Mrejesho: Alinipa penzi nimwingize kazini, sasa ananitishia

Mrejesho: Alinipa penzi nimwingize kazini, sasa ananitishia

umasikini mbaya sana, kidume mzima unashindwa kutafuta laki 2 umalizane na huyo binti hadi unadhalilika kiasi hicho???
Hebu be serious boy!
 
Gharama za ukuadi wakati mwingine mmh. Fanya kikao na HR mrudishe mzigo.
 
Hahahahahahahahahaha Evelyn Salt na Paulo Sergio De Souz wapendwa atoto Apologise lady ...please njooni tumuombee mpendwa wetu aliyerubuniwa akamfahamu binti mpendwa!

Mentor ni hili suala ni mpango wa shetani kabisa, yatupasa tujinyenyekeze mbele ya bwana kwa ajili ya ndugu yetu huyu , sasa inabidi kesho tukutane jioni kwaajili ya maombi ila mje na sadaka kila mtu $500 mimi kama kiongozi wa maombi nitaziombea hizo sadaka nyumbani kwangu ili upako uteremke kwenu watoaji..
 
Last edited by a moderator:
Watu wa Mungu nawasalim,

Kama mtamkumbuka nilishawahi leta habari ya Alinipa penzi ili nimuingize kazini, imebuma, anatishia kuja kazini kuharibu yule mpendwa mwenzangu, binti, ambae alinipa pesa tshs laki mbili ili nikampe HR wetu haweze kumpa kazi.Baadae akanilaghai na kunirubuni na kimakosa tukajikuta tumeshirikiana nae kimwili.Muda ulivyozidi kwenda bila kufanikiwa kazi akaanzisha vurugu akitishia kuja kazini kwangu akidai pesa.

Mrejesho wenyewe;

Juzi huyu binti alikuja kazini kwangu, aliulizia kwa HR akapelekwa, akamweleza hr kuwa ananidai hela kiasi cha laki mbili na kwamba nimemzungusha muda mrefu sitaki kumpa, nikaitwa, nilipoelezwa na HR madai ya binti, kwanza nilikana simfahamu na ndio namuona siku hiyo, nikadai huenda amepatwa na matatizo ya akili.

HR aliita walinzi na kumtoa kwa nguvu mule ndani huku akisema nitaona, baadae nikamwelewesha HR kuwa zile laki mbili nilizompaga mwaka Jana mhusika ndio huyo binti, alinisifu kwa ubunifu wangu mle ndani.

Jioni yake nilikua nimepumzika na familia yangu tukitaza taarifa ya habari, mlango ukagongwa hodi maid kwenda kufungua, nashangaa wameongozana hadi ndani na yule binti aliekuja kazini almanusura nianguke.

Akasema, si ulijifanya mjanja sasa nimekuja kwa mkeo, wife kusikia vile akamuuliza kwani kuna nini G maana wanafahamiana binti anaishi mtaa wa nyuma binti yule bila aibu Alimjibu wife kuwa ""muulize mumeo anajua mm na yeye tuna biashara gani".

Wakaanza kuzozana kwa maneno makali, huku binti akiwa anatoka nje akiendelea kusema vibaya kwamba, jasho la mtu haliliwi, na kwamba nimemjua na hela yake nimemdhulumu

Wapendwa hivi sasa nipo kwenye kumbembeleza wife tangu siku hiyo, nimemkana binti kwamba sijafanya nae chochote isipokua ananidai kweli lakini mama watoto hataki kuelewa kabisa, hanizungumzishi, na hata conjugal rights sijapata since that fateful day.

Ni wazi kabisa huyu binti ametumwa na shetani, ni ibilisi mwenyewe kajibadilisha umbo, ni lucifer, matendo aliyonifanyia sio kabisa, i condemn her in the strongest terms possible nilipanga kumlipa hali yangu ikitengemaa lakini ameshindwa kuwa na subira.

Alinihadaa hadi tukashirikiana, tukamkosea Mungu, sasa bado anaendelea kunifuata kazin na hata nyumbani, mtu ukitoa rushwa ya kupata kazi huwa ni sandakalawe, unaweza kupata au kukosa, huwa haidaiwi.

Yaani huyu binti ni kichaa alieshindikana, naomba mniombee maombi makali sana, ili nyumba yangu itulie, sijui kwanini nilijiingiza kwenye jambo hili

Your prayers are highly needed

Ni juzi tu, miezi kama miwili au chini ya hapo nilitoka kwenye mgogoro na wife, na sasa ndio tulikua tuna recover. Akina na mama, unatafuta kazi, unampa mtu pesa akusaidie, hiyo haitoshi unamrubuni na kufanya nae kitendo ambacho ni chukizo mbele za bwana, na wewe umeokoka.

Nini maana yake?
Mrudishie heka yake na wewe!
Hakuna sala ya udhalimu itakusaidia.
 
Back
Top Bottom