Nipe Maji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 335
- 190
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Charles Mahera, amefunga rasmi mafunzo ya matumizi bora na salama ya vifaa vya TEHAMA kwa walimu wa shule za msingi, yaliyotekelezwa kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Aprili 29, 2025 katika ukumbi wa Shirika la Elimu Kibaha mkoani Pwani , Dkt. Mahera amesema jumla ya washiriki 1,800 wakiwemo Maafisa Elimu Kata 600, Walimu Wakuu 600, na Walimu wa TEHAMA 600 kutoka Halmashauri zote 184 wamepatiwa mafunzo hayo kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kufundisha na kujifunza kwa kutumia TEHAMA.
“Deni lililobaki kwetu Wizara ya Elimu na Ofisi ya Rais TAMISEMI ni kuhakikisha kuwa kila mmoja anatumia maarifa, uwezo na vifaa tulivyo navyo kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bora, yenye ubunifu, inayowaandaa kwa maisha ya sasa na baadaye,” alisema Dkt. Mahera.
Ameongeza kuwa, Rais Dkt. Samia ameendelea kuwekeza katika elimu kwa kujenga shule mpya, kuongeza vyumba vya madarasa, kuimarisha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, pamoja na kutoa ajira kwa walimu. Sisi kama wasimamizi wa sera na utekelezaji tunapaswa kuhakikisha dhamira hiyo ya Rais inatekelezwa kwa vitendo.
Dkt. Mahera pia ametoa wito kwa wakurugenzi wa Halmashauri kuweka mikakati ya kuimarisha usimamizi wa TEHAMA katika shule, kuhakikisha vifaa vinatunzwa na kutumika ipasavyo.
Amehimiza pia kuhakikisha huduma ya chakula inapatikana katika shule zote za kutwa ili kuongeza usikivu na ufanisi wa wanafunzi.
Mafunzo haya yanaendana na maboresho ya Sera ya Elimu ya mwaka 2014 toleo la 2023, ambayo inasisitiza matumizi ya TEHAMA na kuongeza viwango vya sifa za walimu kuanzia elimu ya awali hadi sekondari.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Awali na Msingi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi Suzanne Nusu, amesema shule zote 800 zitakazopokea vifaa vya TEHAMA zinapaswa kuhakikisha vifaa hivyo vinatunzwa, vinatumika ipasavyo, na vinanufaisha pia shule jirani.