Mrejesho; Matibabu India. Tumenusurika kutapeliwa

Mrejesho; Matibabu India. Tumenusurika kutapeliwa

Mkuu katika Ubalozi wetu wa Tanzania uliopo New Delhi kuna Afisa wa Ubalozi anayeshughulikia matibabu kwa watanzania (mwambata wa afya) amekuwa anatoa msaada mkubwa wa kusaidia watanzania wanaota kupatiwa matibabu nchini India. Mimi binafsi amenisaidia kutafuta hospitali za gharama nafuu na amesaidia watanzania wengi sana. Anaitwa Dr. Kheri Goloka. Tatizo la watanzania wengi hawataki kutumia balozi zetu zilizopo nje ya nchi. Wanakwenda kwenye balozi pale wanapopata shida tu. Kumbe wangeweza kupiga simu tu kwenye balozi zetu na kusaidiwa kabla hata hawajakwenda katika nchi usika.
Weka namba za simu watu wamjue

Acha ujuaji usiokuwa na maana yoyote
Huyu ndgu yko sawa
Ila inawezekana wewe ndo wale wapigaji
Tumekushitukia.
Ungezungumza unachokijua wewe kuliko kutuletea taarabu yakumshambulia mtoa maada.
Naomba kuwasilisha
"Huyu jamaa siyo mkweli, hamna mambo kama hayo. Kuondoka Tz lazima uwe na viza ambayo pia utaipata baada ya kupewa invitation for medical care in India from a recognized institution, nao pia hawawezi kukupa invitation bila kupata proper medical history lab. Radiology reports from a recognized medical practitioner or hospital. Sasa huyu jamaa aliendaje? Mji alioenda, Bangalore ni moja kati ya majiji yaliyostaarabika India, kwanza hakuna vidispensary, huyo angesema huku Gujarat au Mumbai ningemuelewa kidogo.
Ni muongo, nina wasiwasi kama amewahi kufika India. Kuhusu gharama ni kweli, wakati mwingine wanakadiria chini, ila ikiwa gharama ni tofauti sana ukiwashupalia hawatakudai zaidi ya budget, lakini wewe mwenyewe unapima na huduma ulizopewa, unaamua kulipa, hawawezi kukupa exact. Mbona sisi tumerudishiwa dola 600 zilizozidi kwenye advance tuliyotoa?
Hakuna wizi kama bongo hata kidogo. Kuhusu Hospital zenye majina makubwa kuwa na huduma mbovu ni kweli kwani sisi tuko Apollo, ni kubwa sana, huduma zile specialized ni nzuri sana, shida ni huduma ndogo ndogo kwa manesi na wahudumu hazivutii saana, ila kwa vyovyote, wako vizuri kuliko sisi. Tunatakiwa tupambane sana kuweza kufika robo ya hawa jamaa. Mgonjwa wangu alitibiwa Regency na Muhimbili kwa jumla ya siku 21 na hakupata huduma inayoeleweka.
Tuliondoka Dar tar 28/4 tukafika asubuhi 29/4 Apollo, tulipokewa Airport moja kwa moja hadi Hospital. Vipimo vyote vilianza immediately na kufika saa mbili usiku treatment plan tayari kesho yake asubuhi saa 1.30 aliingizwa Theater. Wako makini sana kuhakikisha hukai siku nyingi hasa unapokuwa foreigner. Sasa huyu anayejiita mkuu sijui alienda nchi gani, labda Afghanistan. Waforwadie hii testimony yangu please, wasiogopeshwe."
 
Back
Top Bottom