Mrejesho: Alinipa penzi nimwingize kazini, sasa ananitishia

Mrejesho: Alinipa penzi nimwingize kazini, sasa ananitishia

Joined
Jul 29, 2015
Posts
20
Reaction score
199
Watu wa Mungu nawasalim,

Kama mtamkumbuka nilishawahi leta habari ya Alinipa penzi ili nimuingize kazini, imebuma, anatishia kuja kazini kuharibu yule mpendwa mwenzangu, binti, ambae alinipa pesa tshs laki mbili ili nikampe HR wetu haweze kumpa kazi.Baadae akanilaghai na kunirubuni na kimakosa tukajikuta tumeshirikiana nae kimwili.Muda ulivyozidi kwenda bila kufanikiwa kazi akaanzisha vurugu akitishia kuja kazini kwangu akidai pesa.

Mrejesho wenyewe;

Juzi huyu binti alikuja kazini kwangu, aliulizia kwa HR akapelekwa, akamweleza hr kuwa ananidai hela kiasi cha laki mbili na kwamba nimemzungusha muda mrefu sitaki kumpa, nikaitwa, nilipoelezwa na HR madai ya binti, kwanza nilikana simfahamu na ndio namuona siku hiyo, nikadai huenda amepatwa na matatizo ya akili.

HR aliita walinzi na kumtoa kwa nguvu mule ndani huku akisema nitaona, baadae nikamwelewesha HR kuwa zile laki mbili nilizompaga mwaka Jana mhusika ndio huyo binti, alinisifu kwa ubunifu wangu mle ndani.

Jioni yake nilikua nimepumzika na familia yangu tukitaza taarifa ya habari, mlango ukagongwa hodi maid kwenda kufungua, nashangaa wameongozana hadi ndani na yule binti aliekuja kazini almanusura nianguke.

Akasema, si ulijifanya mjanja sasa nimekuja kwa mkeo, wife kusikia vile akamuuliza kwani kuna nini G maana wanafahamiana binti anaishi mtaa wa nyuma binti yule bila aibu Alimjibu wife kuwa ""muulize mumeo anajua mm na yeye tuna biashara gani".

Wakaanza kuzozana kwa maneno makali, huku binti akiwa anatoka nje akiendelea kusema vibaya kwamba, jasho la mtu haliliwi, na kwamba nimemjua na hela yake nimemdhulumu

Wapendwa hivi sasa nipo kwenye kumbembeleza wife tangu siku hiyo, nimemkana binti kwamba sijafanya nae chochote isipokua ananidai kweli lakini mama watoto hataki kuelewa kabisa, hanizungumzishi, na hata conjugal rights sijapata since that fateful day.

Ni wazi kabisa huyu binti ametumwa na shetani, ni ibilisi mwenyewe kajibadilisha umbo, ni lucifer, matendo aliyonifanyia sio kabisa, i condemn her in the strongest terms possible nilipanga kumlipa hali yangu ikitengemaa lakini ameshindwa kuwa na subira.

Alinihadaa hadi tukashirikiana, tukamkosea Mungu, sasa bado anaendelea kunifuata kazin na hata nyumbani, mtu ukitoa rushwa ya kupata kazi huwa ni sandakalawe, unaweza kupata au kukosa, huwa haidaiwi.

Yaani huyu binti ni kichaa alieshindikana, naomba mniombee maombi makali sana, ili nyumba yangu itulie, sijui kwanini nilijiingiza kwenye jambo hili

Your prayers are highly needed

Ni juzi tu, miezi kama miwili au chini ya hapo nilitoka kwenye mgogoro na wife, na sasa ndio tulikua tuna recover. Akina na mama, unatafuta kazi, unampa mtu pesa akusaidie, hiyo haitoshi unamrubuni na kufanya nae kitendo ambacho ni chukizo mbele za bwana, na wewe umeokoka.

Nini maana yake?
 
Hapa ndipo methali ya utavuna ulichopanda inapokuwa na maana. Yataisha tu ndugu, hakunalenye mwanzo likakosa mwisho.
 
pole mkuu ila ukome wanawake sisi ni viumbe tunao tenda ndipo tunatafakari ... ila omba sana ndoa yako umeiingiza mwenyewe kwenye moto .. pole sana
 
Hii ungepeleka kwenye gazeti la Ijumaa Wikienda ungeuza sana!
 
Evelyn salt kuja huku ile ya "kufahamiana" imeleta mrejesho kama ww ni mmoja wa wapendwa unahtajka huku kuokoa ndoa ya watu.
 
sasa si umlipe hiyo laki mbili zake mzozo uishe,alafu wewe matajuana na HR wako?
 
Mwaka huu nimecheka mara tatu tofauti na ninavyocheka......hapo kufahamiana, kujuana....mwisho kulaghaiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom