Sasa ndio yametokea yote hayo, ndugu zake wanajua, serikali ya mtaa wanajua na kata wanajua so mimi sidanganyi na haya yametokea. Wazazi wake na ndugu zake upande wa baba wamemsusia wamesema niende mahakamani nikadai haki yangu na wako pamoja na mimi kwa sababu wananifahamu vizuri na jinsi nilivyohangaika na mtoto wao.
Hii ni messege aliyonitumia baba yake mzazi nanukuu ''Mama nakupenda sana hujanikosea hata siku moja hata kama mtaachana mimi usinitupe, kuhusu suala ya kusimamia huyo mwanangu mimi siwezi nimeshindwa, nenda serikali ya mtaa, polisi au mahakamani upate haki yako'' mwisho wa kunukuu. Hii messege ninayo mpaka sasa hadi nimeiprint kabisa