Mradi wa Gesi "LNG Lindi": Serikali inatarajiwa kutia saini mkataba wa Trilioni 70 hivi karibuni

Peter Madukwa

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
3,135
2,471
Serikali ya Tanzania hivi karibuni inatarajia kutia saini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa gesi asilia "LNG (liquified Natural Gas) Lindi" wenye thamani takribani dolla za Marekani Billioni 30 (trillioni 70).

Kwa mujibu wa gazeti la daily News, mradi huu mkubwa wa gas asilia pamoja na mambo mengine unatarajiwa kuleta matokeo makubwa ktk sekta ya nishati, viwanda, miundombinu, Kilimo, huduma za kijamii na kuongeza wigo wa ajira kwa watanzania.

Aidha, pamoja na mambo mengine serikali inatarajiwa kupata faida kubwa itakayotokana na faida ya mradi huo kwa gawio la zaidi ya 50%.

Mradi huo pia unatarajiwa kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi ktk mikoa ya kusini mwa Tanzania hasa ktk mkoa wa Lindi.

#KAZI IENDELEE
IMG-20220605-WA0042.jpg


Updates: 11.2.2022 Serikali imeasaini makubaliano ya mradi wa gas asilia wa LNG na kampuni ya Equinor

20220612_151514.jpg
Screenshot_20220605-210750_Adobe Acrobat.jpg
Screenshot_20220605-210628_Adobe Acrobat.jpg
 
Yaani kiukweli ni kuwa tutaanza pata hizo asilimia 50 baada ya hao jamaa kurudisha gharama zao
 
Huu mradi bora usitishwe tu.kwa aina ya viongozi tulionao hawa lazima tupigwe tu.Tulidanganywa gesi ya mtwara ingeleta mageuzi makubwa lakini wapi.

Kila sku umeme haueleweki.kama hatuwezi sisi kuichakata bora tuachane nao huu mradi kuliko kuwanufaisha mabeberu kila SKU.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mradi wa gas Mtwara huwezi kufananisha na mradi mkubwa huu wa Lindi.

Ni vitu viwili tofauti kabisa
 
Ata gesi ya mtwara walisema italeta mageuzi makubwa ya uchumi mtwara na mikoa jirani tokeo ni bila bila.

Ata migodi ya geita ma shinyanga walisema italeta mageuzi ya kiuchumi tokeo ni bila bila.

Ccm ni ile ile
 
Back
Top Bottom