Mrejesho: Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mtoa mada anastaajabu ya Musa!!!!
Ayasubiri kuyaona ya firauni
 
Pole, Mmeo ameshaathirika kisaikolojia, ukikutana nae mwambie pole
 
Njoo nikuoe ili upate ulichopoteza, utaishi kwa amani na upendo.
Karibu
 
Habari zenu wadau wa MMU,

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru mods na members wenzangu wote kwa mawazo, ushauri na michango yenu katika thread niliyoleta huku kipindi cha nyuma yenye kichwa kisemacho "mume wangu amempa mimba mdogo wangu"

Nimepata muda wa kutosha kutafakari michango ya mawazo yenu namna ya kumaliza tatizo hili na MUNGU amekuwa upande wangu na nimefanikiwa kufikia muafaka.

Jana ndo ilikuwa siku ya kukutana tena kwenye kikao pamoja na wazazi wa pande zote mbili na safari hii tukihusisha na wachungaji wetu na tulikaa na kufikia muafaka kama ifuatavyo;

Katika kusikiliza maelezo ya pande zote mbili yaani kutoka kwangu na kwa watuhumiwa, mume wangu aliamua kujibu vibaya kikao baada ya kuona anaandamwa na maswali ambayo haya kumfurahisha.

Nasikitika kusema alidiriki kujibu kuwa kama kosa limeshatokea waamue haraka yeye ana mambo ya muhimu ya kufanya kuliko hili.

Akaenda mbali zaidi kuwa hata wao wanajiona ni watakatifu kumuandama na maswali wana nyumba ndogo kibao sema ni kwa vile hawaja kamatwa. Pamoja nahayo akaongeza kuwa hajawahi jutia kosa lake kwani yule si dada yake wala hana ukoo nae kwahiyo ilikuwa ni sawa tu.

Wazazi wake walijaribu kumkatisha asiendelee kuzungumza lkn hakujali akapaza sauti zaid hapo ikabidi wamuache tu aongee mpaka amalize, aliongea mengi na magumu sana sina ujasiri wa kuyaandika hapa kwakuwa hayatamkiki kwa mtu mwenye akili timamu.

Baada ya kumsikiliza kikao kiliniuliza nasemaje kuhusu ndoa yangu.

Sikuwa na la zaidi, niliwaambia kwakuwa kwake ni jambo la kawaida sana na mimi kwangu si la kawaida nisingeweza kuendelea kuishi na mtu mwenye mtazamo tofauti.

Wachungaji walisema wao hawana mamlaka ya kuvunja ndoa ya kikristo lakini kwakuwa mwanaume ameongea maneno yenye dharau inaonesha hana moyo wa toba na angeendelea na uzinzi hivyo wanaungana na mimi katika maamuzi yangu.
Walinishauri nifuate taratibu za kisheria kuvunja ndoa.

Kwa upande wa mdogo wangu yeye alishanifuata zaidi ya Mara kumi kuniomba msamaha, sikuona sababu ya kutomsamehe nilimsamehe na jana niliuthibitisha msamaha wangu katika kikao lakini nilimtahadharisha kutoendelea na shemeji yake nae hakupingana nami katika hilo.

Mwanaume ameanza vitisho kwamba nijiandae kupambana.
Binafsi siogopi nipo tayari kupambana lakini sipo tayari kuendelea kuishi na mwanaume fedhuli kama yeye.

Hapo ndipo tulipo fikia na najiandaa kutafuta talaka kisheria.

Asanteni sana naamini hili limepita imebaki utekelezaji wa utenguzi wa ndoa.

Nakaribisha michango yenu ya mawazo..

Pia niwashukuru kwa kampani yenu katika kipindi kigumu
Umefanya maamuzi sahihi nakupongeza sana
kuna msemo usemao "everybody is going to hurt you,you just gotta find the one who is wroth suffering for" That man is not worth kwa kwel ndio mana ametoa majibu ya dharau kiac icho na ni bora umeyajua kabla ya kuanzisha familia,
 
Dah kazi kweli kweli. Haya endelea na taratibu za kuvunja ndoa
 
Nilitaka kupita bila kusema neno kutokana na ukweli kwamba solution imepatikana. Lakini nikupongeze leah2 kwa maamuzi uliyofikia.

Nimesikitishwa tu na kiburi cha huyo mtalaka wako. Nilitaraji angekuomba radhi na ninaamini kwa convoy kubwa ya wazazi na pastors basi muafaka wenye afya ungepatikana. Ninaamini ulikuwa tayari kusahau na kusamehe. Kiburi chake, majivuno, dharau na kutokuwa na hofu ya Mungu vimemponza.

Hata sisi tuna wakosea wake zetu. Lakini tunajishusha na kuwa wanyenyekevu ili maisha na mapenzi vitamalaki. Kwenye ndoa ya mume jeuri na mke aliye kengeuka lazima vita izaliwe.

Hongera kwa busara zako za kumsamehe mdogo wako. Fungua ukurasa Mpya wa maisha yako. Mungu akutangulie katika wakati huu mgumu wa mapito. Najua maumivu haya kuisha bado itakuchukua muda. Maliza masomo yako. Omba Mungu akuletee Mume. Maisha yaendelee.

Goodluck Mshana
 
Pole tena, maisha na changamoto; usijutie uamuzi wako maana hujui Mungu amekuepusha na nini. Kama kakutisha gadharani kamripoti polisi upate RB kwa usalama wako. Fanya maisha km mume Mungu atakupa. Ungeweza kubadilisha makazi ingekuwa vizuri kiusalama na kisaikolojia. Huyo wewe hukuwa chaguo lake vinginevyo angejutia sana kosa. Ifanye kazi yako ndio mumeo usonge mbele.
 
Pole na kila la kheri katika maisha mapya... Angalau sasa mme wako ataitwa baba. Tatizo nyie wanawake mnaolewa eti mnajifanya hamtaki kuzaa sijui mpaka mmalize shule na bla bla kibao... Hii mianya ya matatizo mnaitafuta wenyewe so usimpe lawama kwa asilimia mia, na wewe una sehemu ya lawama katika jambo hili... Cha muhimu, msamehe, jisamehe na u move forward....

Mimi pia nilikuwa na mtazamo kama wako katika jambo hili, maana alitengeneza mazingira ya uovu huu kutendeka kwa kuweka masharti ambayo huenda yalikuwa kinyume na matarajio ya mwanaume, kama hujajiandaa na maisha ya ndoa usiingie kwenye ndoa.
 
kama mwanaume aliona matarajio yake yanaccheleweshwa kwanini asingezungumza na mkewe toka mwanzo wanatakiwa kukubaliana wenyewe.....kwenda kuzaa na shemeji kwa vile matarajio yao hayakufikiwa ni upuuzi haswa kosa linaoneka kwa mwanaume kutokufanya maamuzi sahihi
 
Siku hizi ukioa au ukiolewa badala ya kujiletea faraja na raha za maisha kwa kumpata mwenzio...kinyume chake unajiletea mahangaiko na mateso kwenye maisha yako......

Badala ya ndoa kuwa baraka na neema zimekuwa ni chem chem ya mabalaa na mafarakano kwenye maisha yako....

Siku hizi ukioa au kuolewa ni kama unajiweka karibu maradhi ya moyo na visukari visivyo na sababu.....au hata kifo kabisa.....

Siku hizi ndoa baada ya kujenga undugu wa karibu kwa kuunganisha familia mbili badala yake zinakuwa chanzo cha uadui baina ya familia mbili......

NDOA ZIMEKUWA NDOANO......
Na ndo ibilisi anavyopenda!
 
Habari zenu wadau wa MMU,

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru mods na members wenzangu wote kwa mawazo, ushauri na michango yenu katika thread niliyoleta huku kipindi cha nyuma yenye kichwa kisemacho "mume wangu amempa mimba mdogo wangu"

Nimepata muda wa kutosha kutafakari michango ya mawazo yenu namna ya kumaliza tatizo hili na MUNGU amekuwa upande wangu na nimefanikiwa kufikia muafaka.

Jana ndo ilikuwa siku ya kukutana tena kwenye kikao pamoja na wazazi wa pande zote mbili na safari hii tukihusisha na wachungaji wetu na tulikaa na kufikia muafaka kama ifuatavyo;

Katika kusikiliza maelezo ya pande zote mbili yaani kutoka kwangu na kwa watuhumiwa, mume wangu aliamua kujibu vibaya kikao baada ya kuona anaandamwa na maswali ambayo haya kumfurahisha.

Nasikitika kusema alidiriki kujibu kuwa kama kosa limeshatokea waamue haraka yeye ana mambo ya muhimu ya kufanya kuliko hili.

Akaenda mbali zaidi kuwa hata wao wanajiona ni watakatifu kumuandama na maswali wana nyumba ndogo kibao sema ni kwa vile hawaja kamatwa. Pamoja nahayo akaongeza kuwa hajawahi jutia kosa lake kwani yule si dada yake wala hana ukoo nae kwahiyo ilikuwa ni sawa tu.

Wazazi wake walijaribu kumkatisha asiendelee kuzungumza lkn hakujali akapaza sauti zaid hapo ikabidi wamuache tu aongee mpaka amalize, aliongea mengi na magumu sana sina ujasiri wa kuyaandika hapa kwakuwa hayatamkiki kwa mtu mwenye akili timamu.

Baada ya kumsikiliza kikao kiliniuliza nasemaje kuhusu ndoa yangu.

Sikuwa na la zaidi, niliwaambia kwakuwa kwake ni jambo la kawaida sana na mimi kwangu si la kawaida nisingeweza kuendelea kuishi na mtu mwenye mtazamo tofauti.

Wachungaji walisema wao hawana mamlaka ya kuvunja ndoa ya kikristo lakini kwakuwa mwanaume ameongea maneno yenye dharau inaonesha hana moyo wa toba na angeendelea na uzinzi hivyo wanaungana na mimi katika maamuzi yangu.
Walinishauri nifuate taratibu za kisheria kuvunja ndoa.

Kwa upande wa mdogo wangu yeye alishanifuata zaidi ya Mara kumi kuniomba msamaha, sikuona sababu ya kutomsamehe nilimsamehe na jana niliuthibitisha msamaha wangu katika kikao lakini nilimtahadharisha kutoendelea na shemeji yake nae hakupingana nami katika hilo.

Mwanaume ameanza vitisho kwamba nijiandae kupambana.
Binafsi siogopi nipo tayari kupambana lakini sipo tayari kuendelea kuishi na mwanaume fedhuli kama yeye.

Hapo ndipo tulipo fikia na najiandaa kutafuta talaka kisheria.

Asanteni sana naamini hili limepita imebaki utekelezaji wa utenguzi wa ndoa.

Nakaribisha michango yenu ya mawazo..

Pia niwashukuru kwa kampani yenu katika kipindi kigumu
Hapo mama umebomoa wala hujajenga. Na for sure nakuhakikishia hao hao waliokuunga mkono kuachana na mumeo kwa kosa ambalo tayari limeshatokea ndio hao hao watakaokusengenya kesho kwa muone huyo alishindwa kumudu nyumba yake. Kiufupi Mimi nilikuwa sitegemei mumeo angaact tofauti na alichofanya. Anyways jitahidi mahakamani kuvunja ndoa ili uweze kuwaunganisha kisheria mumeo na mdogo wako.
 
Waweza kuwa mdhaifu na Ni kitu kigumu Ila huu ndo ukombozi wako usirudi nyuma. Jitahidi asimshawishi Mdogo wako wakaishi naye Ila Hilo nako laweza tokea Ila usirudi nyuma.

Habari zenu wadau wa MMU,

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru mods na members wenzangu wote kwa mawazo, ushauri na michango yenu katika thread niliyoleta huku kipindi cha nyuma yenye kichwa kisemacho "mume wangu amempa mimba mdogo wangu"

Nimepata muda wa kutosha kutafakari michango ya mawazo yenu namna ya kumaliza tatizo hili na MUNGU amekuwa upande wangu na nimefanikiwa kufikia muafaka.

Jana ndo ilikuwa siku ya kukutana tena kwenye kikao pamoja na wazazi wa pande zote mbili na safari hii tukihusisha na wachungaji wetu na tulikaa na kufikia muafaka kama ifuatavyo;

Katika kusikiliza maelezo ya pande zote mbili yaani kutoka kwangu na kwa watuhumiwa, mume wangu aliamua kujibu vibaya kikao baada ya kuona anaandamwa na maswali ambayo haya kumfurahisha.

Nasikitika kusema alidiriki kujibu kuwa kama kosa limeshatokea waamue haraka yeye ana mambo ya muhimu ya kufanya kuliko hili.

Akaenda mbali zaidi kuwa hata wao wanajiona ni watakatifu kumuandama na maswali wana nyumba ndogo kibao sema ni kwa vile hawaja kamatwa. Pamoja nahayo akaongeza kuwa hajawahi jutia kosa lake kwani yule si dada yake wala hana ukoo nae kwahiyo ilikuwa ni sawa tu.

Wazazi wake walijaribu kumkatisha asiendelee kuzungumza lkn hakujali akapaza sauti zaid hapo ikabidi wamuache tu aongee mpaka amalize, aliongea mengi na magumu sana sina ujasiri wa kuyaandika hapa kwakuwa hayatamkiki kwa mtu mwenye akili timamu.

Baada ya kumsikiliza kikao kiliniuliza nasemaje kuhusu ndoa yangu.

Sikuwa na la zaidi, niliwaambia kwakuwa kwake ni jambo la kawaida sana na mimi kwangu si la kawaida nisingeweza kuendelea kuishi na mtu mwenye mtazamo tofauti.

Wachungaji walisema wao hawana mamlaka ya kuvunja ndoa ya kikristo lakini kwakuwa mwanaume ameongea maneno yenye dharau inaonesha hana moyo wa toba na angeendelea na uzinzi hivyo wanaungana na mimi katika maamuzi yangu.
Walinishauri nifuate taratibu za kisheria kuvunja ndoa.

Kwa upande wa mdogo wangu yeye alishanifuata zaidi ya Mara kumi kuniomba msamaha, sikuona sababu ya kutomsamehe nilimsamehe na jana niliuthibitisha msamaha wangu katika kikao lakini nilimtahadharisha kutoendelea na shemeji yake nae hakupingana nami katika hilo.

Mwanaume ameanza vitisho kwamba nijiandae kupambana.
Binafsi siogopi nipo tayari kupambana lakini sipo tayari kuendelea kuishi na mwanaume fedhuli kama yeye.

Hapo ndipo tulipo fikia na najiandaa kutafuta talaka kisheria.

Asanteni sana naamini hili limepita imebaki utekelezaji wa utenguzi wa ndoa.

Nakaribisha michango yenu ya mawazo..

Pia niwashukuru kwa kampani yenu katika kipindi kigumu
 
leah2, wakati wa kikao, kabla mumeo hajaanza kutema pumba, ulishafanya maamuzi yoyote? Je, kama angekupigia magoti kuomba umsamehe, ungekubali? (Napenda kujua nini uliwaza though yameshatokea)

Pole sana, ndoa yaweza kuwa mbingu ndogo, lakini pia yaweza kuwa jehanamu.
 
Back
Top Bottom