Mrejesho: Kilimo cha mpunga Bahi

Jembe halimtupi mkulima , huu msemo umetamalaki sana hapa kwetu tz, lakini Mara kadhaa huwa unakuwaga na ukweli ndani yake.

Msimu wa 2018/19 nilijaribu kulima mpunga bahi hekari 5, japo nilikodi hekari 12 na kuzitifua zote kwa trekta, ila nikakumbana na ukame wakat napandikiza. Nilifanikiwa kuoandikiza mashamba matano tu, maji yakawa yameisha, hivyo nikawa Sina jinsi.

Si haba katika heka hizo tano nimeweza kurudisha mbegu, nimepata magunia 54, yenye ujazo wa debe saba Saba 7,7. Kiukweli nashukuru San mungu Kwan mwaka huu ulikuwa na changamoto sana. Wngine hawakuweza KUVUNA kabisa hata Lita moja.

Nimezidi kunifunza mengi katika kilimo ndugu zangu, wakati mm nimepata vigunia 54, Kuna mtu kapata migunia 400, na mwingine migunia 600, hivyo ukiwa kupanda uhakika wa kupiga pesa kupitia kilimo INAWEZEKANA.

Nimeona si haba niwaletee mrejesho wananzengo kwani Kuna baadhi ya wanajf walitaka mrejesho Mara baada ya kutoka shambani.

Picha hizi hapa.
View attachment 1148431View attachment 1148432View attachment 1148433View attachment 1148434View attachment 1148435View attachment 1148436View attachment 1148437View attachment 1148438View attachment 1148440View attachment 1148444
Mkuu hongera.
 
Mwaka 2018 ilikuwa sherehe ya mavuno bahi, ila 2019 ni kipigo cha mbwa koko, by the way hongera mkuu
Mm binafsi nilienda kukagua mashamba ya pale bahi kwny scheme na sikuvutiwa, kilimo cha bahi kinategemea mvua zinyeshe manyara ndo ziujaze maji ule mto wa msimu. Nikaona ni bora kulimia sehemu yenye maji ya uhakika
 
Nimepitia maswali na majibu humu nimeona bora kilimo cha nyanya mara pengine kuliko mpunga. Sijawahi kulima mpunga, ila mwaka jana nilijaribisha kulima nyanya kwa eneo km nusu eka. Nikapata tenga 142. Niliuza kwa bei tatu. Nilianza kwa sh 60000, baadae ikashuka kidogo 55000, bei ya mwisho nikauza 45000. Mwisho nikitoa gharama zote nilibakiwa na mil5+
Nyanya ni hatari zaidi,mwaka huu ndio imekua na bei nzuri.
 
Mimi Nalima Viaz mviringo Njombe lkn Miaka ya nyuma nmewahi enda kulima mpunga chimala-kapunga. Nilicho gundua n kwamba mpunga unapolima inatakiwa uwe na alternative mvua ikifel unafungulia maji ya kumwagilia hapo 100% unatoboa. Generally agriculture pays!!
Uko sahiii mkuu
 
Jembe halimtupi mkulima. Huu msemo umetamalaki sana hapa kwetu Tz, lakini mara kadhaa huwa unakuwaga na ukweli ndani yake.

Msimu wa 2018/19 nilijaribu kulima mpunga Bahi hekari 5, japo nilikodi hekari 12 na kuzitifua zote kwa trekta, ila nikakumbana na ukame wakati napandikiza. Nilifanikiwa kupandikiza mashamba matano tu maji yakawa yameisha. Hivyo, nikawa sina jinsi.

Si haba katika heka hizo tano nimeweza kurudisha mbegu, nimepata magunia 54, yenye ujazo wa debe saba saba (7,7). Kiukweli nashukuru sana Mungu kwan mwaka huu ulikuwa na changamoto sana. Wengine hawakuweza kuvuna kabisa hata lita moja.

Nimezidi kujifunza mengi katika kilimo, ndugu zangu. Wakati mimi nimepata vigunia 54, kuna mtu kapata migunia 400, na mwingine migunia 600, hivyo ukiwa kupanda uhakika wa kupiga pesa kupitia kilimo INAWEZEKANA.

Nimeona si haba niwaletee mrejesho wananzengo kwani kuna baadhi ya wanaJF walitaka mrejesho mara baada ya kutoka shambani.

Picha hizi hapa

View attachment 1148431View attachment 1148432View attachment 1148433View attachment 1148434View attachment 1148435View attachment 1148436View attachment 1148437View attachment 1148438View attachment 1148440View attachment 1148444
Hongera sana mkuu cha muhimu hapo umepata Elimu nzuri sana ya kilimo hasa kwa vitendo. Nikija kwa upande wa faida mwaka huu hujapata faida Na inawezekana hata mtaji haujarudi
Gunia 54 x 65,000= 3,510,000.
Gharama za kulima mpunga kwa ekari 1 minimum ni laki 8 kwa ekari 5 unakuta ushatumia million 4.

Usikate tamaa umepambana Na changamoto za kilimo kwa vitendo next time utapiga vizuri
 
Nimepitia maswali na majibu humu nimeona bora kilimo cha nyanya mara pengine kuliko mpunga. Sijawahi kulima mpunga, ila mwaka jana nilijaribisha kulima nyanya kwa eneo km nusu eka. Nikapata tenga 142. Niliuza kwa bei tatu. Nilianza kwa sh 60000, baadae ikashuka kidogo 55000, bei ya mwisho nikauza 45000. Mwisho nikitoa gharama zote nilibakiwa na mil5+
Tenga 142 ?????
 
.... msaada wakuu:

_kwa aliewahi kulima mpunga morogoro gharama ya eka moja ni bei gani, kuanzia kukodi shamba mpk kuvuna (jumla)

mbeya na bahi, nazo pia nahitaji msaada nijue gharama.
 
Tafuta eneo la umwagiliaji,kilimo Cha mvua hakiaminiki-nimelima heka3,nimepata gunia 120-trust me mbolea mara3-kilimo Cha umwagiliaji kinalipa,Kila gunia debe 6
 
Back
Top Bottom