Mradi wa mabasi yaendayo kasi DSM ilikuwa idea ya Mkapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mradi wa mabasi yaendayo kasi DSM ilikuwa idea ya Mkapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzito Kabwela, Mar 11, 2012.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Imeelezwa kuwa mradi huu wa mabilioni ya fedha ulibuniwa na kufanyiwa upembuzi yakinifu mwaka 2002.

  Mkurugenzi wa Mradi huo akihojiwa na Radio Clouds mwanzoni mwa wiki hii alisema hadi kufikia mwaka 2004 karibu kila kitu kilikuwa tayari kwa ajili ya mradi huo kuanza.

  Swali ninalojiuliza, Serikali ya awamu ya nne inakaribia kumaliza nusu ya ngwe yake ya mwisho na bado dalili za kuendelea mradi huu hazipo. Je, ni kwamba serikali imefuja pesa za mradi huu muhimu? Na kwanini serikali ya awamu ya nne ijigambe kuwa wao ndio wenye mradi huu wakati huu ulikuwa mwendelezo wa jitihada na ubunifu uliotukuka wa Benjamin William Mkapa?

  Na kama hata mradi huu sio wa serikali ya awamu ya nne serikali hii itamaliza muda wake kwa kutekeleza mradi gani muhimu wa kuukumbuka?
   
 2. B

  BMT JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  japo jf wanamponda mzee mkapa ni kichwa katka hotba yake kwa halmashauri kuu ccm dodoma 25 agosti 2004-USHUPAVU WA UONGOZI!alitaja sifa kuu nne za kiongozi ya kwanza!kiongozi lazma awe na upeo mkubwa wa kubuni malengo na dira!!awamu ya nne inajipanga kukamilisha mradi huo,
   
 3. k

  kuzou JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  haijalishi,ni,idea ya ccm. kwa maana ni wataalamu walioserekalini ndo walobuni na kumshauri lbd waziri kupitia baraza la mawaziri(kikwete alikuemo)ukapitishwa.kwa kifupi mradi fulani ni mafanikio ya serikali nzima huwezi sema ni mkapa peke yake, mfano uwanja wa taifa mkapa aliomba msaada china,kikwete alifuatilia ombi kama foreign minister na ndo yeye alitia sahihi msaada kwa niaba ya tanzania kbl ya ujenzi
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,876
  Trophy Points: 280
  idea yote hii ni upuuzi, treni zetu za mizigo kusimamia tumeshindwa.
  Tuache utopian thinking twendeni tukalime.
   
 5. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkapa alikuwa kichwa. Baadae tutajua
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Mar 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mradi ni wa serikali haijalishi ni serikali ya awamu gani. kuna miradi ambayo mkapa aliirithi toka kwa mwnyi na kuna miradi ambayo kikwete aliirithi toka kwa mkapa na rais ajaye atarithi miradi toka serikali ya Kikwete. Mkuu Mkapa ana sifa ya kujenga Daraja la Mkapa lakini kumbukumbu ni kwamba mradi huu ulianza enzi za mwalimu! Hivyo basi haijalishi.

  Huyo mkurugenzi hakisema ni kwa nini mradi umechelewa tangia 2004! Nijuavyo huo mradi unafadhiliwa na benki ya dunia kwa maana hiyo suala la kula pesa nadhani halipo hapo; bank huwa inaangalia pesa zake kwa macho zaidi ya matano.

  Kuna thread kwenye projects inaongelea suala hili; pitia mkuu.
   
 7. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  NI KWELI MRADI UNAFADHILIWA NA BENKI YA DUNIA. BENKI YA DUNIA IPO MAKINI SANA KUZUIA UBABAISHAJI. INAPOHISI AINA YEYOTE YA UBABAISHAJI AU UBADHIRIFU, MARA MOJA HUZUAIA FEDHA ZAKE. KWA MAONI YANGU NI KWAMBA BAADA YA HUYU JAMAA KUINGIZA SERIKALI YAKE NA KUWACHAGUA AKINA MREMA KUWA WATENDJI WA TANROADs, NDIPO UBABAISHAJI ULIPOANZA NA KUPELEKEA JAMAA KUZUAI PESA YAO. MARA PESA INAPOZUAIWA, KUWASHAWISHI WAIRUDISHE HUWA NI KAZI NGUMU MNO. MARA NYINGI MATUKIO YA MTINDO HUO YAMEPELEKEA MIRADI MINGI KUFA KIFO CHA MENDE [MIGUU JUU].
  KWA UCHACHE LABDA TUUENDELEZE HUO MRADI KWA KODI ZETU BADALA YA HIZO ZA WORLD BANK!!
   
 8. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa mradi ni wa serikali. Tofauti ni mbinu na utayari wa kutekeleza. Mkapa na serikali yake ilikuwa na uwezo mkubwa wa kutekeleza yaliyoachwa na marais wastaafu, pia walikuwa na uwezo wa kubuni miradi mingi. Hili halipingiki na litaendelea kubaki hivyo na sifa hiyo itabakia kuwa hivyo. Serikali yake ilikuwa makini katika utekelezaji akimtegemea Magufuli (kama sijakosea) na timu yake katika masuala ya miundombinu. Miradi mikubwa waliyoibuni tayari chanzo cha fedha kilikuwepo ni suala la utekelezaji tu.

  Kuna mradi mmoja wa kujenga nyumba za watumishi katika wilaya mbalimbali nchini ambao ulibuniwa wakati wake na fedha zilikuwepo hata ujenzi ulianza kwa baadhi ya wilaya.. Nakumbuka huu ulikuwa mpango mbadala baada ya kuuziana nyumba za serikali (yalikuwa mawazo yao). Kama ungetekelezwa ungekuwa na manufaa makubwa kwa watumishi wa hali ya kawaida hususan wilayani.

  Utawala wa JK umeshindwa kutekeleza hayo hata kama chanzo cha fedha kilikuwepo. Zile nyumba mpaka kesho zimeishia vile vile hakuna mwendelezo wowote. Ilikuwa ni miradi endelevu na yenye mantiki na hivi ndivyo Ben atabaki kuwa bora, pamoja na mapungufu yake ya kuruhusu akina JK kwenye suala la EPA, pia nyumba za serikali na NBC.. Ila tutamkumbuka kwa mipango yake thabiti na uwezo mkubwa wa kusimamia mipango hiyo na kusimamia ukusanyaji wa mapato. Nakumbuka mzee wangu aliniambia kuwa kipindi cha Ben alikuwa na uwezo wa kutekeleza malengo ya serikali kwa miaka miwili mfululizo bila kuyumba hata kama wahisani wangegoma kuchangia bajeti. Leo hii huo uwezo upo?

  Alipoachiwa JK hatukutakiwa kurudi nyuma kiasi hiki. Tulitegemea awamu ya kwanza angemalizia yale yote aliyoachiwa na yeye angejikita kwenye bandari, reli, airport, nishati kwa vitendo, pia kurekebisha pale Ben alienda kombo nk.
   
 9. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mr Benjamin W. Mkapa my role modal we will remember you forever, as you can see you will remain in the hearts of Tanzanian, be blessed father
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mradi wa Rapid Bus Transport wa jiji la Dar ungekuwa mradi wa mfano kama planning ya mradi huu ungefanywa vizuri.
  Ni kweli lazima tumshukuru sana Mzee Mkapa kwa kubuni mambo mengi yenye umuhimu kwa Taifa.
  Hatutamsahau Mkapa kwa kuanzisha TANROADS,TRA na huduma nyingi ambazo Kama zingeendeshwa vizuri, utawala bora kwa wananchi ungeendelea kuwa mzuri.

  Mradi huu wa Mabasi ya kazi jijini kwa Leo ni kielelezo cha very poor planning kwa waliopewa kuendeleza mradi huu.
  Mambo yafuatayo yamedhihirika:

  Vituo havijulikani vitakuwa wapi-mradi hauna hati miliki ya sehemu za ujenzi

  Wakandarasi wameteuliwa na kupewa kandarasi kabla hata maeneo ya mradi kujulikana

  Mradi kuendeshwa kwa mtindo wa "management by crisis"-matatizo ambayo yangepaswa kutatuliwa wakati wa planning stage yana usumbua sana mradi.

  Kwa mwenendo wa mradi kwa sasa sitegemei matokeo mazuri na ya wakati katika mradi huu, maelezo, visingizio generally poor project management ndio vinavyo tawala.

  [/LIST]

  [/LIST]
   
 11. B

  BMT JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  wakati mwingine najisemea kama katiba ingekuwa ina ruhusu ni bora angepewa miaka 5 tena ya kutuongoza,,pamoja na lipumba kuwa mtaalamu wa uchumi duniani lakini uwa anasema waz kuwa mkapa aliweza kufanya vizuri sana kukuza ,kuimarisha uchumi wa tanzania,,jk wetu anaonekana kupwaya sana,may be anaweza kufkia malengo
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Pia alikuwa mwizi. Hili tumeshalijua.
   
 13. B

  BMT JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  we jasusi hebu nambie wale ambao unaamini si wez wamefanya nini?
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,120
  Likes Received: 6,600
  Trophy Points: 280
  mkapa alikuwa kichwa, ana ndiye aliyemgeuza hata akawa fisa di.
   
Loading...