Mrejesho ajali ya coaster Tanga

Mwendo kasi.kuna dogo wa bodaBoda.anaona magari yanakwenda polepole akaona anachelewa.aka overtake kushoto.kumbe mbele kuna lori limeharibika limepaki kushoto.na yeye yupo nduki.akajibamiza mwenyewe nyuma la lori.na safari yake ikaishi hapo hapo.ilikuwa saa moja usiku.
 
pole sana. hiyo coaster niliiona pongwe zikiwa zimeongozana mbili...yenu ilikuwa nyuma mida ya saa 1 jioni, usiku niliposikia ajali na kuona rangi ya gari nilihamaki sana. Ugua na uguza pole mwaya.
 
Pole sana. Mungu ni mwema. Inasikitisha sana hospitali teule kukosa umeme. Serikali iangalie vipaumbele muhimu.
 
pole sana. hiyo coaster niliiona pongwe zikiwa zimeongozana mbili...yenu ilikuwa nyuma mida ya saa 1 jioni, usiku niliposikia ajali na kuona rangi ya gari nilihamaki sana. Ugua na uguza pole mwaya.
Ilipita Pongwe kugombea abiria,shukrani
 
Huduma za kijamii (afya, elimu, maji, miundo mbinu kama mifereji kwenye makazi ya watu na mengineyo) sio muhimu sana, kipaumbele chetu ni flyovers, bombardier, reli, nk.
 
Daah pole sana bro.Mungi awatie nguvu na mtoto.Ila nimejifunza jambo ..hospital hizi..Unaweza kufa kama huna hela kwa wakati husika.Maana si wao wa kulaumiwa.Ni aina ya budget zetu za wizara husika.
 
Kadri siku zinavyokwenda utu wa mtu mweusi unazidi kuporomoka kwa kasi ya ajabu sana, Imagine watu wamepata ajali mijitu mingine inakuja badala ya kutoa msaada..inafikiria kuiba mali za wahanga wa ajali, tatizo ni umasikini au roho mbaya sijui..hii sio poa kabisa! By the way pole sana kwa yaliyokukuta katika ajali!
 
Acha Mungu aitwe Mungu, Mungu aliekuokoeni ndie atakae kuponyeni. Nashindwa kuelezea huzini yangu ila Poleni sana sana
 
Pole sana Mkuu, Allah akufanyie wepesi katika kupona InshaAllah.
 
Hospital zetu hapa nchini zinakatisha tamaa sana! Imagine mtu anashonwa zaidi ya masaa mawili bila ganzi + umeme hakuna. Pole sana mkuu
Hizo ndizo gharama za CCM ambazo huwezi kuziona mpaka ufikwe na majanga mkuu. Ndipo unapopaswa kujiuliza vipaumbele vyetu ni vipi tofauti na zamani tukiambiwa tuna maadui watatu wakuu: 1. Ujinga. 2. Umasikini na 3.Maradhi.
Laiti tungeliondoa ujinga, umasikini ungeondoka na afya zingeimarika!! Lakini kwa kuwa watawala wana vipaumbele vyao hayo mambo matatu yataendelea kuwa mwiba mpaka tutakapobadilika kwa kutambua nani anatusababishia hao maadui waendelee kuwepo.
Ikiwa nilipata ajali mwaka 1998 nikashonwa mguu bila ganzi mpaka leo ugonjwa ni uleule bado tunaimbiwa nyimbo umeme na afya vimeimarika napata shida kidogo kuelewa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…