia pindi atakapo zaliwa.
Well, hata kama amelishwa yamimi(sijui ni nini), lakini ukweli mchungu ni kuwa the guy won't vanish any time soon, connection yenu ipo kwa huyo mtoto, mbaya zaidi kwa mdogo wako, unless mumhamishe nchi.

Kingine, naona you get bitter kwa comments zinazoenda opposite, najua upo na hasira, uchungu, unalaani kwa nini ulikutana na fedhuli wa namna hiyo, lakini nikuambie kitu, huu ni mda mzuri pia kujitafakari. Huyu jamaa ana makosa sana, kulala na mdogo wako, mbaya zaidi kumpa mimba ndani mwenu ni kitu kitachukua mda sana kukutoka. Lakini it's time to reflect on "YOU" too. Huwezi kuwa malaika kuwa maisha yako na jamaa you were perfect, huu ndio mda wa kujitafakari. Labda kiburi cha elimu, kazi, pesa...

Bahati mbaya hatuna access na huyo jamaa, he needs therapy, anapitia kipindi kigumu japo hajijui. Huwa nasema, tunahitaji wataalamu wa afya ya akili kama tunavyowahitaji matabibu wengine. Both of you need therapy, mnayopitia ni magumu kudili nayo hivi hivi.

Kila la heri.
 
Yeye si alimtakia mwenyewe mwanaume wa hivyo mkuu? In short mim sio muumini wa kulelewa Mimi siweziacha ingia hata kulala kwenye getto la mwanamke kabisa kamwe.
Hizi tabia tuziepuke zinatudhalilisha.
Hata kama una chumba kimoja kiwe chako aisee
 
Bigbro haita kaa itokee kbsa
..kumsamehe naweza lkn si kurudiana seriously

Muda ni tiba nzuri sana katika maisha. Never ever dare ever say NEVER, chochote kinaweza kutokea katika maisha yetu haya, Muombe sana MUNGU.
 
Well, hata kama amelishwa yamimi(sijui ni nini), lakini ukweli mchungu ni kuwa the guy won't vanish any time soon, connection yenu ipo kwa huyo mtoto, mbaya zaidi kwa mdogo wako, unless mumhamishe nchi.

Kingine, naona you get bitter kwa comments zinazoenda opposite, najua upo na hasira, uchungu, unalaani kwa nini ulikutana na fedhuli wa namna hiyo, lakini nikuambie kitu, huu ni mda mzuri pia kujitafakari. Huyu jamaa ana makosa sana, kulala na mdogo wako, mbaya zaidi kumpa mimba ndani mwenu ni kitu kitachukua mda sana kukutoka. Lakini it's time to reflect on "YOU" too. Huwezi kuwa malaika kuwa maisha yako na jamaa you were perfect, huu ndio mda wa kujitafakari. Labda kiburi cha elimu, kazi, pesa...

Bahati mbaya hatuna access na huyo jamaa, he needs therapy, anapitia kipindi kigumu japo hajijui. Huwa nasema, tunahitaji wataalamu wa afya ya akili kama tunavyowahitaji matabibu wengine. Both of you need therapy, mnayopitia ni magumu kudili nayo hivi hivi.

Kila la heri.
Vyema sana mtumishi. Tatizo lillilopo ambalo ajalipa base ni kaamba bado kuna connection tuu ya mshikaj kwa mtoto na hicho ndo kiini kikubwa kitakachofanya uhusiano wa moja kwa moja kuwepo kwa hali ya chini aidha kwa mdogo mtu sababu base kubwa kitakuwa ni mtoto
 
Mungu hasamei bila kuombwa msamaha tena inategemea na kosa..makosa mengine hugharim toba ya machozi kama unabisha muulize mtume petro alipomkana Yesu Mara tatu toba yake ilikuaje..kingine muulize Yuda yule eskarioti alipo msaliti Yesu hakupewa msamaha mpaka akaamua kujinyonga kukimbia dhambi yake. Anachofanya Mungu ni kukusanya hasira kwaajili ya hukumu ya siku ya mwisho. Kama huamini endelea kutenda dhambi na usizitubie ukijidanganya utasamehewa...

Pia nikushauri acha kuidandia biblia wakati huna ufahamu wa kutosha.
mama samahani, nilikuwa natoa ushauri. najua unaweza kuwa umejibu bila kuelewa. nasema mbele za Mungu kwamba, ushauri niliokupa ndio utakaokusaidia. biblia naifahamu vizuri sana na ndio chakula changu kila siku. sitaki kujitapa kwako kama mimi ni nani kiimani lakini jua kwamba umeongea na mtu mwenye uzoefu sana na mambo hayo. nimeshatoa ushauri watu wengi wenye tatizo kama lako. jambo ambalo halipingiki ni kwamba, Mume wako amefanya kosa kubwa sana, dhambi ya kuzini ni dhambi kubwa sana kwasababu ni dhambi inayo involve makutano ya damu/mwili/nyama. pamoja na kwamba dhambi zote ni sawa lakini madhara yake kiroho hii huwa ni makubwa zaidi.

vilevile, amini usiamini nikuambiacho, MUNGU KUMSAMEHE MTU HAIPO MIKONONI MWA MWANADAMU. hata wewe usipomsamehe mume wako, yeye akishuka mbele za Mungu, Mungu atamsamehe na ataendelea mbele na maisha, ila wewe kwasababu hautamsamehe utabaki na kinyongo na ndio mtengo shetani aliokuwekea ili kuwavuruga (kama story hii uliyoiweka ni ya kweli). kama hii story uliyoiweka ni ya kweli, najua ni vigumu sana kusamehe lakini hata ikichukua muda, jua kwamba unapaswa kusamehe ili kuendelea mbele, either with him or without him....pamoja na kwamba, nitakupa caution moja, if you decide to get back to him someday, angalia sana suala la afya, mkapime miezi mitatu bila kushiriki kwasababu kwa kipindi ambacho pengine hampo, lazima kwa mwanaume asiyemjua Mungu anaweza kutoka nje...this is my only concern....na nisingependa upate matatizo ya afya wakati haukuwa mhuni (kama kweli we ni mtakatifu na unaweza kumnyoshea mtu kidole)....

issue ya toba ya machozi, hakuna mstari hata mmoja kwenye biblia unaosema unatakiwa toba ya machozi. kutoa machozi sio ishara pekee. kinachotakiwa ni moyo wenye toba, Mungu huangalia moyo tu hata kama haujatoa machozi. kuna wanaotoa machozi lakini bado haman kitu. vilevile, kitu cha muhimu kwa mume wako ni kusamehewa na Mungu, hata wewe ukimsamehe kama Mungu hata msamehe atakuwa na dhambi ileile tu. int he contrary, wewe usipomsamehe, Mungu anaweza kumsamehe. msamaha wa Mungu haupo mikononi mwa mwanadamu. niliongea kwamba sisi sote tulikuwa huko, mimi nilikuwa mhuni...lakini leo nimejutia na nimerudi kwa Mungu na ninamwona Mungu katika maisha yangu na nilikuwa najaribu kushare story ya upande wangu pengine itakusaidia.

suala la Yuda iskariot, sio kwamba Mungu hakumpa msameha, hapana, yeye hakutubu akajinyonga, na jua kuwa MUNGU HAFURAHII KIFO CHA MWENYE DHAMBI, hakufurahia hata kifo cha yuda pida.dhambi zetu zijapokuwa nyekundu zitakuwa kama theluji,...mungu anasamehe dhambi zooote, isipokuwa dhambi moja tu ndio Mungu hatasamehe nayo ni "kumkufuru Roho Mtakatifu".

ushauri wangu kwako mara ya pili ni kwamba, mwombee Mume wako ili Mungu amfungue abadilike. ukiona mtu anatenda dhambi anaangamia, sio yeye, ni shetani anamuongoza. hivyo usimhukumu. pia, Mwombe Mungu, kwasababu kwa mazingira ninayoyaona, wewe na yeye wote hamjamjua Mungu ndio maana upo tayari kulipizana kisasi na kushindana vita...kisasi ni cha Mungu si cha mwanadamu. na katika vita zote, mshindi huwa ni shetani si either party. Mungu akusaidie, na akubariki. kuna siku utakuja kuona haya niliyoandika yalikuwa ya msingi. hata hivyo, katika hatua yeyote utakayochukua, jaribu kuforesee impact yake, hakuna product njema ambayo huwa inatoka katika maamuzi ya hasira, hasa ukiwa umekasirishwa kama ilivyo kwako. jitahidi kujizuia kutochukua hatua yeyote bila kuangalia impact; na bila kumshirikisha Mungu katika hatua zako, matokeo yake siku zote huwa ni negative. ninakupa pole lakini nashindwa nikushauri vipi zaidi ya hapo. I hope at least utapata kitu.
 
Bigbro haita kaa itokee kbsa
..kumsamehe naweza lkn si kurudiana seriously
Naomba nikuulize swali baya lakini lenye maana kubwa sana....... Utajisikiaje ukijajua baadae mdogo wako anaishi na baba mtoto wake yaani mume wako wa zamani?
 
Naomba nikuulize swali baya lakini lenye maana kubwa sana....... Utajisikiaje ukijajua baadae mdogo wako anaishi na baba mtoto wake yaani mume wako wa zamani?
Wala haitanisumbua kbsa na kuhakikishia hata kesho njoo umchukue umpelekee kbsa huo ukurasa nimesha ufunga
 
Wanaume ni watu wa kujihesabia haki sana kosa mfanye msamaha aombe mwanamke looh! Siwezi fanya ujinga huo kuolewa si utumwa...eti elimu inampa kiburi!

Mnapenda kuwa watwana ilihali majukumu yanawashinda...zama hizi ni mpya wanawake tumejitambua
 
OK dada najua umekosewa sana sawa lakini kwa kauli hizi naanza kupata mwanga ni kwa nini yote haya yametokea. Sorry nimesema naanza tu kupata mwanga just mwanga. Elimu au fedha haioi wala kuolewa
 
Back
Top Bottom