[/COLOR][/FONT]
Sasa hapa umefafanua hivi...then
Ikiwa kama Taifa letu halina Infrastructure za kufanya transmission (kwa sababu Wachina waimiliki kwa 65%) kuna uhakika gani kuwa contents za TBC zitarushwa kwenye hiyo mitambo ya Wachina na sio Wachina waje na Contents zao? na pia Je itarushwa kwa gharama nafuu?
Watanzania wengine wenye kipaji na uwezo wa kutengeneza Contents kwa gharama nafuu, wataweza vipi kumudu vizingiti vya 1; gharama na 2; vigezo vingine vitakavyowekwa na hao wamiliki?
Hey, inaonekana unazungumza kinadharia zaidi kuliko hali halisi. Katika mazingira "perfect" hilo unalosema linawezekana, lakini tukiangalia mifano ya mikataba yetu na utekelezaji wake Tanzania....kuna dalili kuwa tumejifunza lolote?? Sidhani...
TBC ilitakiwa imili 100% au kama ingeshindwa kabisa basi wao Wamiliki 65% na Wachina 35%.
Itizame hivi. Sasa hivi nikiwa na idea ya show, nina options mbili:
1. Nianzishe TV/Radio station (ninunue mitambo, niombe leseni ya masafa, wafanyakazi, na gharama zihusiano.
2. Nitengeneze show, kwa gharama yangu, niipeleke TBC au ITV n.k, kuwauzia idea wanisaidie kui-air (nadhani ndio business model ya kina Benchmark na Maisha Plus)au nitengeneze pilot kwa bei rahisi (camera za kawaida) halafu niwaconvince wenye TV station wanibackup kwa budget n.k kutengeneza show nzima na ku-air the product.
Kuhusu swala la TBC, ambayo kwenye mfumo mpya watakuwa wanafanya biashara ya content, kutumia infrastructure ya star media, kinadharia they have no obligation to. Kama ITV/StarTV au mtu mwingine yoyote mwenye biashara ya transmission atawapa a better deal wanaweza kwenda huko. Mchina anaweza kurusha content zake kwenye hiyo infrastructure pia, akiwa na leseni ya content. Kwa hiyo TBC, mchina, na mimi na wewe tutaweza kupitisha content zetu humo humo kama station/channel tofauti.
Kuhusu gharama...kinadharia zinabidi ziwe nafuu zaidi. Hali ilivyo kwa sasa, kizingiti kikubwa sana kwa a creative type mwenye idea lukuki za TV show ni teknolojia na mitambo. Huoni inakuwa rahisi kwa huyo mtu kutengeneza content zake bila kujali mambo ya madish, transceiver na spare part zake? Pia, kinadharia, vizingiti vya hao watu wa trasmission vinatakiwe viwe ni vile tu vilivyokubaliwa na TCRA. Kwa sababu kama kila mtu anayefanya biashara ya content ataona ni bora kuwa na mitambo yake, then hamna maaana ya hii switch. Kama nilivyosema hapa ITV na Star TV wameungana kufanya hii biashara, kwa hiyo content zao zitapitia humo. Kwa haraka haraka utaona faida kwa wote wawili, maana wataunganisha technical department and hence kupunguza gharama, na hawata hutaji kila mmoja kuwa na masafa yake, which, masafa ambayo siyo tu ni ya gharama, lakini yanakwisha. Halafu watafocus kwenye kutengeneza content za maana na competitive. Na pia wana chanzo kingine cha mapato kwa kuruhusu watu wengine kutumia miundombinu yao. Ubaya ni kwamba mtu wa nje ya huu muungano itamwia vigumu kutumia huduma zao za transmission, while at the same time expected to compete with them on content. Again hapo TCRA itabdi wafanye kazi.
A lot of this is "in theory" or logic. Lakini kama ulivyosema kwenye Tanzania yetu anything is possible.