Mrejesho; Matibabu India. Tumenusurika kutapeliwa

Mrejesho; Matibabu India. Tumenusurika kutapeliwa

Mkuu umefanya jambo la muhimu sana umeongea na kuonyesha watu wanavyotapeliwa najua kuna watanzania wengi wametapeliwa na hata wengine kupoteza maisha lakini hawajasema. Ushauri wangu kwa vyombo vya habari nchi magazeti, radio na tv wajikite kufanya habari za uchunguzi ili kutusaidia watanzania. Mkuu natumaini mgonjwa wako atapata nafuu mapema kila la kheri.
 
Hongera na asante kwa mrejesho mahsusi, utawasaidia wengi in future
 
Ni Mil 8 ya dawa pekee, tena nilienda kununua mjini kufuata punguzo. Ni dawa kali na za kutumia muda mrefu. Huwezi amini dawa hizo hizo hapa Tz ni zaidi ya 40 mil.
....aisee kama kweli Mungu yupo,
..mi sina dhambi kaaabisa!!!
 
Usijali kaka. Nia ni kusaidiana. Nilipata huduma Gleneagles Global Hospitals, Bangalore. Nilijifunza mengi hapo ikiwa ni pamoja na kukwepa gharama ambazo si za lazima.
Mkuu nipe contact zao kuna ndugu yangu anataka kwenda huko
 
Habari wakuu.

Napenda kutoa shukrani kwa wana JF wenzangu waliojitoa kunishauri katika ombi langu nililolitoa mwezi januari mwaka huu katika uzi huu msaada hospitali nzuri ya kansa nchini india. Wapo walionishauri kwenye thread na wengine PM. Wote asanteni.

Pamoja na shukrani, nia ya uzi huu ni kueleza changamoto nilizokumbana nazo ili walau mtu mwingine ambaye hana mwanga juu ya matibabu nchini India asije kuzipitia.

Kabla ya kuomba ushauri hapa nilikuwa nimeshatafuta mwenyewe Hospitali kadhaa na nilikuwa nimeshapokea makadirio ya gharama ya matibabu ya hospitali hizo. Hospitali nyingi zilikuwa ngeni masikioni mwangu hivyo nilizihofia ubora wake na kubaki na dhana kuwa Hospitali nzuri na kubwa India ni ile wanayopenda kwenda kutibiwa viongozi wetu.

Nilipokea pia makadirio yao ambayo hayakuwa ya kutisha sana japo tayari nilikuwa nimeshapewa angalizo hapa JF kuwa wana tabia ya kutaja kiasi kidogo halafu ukishafika kule wanabadirika. Nikiwa nawaza hilo akatokea mgonjwa anayetaka kwenda moja ya Hosp zao na alipewa makadirio ya Dollar 15,000 na yeye akabeba Dolla 20,000 ili awe na ziada. Nikaona huyo nimuache atangulie halafu then atakuwa ananipa mrejesho kama ni kweli. Basi wiki ya kwanza tu Dollar 20,000 zote zikaisha, hadi wiki ya tatu akawa katumia dollar 40,000. Ikawa ndugu wanauza vitu wanamtumia fedha. Hii ilinitisha na nikaghairi kwenda huko.

Nikiwa sijui la kufanya, akatokea msamaria mwema akanishauri niende Hospitali flani Dar Es Salaam kuwa kuna daktari atanisaidia kuniunganisha na hospitali nzuri na nafuu. Nikamuona huyo Dr, akaniunganisha na hospitali hiyo huku akinihakikishia kuwa wana gharama nafuu sana na ni waaminifu sana, kwamba ni kama taasisi ya dini inayotoa msaada.

Tukaondoka kwenda India. Tukapokelewa airport na watu wa “Hospitali” hiyo. Ile kufika hospitalini kwao tukashangaa kukuta ni kama dispensary. Kuna vyumba vinne tu vya kulaza wagonjwa. Kuna mgonjwa mmoja tu tena Mtanzania aliyeelekezwa na dokta huyo huyo aliyetuelekeza sisi. Ana wiki tatu, hajatibiwa bali anasubiri majibu ya vipimo. Kumbe hako ka dispensary wanafanya udalali. Ukishawatajia ugonjwa, wanaenda hospitali kubwa kutafuta Dr wa tatizo hilo then akiandika vipimo wanakuchukua na kukupeleka Diagnostic Centre mahali kwingine then unapima halafu unarudishwa kwenye kituo chao kusubiri majibu. Siku ya operation huyo Dr anakuja kukufanyia kwenye hako kakituo then unamlipa hela yake na baada ya hapo unalipa gharama zote za kukuhudumia baada ya operation. So kama uanatakiwa kuonwa na madaktari tofauti itabidi waitwe kwa style hii hii au utibiwe nusu.

Mwenyeji wetu alitushauri tuchague chumba kati ya vitatu vilivyobaki na kila chumba ni karibu laki 2 kwa siku na kwamba haturusiwi kukaa nje ya hospitali. Tulibishana hadi usiku wa manane. Katikati ya ubishi wetu akaja Dr waliyetuandalia akatupa treatment plan yake. Ikawa ni ghali sana ukijumuisha na gharama za kukaa pale. Tulikataa.

Kufupisha habari, baada ya hekaheka zote, siku ya pili tukafanikiwa kutoroka pale japo kwa shida na ikawa ni risk sana. Nikampa address mtu wa bajaji (wanaita Auto) atupeleke Hospitali nyingine ambayo tuliwasiliana nayo kabla hatujaondoka Tanzania, ila hatukuwa na nia nayo. Tuliamua kukimbilia hapo kwa sababu ndio hospitali ilikuwa mji tuliokwenda so hatukuwa na choice. Mungu mkuu, tukakuta ni kubwa sana, Multi-specialty, wamejipanga kila idara. Gharama ni nafuu sana na tukatafutiwa nyumba ya kupanga jirani na hospitali na kila siku wanatufata na gari na kuturudisha. Gharama ya matibabu ni kwa package na ukishalipa hakuna cha ziada, unasubiri tu kukabidhiwa mgonjwa wako baada ya matibabu. Wana huduma nzuri sana. Kama bei hujaiafiki unaweza omba wakapunguza kidogo. Kwa kweli mgonjwa wangu alitibiwa vizuri, haraka na kwa gharama nafuu sana tofauti na watu walivyokuwa wananitisha habari za milioni 50 hadi 70 kabla ya kuondoka.

Nilichojifunza

1. Watu wengi hatuna taarifa sahihi juu ya matibabu India so baadhi ya madaktari hapa nchini wanageuka madalali na hata kuingiza watu matatizoni ili mradi kuna kitu wanapata.

2. Wenzetu wako juu sana kimatibabu na teknolojia na gharama wakati mwingine ni za kawaida sana japo ukiingia kichwa kichwa utaliwa.

3. Kuna hospitali nyingi na nzuri sana ila hazina majina huku kwetu. Bahati mbaya hospitali inayofahamika huku kwetu hawaaminiki tena. Gharama zao ziko juu na bado wanabambikiza bill. Wanatumia umaarufu wao vibaya.

4. Vipo vingi vinavyochangia gharama ya matibabu kuwa kubwa. Malazi huchangia sana so ni bora kuhakikisha Hospitali inakutafutia nyumba nafuu mapema kabla ya safari.

5. Dawa katika pharmacy za hosp ni ghali kuliko mtaani so ni bora unapaondikiwa dawa za gharama ukanunue pharmacy kubwa mjini coz wanatoa punguzo la bei ukiomba. Wakati mwingine hata nusu bei unauziwa.

6. Chakula ni changamoto kubwa, vyakula vyao ni tofauti kabisa. Hivyo ni vyema kusafiri na unga, mchele, na maharagwe kama mnapendelea. Vitu hivyo havipatikani kabisa. Vyakula vingine vyote bei ni kama hapa hapa Tanzania.

Narudia tena kuwashukuru wote walionichangia mawazo na mimi nimeona nitoe mrejesho ili uwe mwanga kwa wengine. Asanteni wana JF.
Naomba kuwasilisha
"Huyu jamaa siyo mkweli, hamna mambo kama hayo. Kuondoka Tz lazima uwe na viza ambayo pia utaipata baada ya kupewa invitation for medical care in India from a recognized institution, nao pia hawawezi kukupa invitation bila kupata proper medical history lab. Radiology reports from a recognized medical practitioner or hospital. Sasa huyu jamaa aliendaje? Mji alioenda, Bangalore ni moja kati ya majiji yaliyostaarabika India, kwanza hakuna vidispensary, huyo angesema huku Gujarat au Mumbai ningemuelewa kidogo.
Ni muongo, nina wasiwasi kama amewahi kufika India. Kuhusu gharama ni kweli, wakati mwingine wanakadiria chini, ila ikiwa gharama ni tofauti sana ukiwashupalia hawatakudai zaidi ya budget, lakini wewe mwenyewe unapima na huduma ulizopewa, unaamua kulipa, hawawezi kukupa exact. Mbona sisi tumerudishiwa dola 600 zilizozidi kwenye advance tuliyotoa?
Hakuna wizi kama bongo hata kidogo. Kuhusu Hospital zenye majina makubwa kuwa na huduma mbovu ni kweli kwani sisi tuko Apollo, ni kubwa sana, huduma zile specialized ni nzuri sana, shida ni huduma ndogo ndogo kwa manesi na wahudumu hazivutii saana, ila kwa vyovyote, wako vizuri kuliko sisi. Tunatakiwa tupambane sana kuweza kufika robo ya hawa jamaa. Mgonjwa wangu alitibiwa Regency na Muhimbili kwa jumla ya siku 21 na hakupata huduma inayoeleweka.
Tuliondoka Dar tar 28/4 tukafika asubuhi 29/4 Apollo, tulipokewa Airport moja kwa moja hadi Hospital. Vipimo vyote vilianza immediately na kufika saa mbili usiku treatment plan tayari kesho yake asubuhi saa 1.30 aliingizwa Theater. Wako makini sana kuhakikisha hukai siku nyingi hasa unapokuwa foreigner. Sasa huyu anayejiita mkuu sijui alienda nchi gani, labda Afghanistan. Waforwadie hii testimony yangu please, wasiogopeshwe."
 
Hoja ya msingi hapa siioni. Suala la visa ni kweli moja ya vigezo ni invitation letter. Na si kweli kuwa hosp inatoa invitation letter kwa mtu aliyewatumia reports tu. Vipi mtu akipenda kwenda kufanya body check up, anatuma report gani? Aache kukariri. Invitation letter inatolewa wakati wowote unapoihitaji baada ya kuwasiliana na hosp. Na wanazituma haraka ili uharakishe kwenda. Ukitaka jaribu kuwasiliana na hosp yoyote India uwaambie una mgonjwa tatizo fulani ila hana reports uone kama watamkataa.

Pia, ni wapi nilipozungumzia kuwa hosp kubwa kama Apollo zina huduma mbovu?

Na kuhusu Bangalore kuwa na ustaarabu tu si kweli. Bangalore ni kama zilivyo sehemu nyingine duniani..wastaarabu wapo, madalali wapo, wezi, walevi n.k. Na pia kuna vihospitali vingi vidogo vyenye hadhi ya chini kuliko hata hosp zetu na ukiwasiliana nao kila ugonjwa wanajifanya wanatibu kumbe wanasubiri ufike wakutafutie Dr. Ni kweli utatibiwa japo unaweza usitibiwe kikamilifu ila pesa ya maana itakutoka maana kila upande utataka ule.

Nia yangu ni kuwapa tahadhari wana JF wenzangu, wajue usanii upo. Najua mnaofanya biashara hizi mtakasirika.
 
Mkuu umefanya jambo la muhimu sana umeongea na kuonyesha watu wanavyotapeliwa najua kuna watanzania wengi wametapeliwa na hata wengine kupoteza maisha lakini hawajasema. Ushauri wangu kwa vyombo vya habari nchi magazeti, radio na tv wajikite kufanya habari za uchunguzi ili kutusaidia watanzania. Mkuu natumaini mgonjwa wako atapata nafuu mapema kila la kheri.
Ni kweli mkuu. Watu wengi hawajui mambo haya na wakati mwingine ukifika huko ukadalaliwa unadhani kuwa ndio utaratibu...unabaki unaugulia maumivu. Wengi wanadhani kuwa ni kama huku Tz kuwa Dr mzuri hadi umsubiri hospitali flani ndogo ya pembeni so ukidalaliwa unaona kama umesaidiwa.
 
Kwa vile umeamua kuwasaidia Watu kwa moyo.. na kwa vile yule doctor wa kibongo alikuwa anacheza na maisha ya mgonjwa wako... Ni vizuri ufanye editing ya hii taarifa ukaweka jina la huyo doctor na jina la hiyo dispensary uliyoenda I'li Watu wajue na wajifunze.... Otherwise taarifa yako imekuwa kama wa wabunge wa ccm... Wale wanafiki.....
Mkuu mi naona jamaa anaogopa mashindano ya kuchafuana mtandaoni kwani huyo dr akimtaja naye atakuja hapa kujitetea , kwa kutaja hospital aliyopata huduma amesaidia watu pia
 
Mkuu mi naona jamaa anaogopa mashindano ya kuchafuana mtandaoni kwani huyo dr akimtaja naye atakuja hapa kujitetea , kwa kutaja hospital aliyopata huduma amesaidia watu pia
Ni kweli mkuu. Na anaweza asije hapa ila akanifanyizia pembeni. Heri nusu shari...
 
Hivi kwanini watu hawafikirii kwenda uchina au thailand
 
poleni sana la msingi zaidi kama mgonjwa amepata matibabu na anaendelea vizuri na jambo la heri.

Kusamehe pia ni kupona kama umeshawasamehe wote waliotaka kukuingiza mkenge ni vyema na pia umefanya jambo la maana kuwaambia ukweli
Ni kweli mkuu. Kusamehe nayo ni dawa. Kikubwa ni tahadhari kwa ajili ya siku za usoni.
 
Back
Top Bottom