Habari wakuu.
Napenda kutoa shukrani kwa wana JF wenzangu waliojitoa kunishauri katika ombi langu nililolitoa mwezi januari mwaka huu katika uzi huu msaada hospitali nzuri ya kansa nchini india. Wapo walionishauri kwenye thread na wengine PM. Wote asanteni.
Pamoja na shukrani, nia ya uzi huu ni kueleza changamoto nilizokumbana nazo ili walau mtu mwingine ambaye hana mwanga juu ya matibabu nchini India asije kuzipitia.
Kabla ya kuomba ushauri hapa nilikuwa nimeshatafuta mwenyewe Hospitali kadhaa kupitia google na nilikuwa nimeshapokea makadirio ya gharama ya matibabu ya hospitali hizo. Hospitali nyingi zilikuwa ngeni masikioni mwangu hivyo nilizihofia ubora wake na kubaki na dhana kuwa Hospitali nzuri na kubwa India ni zile wanazokwenda kutibiwa viongozi wetu.
Nao pia niliwachek, nikapokea pia makadirio yao ambayo hayakuwa ya kutisha sana japo tayari nilikuwa nimeshapewa angalizo hapa JF kuwa wana tabia ya kutaja kiasi kidogo cha makadirio ya matibabu (cost estimate) halafu ukishafika kule gharama inabadilika mara dufu.
Nikiwa sijui la kufanya, akatokea msamaria mwema (ndugu) akanishauri nimtafute daktari fulani atanisaidia kuniunganisha na hospitali nzuri na nafuu, hata yeye kuna kipindi alishamsaidia (ni kweli alishauguliwa na mtoto). Nikamuona huyo Dr, kuna hospitali akaniunganisha nayo huku akinihakikishia kuwa wana gharama nafuu sana na ni waaminifu sana, kwamba ni kama taasisi ya dini inayotoa msaada. Nikakubali ila nikawa na mashaka coz nimemuomba mawasiliano yao, ananizungusha tu. Anaongea nao yeye tu. Jina hanitajii. Nikamuomba jina akanipa. Nilijaribu kuwasechi mtandaoni siwaelewi. Nikimuuliza Dr ananiambia usijali. Wako vizuri.
Basi, tukaondoka kwenda India. Tukapokelewa airport na watu wa hiyo “hospitali”. Ile kufika hospitalini kwao tukashangaa kukuta ni kama dispensary, jengo dogo (kwa upana) kama la ghorofa nne. Kuna vyumba vinne tu vya kulaza wagonjwa. Kuna mgonjwa mmoja tu tena Mtanzania aliyeelekezwa na dokta huyo huyo aliyetuelekeza sisi. Ana wiki tatu, hajatibiwa bali anasubiri majibu ya vipimo. Kumbe hako ka dispensary wanafanya udalali. Ukishawatajia ugonjwa, wanakwambia wanatibu then wanaenda hospitali kubwa kutafuta Dr wa tatizo hilo then akiandika vipimo wanakuchukua na kukupeleka Diagnostic Centre mahali kwingine, unapima halafu unarudishwa kwenye kituo chao kusubiri majibu. Siku ya operation huyo Dr anakuja kukufanyia kwenye hako kakituo, unamlipa hela yake na baada ya hapo unalipa gharama zote za kukuhudumia baada ya operation + gharama za chumba. So kama unatakiwa kuonwa na madaktari tofauti itabidi waitwe kwa style hii hii au utibiwe nusu.
Mwenyeji wetu wa hiyo hosp ndogo alitushauri tuchague chumba kati ya vitatu vilivyobaki na kila chumba ni karibu laki 2 kwa siku na kwamba haturusiwi kukaa nje ya hospitali. Tulibishana hadi usiku wa manane. Katikati ya ubishi wetu akaitwa Dr waliyetuandalia, akatupa treatment plan yake. Ikawa ni ghali sana ukijumuisha na gharama za kukaa pale. Tulikataa.
Kufupisha habari, baada ya hekaheka zote, siku ya pili tukafanikiwa kutoroka pale japo kwa shida na ikawa ni risk sana. Nikampa address mtu wa bajaj (wanaita Auto) atupeleke Hospitali nyingine ambayo tuliwasiliana nayo kabla hatujaondoka Tanzania, ila hatukuwa na nia nayo. Tuliamua kukimbilia hapo kwa sababu ndio hospitali ilikuwa mji tuliokwenda so hatukuwa na choice. Mungu mkuu, tukakuta ni kubwa sana, Multi-specialty, wamejipanga kila idara. Gharama ni nafuu na bado nikaomba punguzo kidogo, na tukatafutiwa nyumba ya kupanga jirani na hospitali, baada ya operatin tukahamia mtaani. Kila siku wanatufata na gari na kuturudisha. Gharama ya matibabu ni kwa package na ukishalipa hakuna cha ziada, unasubiri tu kukabidhiwa mgonjwa wako baada ya matibabu. Wana huduma nzuri sana. Kwa kweli mgonjwa wangu alitibiwa vizuri, haraka na kwa gharama nafuu.
Nilichojifunza
1. Wenzetu wako juu sana kimatibabu na teknolojia na gharama wakati mwingine ni za kawaida sana japo ukiingia kichwa kichwa utaliwa.
2.Kuna hospitali nyingi na nzuri sana ila hazina majina huku kwetu.
3. Vipo vingi vinavyochangia gharama ya matibabu kuwa kubwa. Malazi huchangia sana so ni bora kuhakikisha Hospitali inakutafutia nyumba nafuu mapema kabla ya safari.
4. Dawa katika pharmacy za hosp ni ghali kuliko za mtaani so ni bora unapaondikiwa dawa za gharama ukanunue pharmacy kubwa mjini coz wanatoa punguzo la bei ukiomba. Wakati mwingine hata nusu bei unauziwa.
5. Chakula ni changamoto kubwa, vyakula vyao ni tofauti kabisa. Hivyo ni vyema kusafiri na unga, mchele, na maharagwe kama mnapendelea. Vitu hivyo vinapatikana ila radha yake haieleweki. Vyakula vingine vyote bei ni kama hapa hapa Tanzania.
Narudia tena kuwashukuru wote walionichangia mawazo. Asanteni wana JF.