Habari za asubuhi wana JF
Mwezi wa saba nilipost mkasa kuhusu matatizo na mume wangu https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/876139-maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu-10.html
Baada ya kupata ushauri kutoka kwa wana JF, ndugu zangu na upande wa mume niliamua kuongea naye kuhusu tabia zake, lakini hakuweza kubadilika. Siku moja aliondoka kwenda Msata kama alivyodai mwezi mzima bila kuaga wala kujua naishije pale nyumbani. Siku zote hizo hakuwa anapiga simu mpaka mimi ndio nimpigie.
Nilichukua uamuzi wa kumuomba baba yake amuite ili tuweze kuyaongea kama familia zote mbili. Baba aliitisha kikao cha kukutana na familia za pande zote lakini alikataa kuja na kusema mimi niondoke pale nyumbani na asinikute maana ataniumiza.
Nikaamuakupeleka shauri baraza la kata kwasababu imeshindikana kwa ngazi ya familia. Kata nako aliitwa mara tatu lakini hakufika. Kumbe siku zote hizo yuko hapahapa Dar anaishi na yule mwanamke ambaye alimtambulisha polisi kama mke wake na pia alishawahi kumleta pale myumbani.
Mimi nikachukua uamuzi wa kuondoka pale nyumbani chini ya mjumbe na mjomba wake nikaenda kwa dada yangu. Siku hiyo naondoka nilikutana naye njiani anarudi nyumbani akiwa na yule mwanamke, kumbe alimuambia mjomba wake akiondoka tu mke wangu uniambie mimi niko karibu nitakuja.
Alipofika pale nyumbani siku ileile aliondoka na vitu vyote pale nyumbani na akaweka mpangaji baada ya siku mbili yeye akaondoka akarudi kwa yule mwanamke. Jana baraza la kata limenipa barua ya kwenda mahakamani kudai talaka na madai mengine baada ya huyu mwanaume kushindwa kutoa ushirikano baraza la kata.
Nimeshafungua kesi mahakama ya mwanzo na leo ndio taandikiwa wito wa kumuita mahakamani. Pamoja na kupangisha nyumba ambayo tumejenga wote bila ridhaa yangu pia aliondoka na gari yangu.
Nawashukuru sana wana JF kwa michango yenu, pia na member mmoja ambaye amekuwa msaada mkubwa kwangu mpaka nafikia hatua hii. Michango yenu ni muhimu sana hasa kipindi hiki cha kudai haki yangu.
Asanteni sana
Mungu awabariki sana