Mradi wa kukodisha tractors - maeneo gani yanalipa?

MOTD

New Member
Nov 22, 2011
3
0
Wakuu salaam!

Naomba kwa wenye ufahamu wanisaidie yafuatayo:

1. Ni maeneo gani yanalipa ukipeleka trekta la kukodi?
2. Ni kiasi gani kwa heka moja?
3. Na ni HP ngapi zinaweza kufanya kazi (2wd or 4wd)
4. Chochote unachoweza kuchangia

Natanguliza shukrani
 
Ifakara mkuu. 4wd ndio safi zaidi, kwani baada ya kilimo kuna kuvuta magogo na maliasili nyingine. HP angalia zaidi ya 105, chini ya 90 ni kasheshe, labda ikakatue mabonde ya mpunga mpunga. Bei za mwaka jana ilikuwa elf50 kwa heka.

NB: hakikisha uko tayari kukaa porini. Ukimkabidhi mtu utalia machozi ya damu. Hesabu za tractor hazithibitiki, usije kuambiwa umelima heka 4 siku nzima, kumbe wazee wamelima 15.
 
Hili siyo tatizo tena,modern tractors zinayo GPS tracking device inayokuwezesha
kujua ukubwa wa eneo lilolimwa pamoja na masafa kati ya shamba na shamba. Hata hivo Ukizingatia bei ya mafuta,vilainisho,spare na kuchakaa kwa tractor biashara ya kukodisha tractor hailipi sana ukilinganisha na kulitumia kulima shamba lako mwenyewe mfano eka 50 hadi 100 za mpunga.
 
Hapo inabidi akomae mwenyewe hata akimwamini ndugu lazima amlize tu.
Mfanyakazi atanunua tractor jipya wewe tajiri lako linachoka hata ghalama inakuwa haijarudi.
 
NB: hakikisha uko tayari kukaa porini. Ukimkabidhi mtu utalia machozi ya damu. Hesabu za tractor hazithibitiki, usije kuambiwa umelima heka 4 siku nzima, kumbe wazee wamelima 15.

Hili siyo tatizo tena,modern tractors zinayo GPS tracking device inayokuwezesha
kujua ukubwa wa eneo lilolimwa pamoja na masafa kati ya shamba na shamba. Hata hivo Ukizingatia bei ya mafuta,vilainisho,spare na kuchakaa kwa tractor biashara ya kukodisha tractor hailipi sana ukilinganisha na kulitumia kulima shamba lako mwenyewe mfano eka 50 hadi 100 za mpunga.
Dah chief uko deep, lakini sasa bei ya hizo modern tractors si ndio £12,000 kuendelea? ukijumlisha £2500 za kulituma.... hapo si chini ya milioni za kitanzania Sasa return yake hapo ni miaka mingapi ya kilimo, kwa kuwakodioshia watu...
Kulima mwenyewe ni poa sana, ila kama mambo hayajakaa sawa inabidi uwalimie na wengine wachangie kurudisha gharama za manunuzi ya Tractor...
 
kaka nimekuelewa lakini ebu jaribu maeneo ya kibaigwa na manyara udongo wake sio mgumu wa kuuwa mashine na mahitajio ni makubwa mno.Wanakolima mpunga ni hatari kwa mashine
Pia nakushauri kama bado ujakaa sawa tafuta mtaji wako wamafuta kakopeshe mafuta yaani unawalimia then ulipwe mazao baada ya navuno inalipazaidi kuliko kulipwa cash
 
Wakuu nawashukuru saana... nilikua nategemea kutumia Trekta zangu mbili (MF165 na nyingine MF 290 zote 2wd), naendelea kupokea na kuchanganua michango yenu

Nawashukuru!
 
4WD ni bora zaidi,mimi nina uzoefu na ifakara na bei kwa sasa kibua ni 40000 na sare ni 45000!! Ila sie kushauri ufikirie sana kukodisha trekta ila kwa mwanzo itakusaidia kupata mtaji wa mafuta na kusoma mazingira...Ushauri tafuta eneo ambalo utakuwa unakodisha kwa mchana alafu usiku unalima mashamba yako, kwa njia iyo utatoka mkuu
 
tractor for sale in zanzibar. Massey ferguson 1104. 110 hp. 2 wd. made in england . good condition. price 10100 usd. low price for fast sale. contact for more information +255773420188
 
Back
Top Bottom