Mrejesho; Matibabu India. Tumenusurika kutapeliwa

Mrejesho; Matibabu India. Tumenusurika kutapeliwa

Hongera sana kwa kufanikisha matibabu.
1. Hivi si tuna ubalozi India? Kwanini wasingesaidia katika hili (kutafuta hospitali na malazi) au hairuhusiwi?
2. Pia kama ungeweza ungetaja jna la hiyo hospital ingesaidia wengine pia.
3. Huyo Dr aliyukuingiza chaka ungemtaja tu ni wizi huu.
Assnte mkuu.
1. Ubalozi wana msaada sana ukiwatumia. Kabla sijaondoka niliwaomba msaada. Waliniunganisha na hosp ila ikawa ghali sana. Kuhusu malazi, hawaandai wao, ni mwenyeji wako(hosp) unayokwenda ndio wanaandaa.
2. Jina la ni Gleneagles Global Hospitals, Bangalore.
3. Mkuu, aliyenipeleka kwa huyo Dr ni mtu tunaheshimiana sana na alifanya kwa nia njema. Niliporudi nilimshtakia yule aliyenipeka kwa Dr. Alimsema sana. Dr aliomba msahama kuwa yeye hakuwa anajua mchezo wao na hajawahi kwenda huko so yaishe. Kwa uzi huu najua ameshanijua. Nisingependa kuingia matatizoni nae.
 
Pole na hongera kwa Mungu kukjalia kupata matibabu.
Huyo Dr aliyukuingiza chaka ungemtaja tu ni wizi huu. Chukua anonymity ya hapa kumtaja please na ni wa hospitali gani.
Asante mkuu. Hapana siwezi mtaja coz kwa uzi huu tu ameshanijua. Nilimshamshatakia kwa mtu alinenipeleka kwake na kesi ikaisha. Aliomba radhi. Ila pia niliporudi nilienda wizarani kuwasimulia yote haya.
 
Hongera sana ila hujatuambia kuhusu mgonjwa wako anaendeleaje na vipi kuhusu hiyo hosp aliyotibiwa jina lake na kama ina ithibati ya kimataifa
Asante mkuu. Mgonjwa yuko vizuri. Anafanya shughuli zake kama kawaida. Tunasubiri check up tu. Ni Gleneagles Global hospitals mkuu.
 
Asante mleta mada na pole sana kwa kuuguza. Mimi naamini ukitaka huduma siku hizi kama nje ya nchi ambako hakufikiki kirahisi kwanza anza na google. Fanya search. Tafuta information. Ukishaona hata website haijisomi kuwa makini zaidi.

Kama walivyosema wengine, hizi ndo zingekuwa kazi mojawapo za mabalozi wetu. Wanachukua information kama hizi wanaziweka kwenye ubalozi. Mtu akizihitaji basi anajua pa kuanzia.

Swali tofauti: Hivi Tanzania ni insurance company gani unaweza kuitumia kutibiwa nje ya nchi. Yaani wanatoa package nzuri?

Maana siku hizi naona waTanzania wengi tunakata insurance kutimiza matakwa ya sheria na mwisho wa siku hazitusaidii especially tukihitaji matibabu zaidi nje ya nchi. Mwisho wa siku mtu unaanza kuuza asset ili uweze kuokoa uhai wa mpendwa wako.
 
Asante mkuu. Ni kweli utafiti wa kutosha ni muhimu. Mimi nilianza kupata mashaka hata kabla ya kuondoka ila aliyeniunganisha akawa ananiambia kuwa nisihofu. So nikashindwa kuhoji zaidi kwa kuwa naona kama nasaidiwa.

Kuhusu insurance za hapa kwetu sina hakika japo niliona baadhi ta wagonjwa hasa wa kutoka uarabuni wanatumia.
 
Pole sana kwa kuuguza!

Jf ipo kufichua watu kama hao, ni vema tuweke wazi ni hospital na dr yupi anajihusisha na kupeleka watanzania tena wenye shida kwa matapeli!
Mtaje hapa mkuu
 
Habari wakuu.

Napenda kutoa shukrani kwa wana JF wenzangu waliojitoa kunishauri katika ombi langu nililolitoa mwezi januari mwaka huu katika uzi huu msaada hospitali nzuri ya kansa nchini india. Wapo walionishauri kwenye thread na wengine PM. Wote asanteni.

Pamoja na shukrani, nia ya uzi huu ni kueleza changamoto nilizokumbana nazo ili walau mtu mwingine ambaye hana mwanga juu ya matibabu nchini India asije kuzipitia.

Kabla ya kuomba ushauri hapa nilikuwa nimeshatafuta mwenyewe Hospitali kadhaa na nilikuwa nimeshapokea makadirio ya gharama ya matibabu ya hospitali hizo. Hospitali nyingi zilikuwa ngeni masikioni mwangu hivyo nilizihofia ubora wake na kubaki na dhana kuwa Hospitali nzuri na kubwa India ni ile wanayopenda kwenda kutibiwa viongozi wetu.

Nilipokea pia makadirio yao ambayo hayakuwa ya kutisha sana japo tayari nilikuwa nimeshapewa angalizo hapa JF kuwa wana tabia ya kutaja kiasi kidogo halafu ukishafika kule wanabadirika. Nikiwa nawaza hilo akatokea mgonjwa anayetaka kwenda moja ya Hosp zao na alipewa makadirio ya Dollar 15,000 na yeye akabeba Dolla 20,000 ili awe na ziada. Nikaona huyo nimuache atangulie halafu then atakuwa ananipa mrejesho kama ni kweli. Basi wiki ya kwanza tu Dollar 20,000 zote zikaisha, hadi wiki ya tatu akawa katumia dollar 40,000. Ikawa ndugu wanauza vitu wanamtumia fedha. Hii ilinitisha na nikaghairi kwenda huko.

Nikiwa sijui la kufanya, akatokea msamaria mwema akanishauri niende Hospitali flani Dar Es Salaam (jina nalihifadhi) kuwa kuna daktari atanisaidia kuniunganisha na hospitali nzuri na nafuu. Nikamuona huyo Dr, akaniunganisha na hospitali hiyo huku akinihakikishia kuwa wana gharama nafuu sana na ni waaminifu sana, kwamba ni kama taasisi ya dini inayotoa msaada.

Tukaondoka kwenda India. Tukapokelewa airport na watu wa “Hospitali” hiyo. Ile kufika hospitalini kwao tukashangaa kukuta ni kama dispensary. Kuna vyumba vinne tu vya kulaza wagonjwa. Kuna mgonjwa mmoja tu tena Mtanzania aliyeelekezwa na dokta huyo huyo aliyetuelekeza sisi. Ana wiki tatu, hajatibiwa bali anasubiri majibu ya vipimo. Kumbe hako ka dispensary wanafanya udalali. Ukishawatajia ugonjwa, wanaenda hospitali kubwa kutafuta Dr wa tatizo hilo then akiandika vipimo wanakuchukua na kukupeleka Diagnostic Centre mahali kwingine then unapima halafu unarudishwa kwenye kituo chao kusubiri majibu. Siku ya operation huyo Dr anakuja kukufanyia kwenye hako kakituo then unamlipa hela yake na baada ya hapo unalipa gharama zote za kukuhudumia baada ya operation. So kama uanatakiwa kuonwa na madaktari tofauti itabidi waitwe kwa style hii hii au utibiwe nusu.

Mwenyeji wetu alitushauri tuchague chumba kati ya vitatu vilivyobaki na kila chumba ni karibu laki 2 kwa siku na kwamba haturusiwi kukaa nje ya hospitali. Tulibishana hadi usiku wa manane. Katikati ya ubishi wetu akaja Dr waliyetuandalia akatupa treatment plan yake. Ikawa ni ghali sana ukijumuisha na gharama za kukaa pale. Tulikataa.

Kufupisha habari, baada ya hekaheka zote, siku ya pili tukafanikiwa kutoroka pale japo kwa shida na ikawa ni risk sana. Nikampa address mtu wa bajaji (wanaita Auto) atupeleke Hospitali nyingine ambayo tuliwasiliana nayo kabla hatujaondoka Tanzania, ila hatukuwa na nia nayo. Tuliamua kukimbilia hapo kwa sababu ndio hospitali ilikuwa mji tuliokwenda so hatukuwa na choice. Mungu mkuu, tukakuta ni kubwa sana, Multi-specialty, wamejipanga kila idara. Gharama ni nafuu sana na tukatafutiwa nyumba ya kupanga jirani na hospitali na kila siku wanatufata na gari na kuturudisha. Gharama ya matibabu ni kwa package na ukishalipa hakuna cha ziada, unasubiri tu kukabidhiwa mgonjwa wako baada ya matibabu. Wana huduma nzuri sana. Kama bei hujaiafiki unaweza omba wakapunguza kidogo. Kwa kweli mgonjwa wangu alitibiwa vizuri, haraka na kwa gharama nafuu sana tofauti na watu walivyokuwa wananitisha habari za milioni 50 hadi 70 kabla ya kuondoka.

Nilichojifunza

1. Watu wengi hatuna taarifa sahihi juu ya matibabu India so baadhi ya madaktari hapa nchini wanageuka madalali na hata kuingiza watu matatizoni ili mradi kuna kitu wanapata.

2. Wenzetu wako juu sana kimatibabu na teknolojia na gharama wakati mwingine ni za kawaida sana japo ukiingia kichwa kichwa utaliwa.

3. Kuna hospitali nyingi na nzuri sana ila hazina majina huku kwetu. Bahati mbaya hospitali inayofahamika huku kwetu hawaaminiki tena. Gharama zao ziko juu na bado wanabambikiza bill. Wanatumia umaarufu wao vibaya.

4. Vipo vingi vinavyochangia gharama ya matibabu kuwa kubwa. Malazi huchangia sana so ni bora kuhakikisha Hospitali inakutafutia nyumba nafuu mapema kabla ya safari.

5. Dawa katika pharmacy za hosp ni ghali kuliko mtaani so ni bora unapaondikiwa dawa za gharama ukanunue pharmacy kubwa mjini coz wanatoa punguzo la bei ukiomba. Wakati mwingine hata nusu bei unauziwa.

6. Chakula ni changamoto kubwa, vyakula vyao ni tofauti kabisa. Hivyo ni vyema kusafiri na unga, mchele, na maharagwe kama mnapendelea. Vitu hivyo havipatikani kabisa. Vyakula vingine vyote bei ni kama hapa hapa Tanzania.

Narudia tena kuwashukuru wote walionichangia mawazo na mimi nimeona nitoe mrejesho ili uwe mwanga kwa wengine. Asanteni wana JF.
JF is where we dare to talk openly.
Ni muhimu sana na kwa manufaa ya umma ukamtaja huyo daktari tapeli na hospitali yake tapeli ya huko India.
Pia utaje jina la hiyo hospitali nzuri uliyopata matibabu yake.
Usipofanya hivo, mbali na kuwaweka wenzio katika hatari ya kutapeliwa, wewe pia unaweza onekana tapeli kwa kupiga promo hospitali (isiyo na jina) afu watu wakikufuata uwafanyie udalali.
Hivyo funguka mkuu. Ni muhimu sana.
 
Mkuu panda mlima.....wa posts. Mbona Kiongozi keshalitaja hilo jina la hiyo hospital zaidi ya mara tatu?

Again, kuhusu jina la Daktari, nadhani ameshasema kwa nini hayuko comfortable kutaja majina. Nashauri ingia PM mtete. Utalipata jina la muhusika.
 
Roughly ulitumia sh ngapi kwa gharama zote ( matibabu, kula, kulala na usafiri kwa mgonjwa na mhudumu)?
 
Roughly ulitumia sh ngapi kwa gharama zote ( matibabu, kula, kulala na usafiri kwa mgonjwa na mhudumu)?
Jumla ilifika mil 22. Nauli mil 3, vipimo laki 8, upasuaji mil 8 (ijumuisha chakula kwa sisi wawili, dawa na huduma zote mgonjwa akiwa wodini n.k), dawa za kutumia tutakaporudi Tanzania mil 8, nyumba mtaani mil 1.1, ni kiasi kilichobaki kwa ajili ya chakula tulichokuwa tunajipikia mtaani na mambo madogo madogo. Tuligundua gharama ingeshuka sana kama tungekataa ward tuliyopangiwa. Uchaguzi wa ward unabadirisha sana gharama.
 
Jumla ilifika mil 22. Nauli mil 3, vipimo laki 8, upasuaji mil 8 (ijumuisha chakula kwa sisi wawili, dawa na huduma zote mgonjwa akiwa wodini n.k), dawa za kutumia kutumia tutakaporudi Tanzania mil 8, nyumba mtaani mil 1.1, ni kiasi kilichobaki kwa ajili ya chakula tulichokuwa tunajipikia mtaani na mambo madogo madogo. Tuligundua gharama ingeshuka sana kama tungekataa ward tuliyopangiwa. Uchaguzi wa ward unabadirisha sana gharama.
Asante Mkuu.
Hapo mwisho sijakuelewa vizuri ni kwamba Kwa maana nyingine mngekaa wardini mlikopangiwa gharama ingekuwa chini ya hapo?
 
MKuu hizo dawa za kuja kutumia nyumbani nazo ni million 8? Au ilikuwa kwenye ile million 8 za mwanzo?
 
Asante Mkuu.
Hapo mwisho sijakuelewa vizuri ni kwamba Kwa maana nyingine mngekaa wardini mlikopangiwa gharama ingekuwa chini ya hapo?
Maana yangu ni kuwa. Kuna suite wards, hii inakuwa ni mgonjwa mmoja na ina jiko na sebule na kila kitu unapewa. Private na semi private wards, hizi unapewa chakula na vinywaji (prvt mgonjwa mmoja na semi wagonjwa wawili japo kuna partition ya pazia kubwa), nako unapewa chakula na vinywaji kadili utakavyo na kitanda cha pembeni cha ndugu. General ward ina vitanda kama 10 hivi, ni kuzuri sana na kuna partition pia ila hawatoi chakula na vinywaji na ndugu anapewa kiti tu na si kitanda. Vyumba vyote huduma za kimatibabu ni sawa tofauti ni hizo huduma ambazo za ziada. So, private ward to general ward tofauti ya gharama inaweza kuwa 30%-40% kwa matibabu ya tatizo hilo hilo. Ubaya hawasemi haya mwanzo. Kama issue ni chakula unaweza pika nyumbani ulikofika ukamletea mgonjwa, maana gari la bure lipo unaita tu dereva akupeleke nyumbani anytime. Samahani kwa maelezo marefu.
 
MKuu hizo dawa za kuja kutumia nyumbani nazo ni million 8? Au ilikuwa kwenye ile million 8 za mwanzo?
Pole sana na ahsante kwa kutujuza ili wengine wasiendelee kuliwa
 
Asante
Pole sana na ahsante kwa kutujuza ili wengine wasiendelee kuliwa
Asante kiongozi. Nilienda nikiwa sina mwanga wowote na baada ya kurudi sikuona sababu ya kukaa kimya.
 
Back
Top Bottom