Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Niliwahi kuandika huko nyuma (abt 3 years ago) kuwa huwezi kumjua fisadi kwa kuangalia gari, cheo, hadhi, nyumba anayoishi n.k Ufisadi hauwezi kupimwa kwa namna hiyo. Nilikataa kuwa ufisadi siyo dini, rangi, kabila wala hali ya maisha. Ufisadi NI VITENDO! Mtu hawi fisadi kwa sababu maelfu ya watu wanamuita fisadi; mtu hawi fisadi kwa sababu tunamchukia au anachukiza. Ufisadi ni VITENDO.
Katika hili ninachoona ni maelezo ya mradi wa Dr. Mwinyi. Hilo peke yake haliwezi hata kidogo kumfanya kuwa fisadi.
a. Je, mali hii imetangazwa katika tangazo la mali kwa mujibu wa sheria ya Maadili?
b. Je, inaendana na kipato chake
c. Je, katika kupata kiwanja, mkopo n.k ametumia cheo chake kuathiri mchakato wowote. Kwa mfano, mtu mwingine alikuwa apewe eneo hilo lakini kwa vile yeye ni Waziri akapata upendeleo wa pekee? Au, kama alipata mkopo Benki je vigezo vilivyotumika kumpa yeye mkopo vyaweza kutumika kumpa Mtanzania mwingine (asiye na cheo au ujiko wa kisiasa na nasaba kama wa wake) kumpatia mkopo?
d. Je, ujenzi wake wa hizo apts umezingatia vigezo vyote vya ujenzi? Je eneo hilo zilipojengwa lilikuwa zoned kwa ajili ya makazi ya watu?
So.. ni katika kutafuta majibu ya maswali haya ndipo tunaweza kusema "ufisadi" wa mtu fulani. Kumbuka... UFISADI NI VITENDO!
Kiranga,
Ningekuwa bongo sasa hivi mbona hii ni kazi ndogo tu? Remember I am Jasusi, no?
Hapana. Wote mafisadi. Baba fisadi, mwana fisadi. Si huyu ndiye aliyepewa tender ya kuingiza magari ya kijeshi wakati wa utawala wa baba yake na kuliletea jeshi magari yasiyofaa kutoka Dubai?
mtoa rushwa na mpokea rushwa wote lile neno alilotumia mwalimu mali manganya?
A person is presumed innocent until proven guilty, the burden of proof is on the accusing party, not the accused.Ndiyo maana nasema toeni ushahidi.na kama unasema ni enterprneur tupe faili la biashara zake na kodi anayo lipa na pia uhaki katika kufanya biashara zake dhidi ya mtu mwingine.
Nilishasema familia hii inanuka rushwa, lakini huwezi kuiongeza hii kama rushwa kwa sababu tu familia hii inanuka rushwa, inabidi uionyeshe hii kama rushwa in it's own right.na kumbuka kuna kisa kilitokea ilipokuwa ofisi ya zambia airways kuchukulia na familia ya kwanza wakati huo, wakati kiutaratibu hiyo sehemu ilitakiwa iwe available kwa applicant wa kwanza, sasa hiyo utasema ni fair play, kuna loliondo gate, kuna dhahabu kusafirishwa nje, kuna uwanja wa kia kukodishwa kwa $1000.00 kwa mwezi kwa miaka 25 nk hadithi ni ndefu hata hatuwezi kuimaliza leo , bali tunakupa viashiria vya mchezo mchafu.
Kweli mkuu Jasusi, baba na mtoto wote ni mafisadi. Enzi ya baba yake ndio mandhali ya fukwe zetu zote kule baharini ziliharibiwa kwa kupewa wafanyabiashara wahindi; ndio wakati huo Ladwa akapewe ufukwe na kujenga Golden Tulip na Subash Patel akajenga Whitesands na Sea Cliff hotels !! Kote huko walikuwa wanafisadi tu!! Mtoto nae akapewa unaibu waziri wa Afya enzi ya Mkapa chini ya mamaFisadi Anna Abdalla wakala magendo lukuki ya kuagiza dawa kule Medical stores Department!! Hata kama atasema kuwa amekopa hizo billioni kumi hiyo itakuwa ni gelesha tu ukweli ni kwamba huyu kijana ni mchafu!!
Nadhani hapa wote tunamiss point ya mleta hoja!!!
Kama waziri wa jamhuri, na unakuwa na biashara kubwa za namna hii, ile sheria ya JK ya biashara na siasa inakaa vipi hapa??
Nadhani si vibaya mawaziri kuwa na biashara za kusaidia kujikimu maisha, lakini ili la kuwa na top business people tena mawaziri inabidi mjadala ufanyike tuone lipi ni bora.
Jamani mwacheni bwana mdogo..huyu dogo pamoja na kuwa ametoka familia ya rais mstaafu yupo cool...
..sikatai kuwa baba yake alimpa viwanja sehemu nzuri...lakini naye ana akili ....alitumia viwanja vyake kuanza biashara ya kujenga na kupangisha nyumba...
.na kwa wale msiojuwa biashara hii ..unahitaji tu kuwa na eneo prime...mtaji wa kujenga unapewa na benki...wanabaki na hati...,na wengine wanakutaka malipo ya rent yapitie kwenye akaunti yao...its a good deal ...ukiamua kuuza nyumba unapata pesa maradufu......
Pia kitendo cha hussein kuweka jina lake kwenye mradi ni cha kupongezwa.....kwani angeweza kuandika jina la muhindi pale na msingejuwa....tuache wivu...tuwaunge mkono wenzetu pale wanapofanya mambo kwa uwazi..ili ku encourage ....wengine pia wawe wawazi!!!
Tabia ya kuita kila mtu fisadi inasababisha unafiki kwa viongozi ....tunawajuwa kina msutya wana hadi magorofa JAPAN....kwa ajili ya unafiki kaama huu...tumpongeze kijana amekuwa muwazi na anafanya juhudi kuongeza kile alichopewa na baba yake kama mbegu!!.
..NADHANI furaha yenu mngependa kuona anauza na kutawanya ovyo kama teja!!!
kwa wale wenye maeneo sehemu nzuri na hawajui cha kufanyia ni bora wakaomba ushauri tu.....angalieni hata kijitonyama ,mwenge etc magorofa yanapanda ovyo...wengi wanakopa ..si mafisadi wote!
J
Ningependa kuijua kwa undani kama imekataza viongozi wasifanye biashara kabisa na sasa tunarudi kwenye Azimio la Arusha pole pole, maana wako wengi viongozi wenye biashara ati, tuanze kuwasakama wote.
rushwa ina muonekana mwingi, mojawapo ni kutumia madaraka yako. wewe mwenyewe umesema tatizo ni wafanyakazi wa ardhi kuwa tetemekea wakubwa, sasa hapa inaonyesha cheo/jini limetumika ili kupata hicho alicho kipaHujaonyesha kwamba katoa wala kupokea rushwa lakini.
circurmstatial evidence ina mu-implicate, kupata nyumba/kiwanja ambapo wengine ni vigumu au haiwezekani kupata na tunasema watu wote ni sawa, labda uniambie leo hii hii ni kauli tu ya kisiasa na haina ukweli wowote.A person is presumed innocent until proven guilty, the burden of proof is on the accusing party, not the accused.Ndiyo maana nasema toeni ushahidi.
nimeisha kupa msemo wa kiislamu haramu huza haramu., sasa chanzo cha mtaji ni batili je kinacho zaliwa hapo si batili? wewe ni corporate lawyer nafikiri unaweza kunielezea vizuri kwenye huu msemo.Nilishasema familia hii inanuka rushwa, lakini huwezi kuiongeza hii kama rushwa kwa sababu tu familia hii inanuka rushwa, inabidi uionyeshe hii kama rushwa in it's own right.
Elewa kwamba ninapotaka vitu solid sina nia ya kumtetea Mwinyi per se, nina nia ya kutetea thorough examination hapa JF, tusije kuwa a virtual lynch mob iliyo tayari kum lynch mtu yeyote atakayepigiwa ukelele wa fisadi, ili mradi ana fit profile tu.
Mtoto wa mkubwa na ana ma deal makubwa kubwa, si lazima kila mtoto wa mkubwa mwenye deal kubwa awe fisadi, na kama ni fisadi, hatuitendei haki movement ya anti ufisadi kwa kuja na vikauli visivyo na viwango wala harufu ya credibility, katika kutumia upepo wowote unaovuma kutoka kwa hawa watu kuja kwetu kama uthibitisho wa ufisadi, tutakuwa sisi ndio mafisadi wa kweli, maana tutaifisadi haki ya mtu kuwa "innocent until proven guilty" in our court of JF opinion.
nimeisha kupa msemo wa kiislamu haramu huza haramu., sasa chanzo cha mtaji ni batili je kinacho zaliwa hapo si batili? wewe ni corporate lawyer nafikiri unaweza kunielezea vizuri kwenye huu msemo.
nimeisha kupa msemo wa kiislamu haramu huza haramu., sasa chanzo cha mtaji ni batili je kinacho zaliwa hapo si batili? wewe ni corporate lawyer nafikiri unaweza kunielezea vizuri kwenye huu msemo.
rushwa ina muonekana mwingi, mojawapo ni kutumia madaraka yako. wewe mwenyewe umesema tatizo ni wafanyakazi wa ardhi kuwa tetemekea wakubwa, sasa hapa inaonyesha cheo/jini limetumika ili kupata hicho alicho kipa.
circurmstatial evidence ina mu-implicate, kupata nyumba/kiwanja ambapo wengine ni vigumu au haiwezekani kupata na tunasema watu wote ni sawa, labda uniambie leo hii hii ni kauli tu ya kisiasa na haina ukweli wowote..
Pili takukuru wakikufuata huwa wanaanza na circumstatial evidence ili ku-build up the case na hii pia inaendana na Sheria za Mali za Viongozi ilikuona kile kilicho au kuzaniwa kupatika kwa njia zisizo.
hata sheria za kodi na money koundering zinaweza kukazia jambo.
I understand some of you are suprised at this level dough. How do you know he is the sole shareholder? Maybe he is representing someone else. And if it is him how do you know ana assets gani zakupata collateral? Mashamba, investments nyingine? Huyu mtu kaja na thread isiyo na malelezo yoyote na nyie mnaleta ujamaa hapa na kumsupport... Being rich does not make anyone mchafu and yes there are people worth several million dollars so what? Nchi ikiwa na matatizo ndio kila mtu awe maskini? Toeni sababu au muacheni mwinyi apete tuu. SO you think he stole 10billion and is using it to build apartments.. Are you insane.lol No one invests using their own money to do things like that.. It is almost always the bank's money.. (and nasema haya as a corporate lawyer often dealing with these types of arrangements and furthermore I myself do modest investment in real estate) So swala la watu walizoea mishara ha laki 5 ama 1.5m kuanza shangaa mtu anacheza na 10 million dollars (it doesnt mean hizo hela anakula.. it is an investment portfolio sio sawa na mshahara..) MwanaFA umepatia kusema kuwa kuna watu wana some kind of class-beef. I am not a fan of social strata myself but it is a natural consequence of human interaction a special in the Capitalistic world.
I myself plan to retire with around 100 million dollars..does that mean I have ufisadi in my plans..NO way. Its just personal ambition and vision. Mtu asi invest, fisadi..
Jamani mwacheni bwana mdogo..huyu dogo pamoja na kuwa ametoka familia ya rais mstaafu yupo cool.....sikatai kuwa baba yake alimpa viwanja sehemu nzuri...lakini naye ana akili ....alitumia viwanja vyake kuanza biashara ya kujenga na kupangisha nyumba....na kwa wale msiojuwa biashara hii ..unahitaji tu kuwa na eneo prime...mtaji wa kujenga unapewa na benki...wanabaki na hati...,na wengine wanakutaka malipo ya rent yapitie kwenye akaunti yao...its a good deal ...ukiamua kuuza nyumba unapata pesa maradufu......
Pia kitendo cha hussein kuweka jina lake kwenye mradi ni cha kupongezwa.....kwani angeweza kuandika jina la muhindi pale na msingejuwa....tuache wivu...tuwaunge mkono wenzetu pale wanapofanya mambo kwa uwazi..ili ku encourage ....wengine pia wawe wawazi!!!
Tabia ya kuita kila mtu fisadi inasababisha unafiki kwa viongozi ....tunawajuwa kina msutya wana hadi magorofa JAPAN....kwa ajili ya unafiki kaama huu...tumpongeze kijana amekuwa muwazi na anafanya juhudi kuongeza kile alichopewa na baba yake kama mbegu!!.....NADHANI furaha yenu mngependa kuona anauza na kutawanya ovyo kama teja!!!
kwa wale wenye maeneo sehemu nzuri na hawajui cha kufanyia ni bora wakaomba ushauri tu.....angalieni hata kijitonyama ,mwenge etc magorofa yanapanda ovyo...wengi wanakopa ..si mafisadi wote!
kinachofanyika sasa hivi ni kuhalalisha fedha haramu kwa kuingiza kwenye biashara halali. (haihusianina masuala ya mwinyi), inakuwa pale mtu anaiba bilioni 1 ya fedha za umma halafu anaenda kujenga nyumba za kupanga, sasa akiisha jenga nyumba ya kupanga wale waliobiwa (wananchi) wanajipanga kutoa pongezi kwa jinsi alivyowekeza. Hawajui kwa kufanya hivyo wamehalalisha ule wizi na hivyo kuwafanya watu wengine nao watumie mbinu hiyo hiyo.
Inakuwa ni sawa na mtu ambaye anakuja na kukuibia jogoo lako, halafu wewe unakosa kitoweo halafu anarudi anakuuzia jogoo aliyekaangwa vizuri na limau kibao, kwa bei ya juu kuliko wewe mwenyewe ulivyotarajia. Kwa vile unaona amechukua muda kumkaanga jogoo yule na kumtia limau na mdalasini basi unafurahia kununua kitoweo hicho japo wajua jogoo ni lako!
Kiranga,
Nimesema siko Tanzania kwa sasa kwa sababu nilidhani watu wataniuliza ushahidi ambao najua unaweza kupatikana kirahisi . Lakini kama ni kutetea speculations zangu, hilo jumba la Mwinyi pale Seaview nimeshaonyeshwa mara nyingi, na nijuavyo lilikuwa mali ya National Housing kabla ya Mwinyi kuamua kuwarudishia wahindi nyumba zao zilizochukuliwa wakati wa utaifishaji. Nimekaa Upanga kuanzia mwaka 1973 na najua pale hakukuwa na open space, kama alivyosema August. Kwa hiyo ni wazi Daktari alipewa hilo jengo na baba yake. Asingeweza kulinunua kwa sababu wakati baba yake anakuwa rais mwaka uliofuata alienda kusomea udaktari Uarabuni. Unless mtu aniambie kuwa alirudi na mabilioni ya dinars kutoka kwa Waarabu, highly unlikely. Kwa hiyo kama ni kutetea speculations zangu I stand to be counted..
Hata jengo lake jingine pale Mikocheni kuna wazalendo walinionyesha.
kama Ujasusi wako kusema Dr. Mwinyi kasomea Uarabuni..basi wewe si Jasusi ni Unafanana na Shigongo..kwa Udaku..km ukisema hujui huwezi kuitwa Mjinga...!!!Kiranga,
Nimesema siko Tanzania kwa sasa kwa sababu nilidhani watu wataniuliza ushahidi ambao najua unaweza kupatikana kirahisi . Lakini kama ni kutetea speculations zangu, hilo jumba la Mwinyi pale Seaview nimeshaonyeshwa mara nyingi, na nijuavyo lilikuwa mali ya National Housing kabla ya Mwinyi kuamua kuwarudishia wahindi nyumba zao zilizochukuliwa wakati wa utaifishaji. Nimekaa Upanga kuanzia mwaka 1973 na najua pale hakukuwa na open space, kama alivyosema August. Kwa hiyo ni wazi Daktari alipewa hilo jengo na baba yake. Asingeweza kulinunua kwa sababu wakati baba yake anakuwa rais mwaka uliofuata alienda kusomea udaktari Uarabuni. Unless mtu aniambie kuwa alirudi na mabilioni ya dinars kutoka kwa Waarabu, highly unlikely. Kwa hiyo kama ni kutetea speculations zangu I stand to be counted..
Hata jengo lake jingine pale Mikocheni kuna wazalendo walinionyesha.
kama Ujasusi wako kusema Dr. Mwinyi kasomea Uarabuni..basi wewe si Jasusi ni Unafanana na Shigongo..kwa Udaku..km ukisema hujui huwezi kuitwa Mjinga...!!!