Mradi wa Digital Broadcasting TBC

Mradi wa Digital Broadcasting TBC

This is good. Tatizo mambo ya nchi hii inatuweka hasara sana kabla mambo hayakaa sawa. Nilikuwa na dikoder ya GTV. Jamaa wakafunga ofisi wakatuacha hewani mpaka leo. Nikajiunga na DSTV shingo upande kwa sababu jamaa ni ghali sana na wameendelea kuwa ghali kwa sababu hawana compititors. Nikaona wananifilisi bure nikaachana nao. Nimebeki na madicoder ambayo sina kazi nayo. Hii iki take off vizuri nitatupa hayo matakataka ya DSTV. Muhimu waache uhuni wafanye kazi na sisi tutawaunga mkono
 
....Tulidhani Tumepata Kumbe Tumepatikana .... !!!😡 😡
 
Na mimi nimenunua ka startimes decorder kako clear hata local channe;
 
Mimi ndio kwanza nimemenunua hicho king`amuzi hapa Arusha na wakasema wataanza rasmi leo, ila wasiwasi wangu ni uendelevu wake na utapeli kama wa GTV. DSTV wana bei za juu sana kutokana na kukosa ushindani kama ilivyokuwa TTCL kabla ya makampuni ya simu hayajaingia. Tuone, mimi na amini vita vya panzi furaha kwa kunguru. Big up na wengine wajitokeze.
 
Mkuu shida ya viongozi wetu wengi kwenye taasisi za umma hawajakaa kijasiliamali.

Inawezekana labda ni kutokuwa makini, au ukosefu wa mtaji (?) au teknolojia.

Hivi hawa ndo Startimes? nimenunua decoda yao! ukiondoa TBC BBC CCTV na france24 zilizobaki nikatuni tu! au nimeuziwa decoda ya chekechea?
 
Hivi hii tbc 2 ndio wameshindwa kuiweka sawa au inakuwaje? Au hapo ndo imekamilika? Test hadi lini? Si rais alishazindua? Mbona haina ubora kama tbc 1? Hawa jamaa wanaboa. Sie wengine tunataka kuona marudio ya mechi ila ubora wa picha unaharibu. Kama wapo hapa watuambie maana hata namba zao walizotoa hazipatikani
 
Back
Top Bottom