Je, kilimo cha Mpunga kina tija mpaka kuitegemea kazi hiyo hiyo?

sir charito

Member
May 14, 2019
58
25
Wadau mimi ni mfanya biashara, nina duka la jumla la mahitaji ya nyumbani lakini kwa kuwa nimefanya mda mrefu nimechoka. Kwa kuwa nashinda dukani mwenyewe natamani nifunge hili duka halafu ninunue trekta na kukodi heka angalau 50 za mpunga Mbarali Mbeya na kwenda kusimamia mwenyewe.

Sasa naomba ushauri wadau, kazi hiyo ya kulima tu labda na trekta inaweza kunifanikisha mahitaji yangu yote pasipo kua na kazi ingine?

Mdau mwenye uzoefu na haya mambo naomba ushauri.

sir charito

Kilimo cha mpunga kinahitaji mtaji mkubwa (kukodi Shamba, kuliandaa, mbegu, kupanda, ng'olezi, madawa, ombaini ya kuvunia, turubai, viloba, wanaopakia kwenye magunia na kushona, kuyatoa shamban hd godauni, kulipia godauni, ushuru nk) a huku matokeo yake yakitegemea hali ya hewa isiende tofauti.

Pia, baada ya mavuno unahitaji uutunze mpunga huo godauni Kwa miezi kadhaa ili bei iwe nzuri sokoni. Kumbuka wakati wote huo pesa haizunguki.



sir charito

Nenda kalime Mbarali-Mbeya lkn usimamie mwenyewe.

Hakikisha shamba linaingia MAJI kabla hujalikodisha au kulinunua. Huu ndio wakati muafaka wa kufanya utafiti wa shamba zuri kwa sababu utaona kama limevunwa. Uliza Majirani kupata taarifa za shamba husika kama linaingia MAJI. Usiingie kichwa kichwa kwa kuangalia uzuri wa shamba kwa macho.

Anza kwa kununua Power tiller kwa ajili ya kulimia shamba lako lakini pia utakodishwa kulima mengine hivyo kipato kitaongezeka na kusaidia kuhudumia shamba lako.

USIMAMIZI ndio kila kitu. Usiwe kama wale mabishoo wa Dar kwenda kulima Vitunguu Ruaha, waliishia Guest na kutuma vijana shamba. Kilichowakuta wanakijua wenyewe. Nenda angalia kila hatua inayofanyika shambani. Mbegu nzuri ya Biashara ni Saro!

Mwisho, kumuachia mtu biashara Dar ndio mwanzo wa kuiangamiza, labda kama Mkeo au Mumeo ambaye mmeshibana, otherwise subiri mabua!!



Acha nikupe madini bro. Acha kununua trekta, chimba kisima, kuchimba kisima ni milioni 15. Hapo jumlisha installations zote na jenereta kubwa incase hakuna umeme huko.

Jinsi ya kulima kutokana na experience yangu, mfano sasa hivi nyanya bei ghali kwahiyo rudi nyuma miezi mitatu, maana yake mwezi wa tatu unaweka miche, mwezi wa sita utakua umevuna wakati huo kumbuka walima nyanya wengi wanategemea mvua, hivyo hutakua na washindani wengi hivo kufanya nyanya bei yake kua juu.

Ukifika mwezi wa saba unalima tikiti, mwezi wa kumi unavuna. Wakati huo Dar jua linakua kali kweli, unasafirisha Dar unapeleka Temeke pale sokoni, na matiki miezi hiyo yanakua adimu sana.

Utapiga hela mpaka wakuite Freemason. Ukiwa na hekari nyingi usiwe na tamaa ya kulima zote, kodisha kwa wengine kwakua kisima kinakuepo hivo watagombania hatari. Hizo hela za kukodishia ndo zitaendesha gharama za mazao yako.

N B:
Hata ukiwa unapiga hela usiwaambie waliokodisha kwako, mana zama izi information is power. hata ukipga hela we endeleaa kulalama kua vyuma vimekaza na Magu kabana, wakija kushtuka ushafika mbali
 
sir charito

kilimo jiandae kufa kwa presha kama ndio sehemu pekee unaitegemea...Nakushauri kuwa kama ndugu yetu wa FOREX wewe nunua trekta au tafuta trekt nenda nayo mashambani fanya kazi ya kulima mashamba ya watu..Kusanya hela kwanza then ukiingia kwenye kilimo unaingia unalima aina tofauti tofauti za mazao.

Usitegemee mpunga tu,ukiingia kwenye kilimo ukitegemea kutoka kwa zao moja hauna tofauti na mtu anae BET so ili uone matokeo chanya ya kilimo..Tafuta capital kwanza halafu ukiingia Unalima mazao hata mawili au matatu..pakigoma huku kule panatiki.

Hali yenyewe ya hewa hiii haieleweki..borra utulie zako kwenye duka lako biashara haiendi mali yako inabaki unaiona ila Kilimo ukichana MKEKA mzeee ni unarudi down to ZERO.

Usi beep kilimo...tafuta vocha kisha PIGA.
 
Tatizo hatuambiwi ukweli ili kilimo kikutoe unahtaji MTAJI ULIOSHIBA wengi tunadanganywa kua Kilimo ni JEMBE na ARDHI na MKULIMA thubutuuuu,ukitaka kulima useme YES namimi mkulima watu wavutike kulima na wao hakikisha una CAPITAL...mtafute ndugu yetu SUMRY ukimskiliza akikusimulia kilimo unakua interested na KILIMO.

Kilimo ni kizuri only if UKIWA NA MTAJI ULIONONA...nadhani ni best place to be kama unahamu ya kushika mahela mahela mengi uyafunge kwenye raba bendi na sio uyaeke kwenye wallet.
 
Hahahah kilimo kisikie vijiweni tu.
Ukija Field huku ni kama mtoto wa 2010 kupewa Necta ya 1970!

Msidanganywe na Motivational Spika hao ambao wanawahubiria theory za kufanikiwa na kukusanya viingilio vyenu.
 

Attachments

  • IMG20190610152553.jpg
    IMG20190610152553.jpg
    526.1 KB · Views: 70
  • IMG20190610152534.jpg
    IMG20190610152534.jpg
    449.2 KB · Views: 77
nimeshagundua tatizo,huyu jamaa anaogopa kuacha mtu dukani eti ataibiwa,,sasa sijui akiugua itakuaje?,chakufanya ajili mtu,halafu kwenye kilimo usiende kwa gia zote,anza kidogo kidogo
 
Back
Top Bottom