Mradi wa "AFCON City" Arusha: Ni Upigaji au uzembe? Wananchi tumelipa mamilioni, viwanja vimebaki kuwa pori!

Mradi wa "AFCON City" Arusha: Ni Upigaji au uzembe? Wananchi tumelipa mamilioni, viwanja vimebaki kuwa pori!

nimechafukwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
290
Reaction score
237
Wana-JF,
Mnamo Agosti mwaka huu, Serikali kupitia Wizara ya Ardhi ilitangaza fursa kubwa kwa wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla. Tulitangaziwa uuzaji wa viwanja katika eneo la Olmoti/Oloresho, eneo ambalo limezunguka uwanja mpya wa kisasa wa Samia Suluhu Stadium.

Lengo lilikuwa ni kutengeneza mji wa kisasa, "AFCON City," ambao utakuwa kioo cha nchi yetu wakati wa mashindano ya AFCON 2027. Sisi kama wadau tuliupokea mradi huu kwa mikono miwili tukiamini ni wakati wa kuichangamkia fursa.

Mwili wa Habari, Changamoto inaanza hapa: Wengi wetu tushajilipia viwanja hivi kwa gharama kubwa sana. Bei ya chini kabisa ilikuwa Shilingi 27,000 kwa Square Meter. Hizi ni fedha nyingi ambazo wananchi wametoa wakiamini wanakwenda kuwekeza kwenye miundombinu iliyoandaliwa.

Hadi tunavyozungumza sasa, hakuna kinachoendelea eneo la mradi. Hakuna barabara, hakuna maji, wala umeme. Ukifika eneo la mradi sasa hivi ni aibu, ni pori tupu! Watu walionunua maeneo yale wana malengo ya kujenga Hotels, Airbnbs, na makazi ya kisasa ili kuendana na hadhi ya mashindano. Sasa utajengaje katikati ya pori pasipo na miundombinu?

Nimefika ofisi za Ardhi Mkoa wa Arusha mara kadhaa kutafuta majibu, lakini majibu ni ya kusuasua. Wanasema wanajipanga na kusubiri fedha kutoka Serikali Kuu. Hivi inawezekana vipi watu wamelipia viwanja kwa mamilioni, halafu Serikali ishindwe kurudisha asilimia ndogo ya fedha hizo kwa ajili ya kufungua barabara na kuweka huduma muhimu?

Maswali ya Kuhitimisha

* Je, Wahusika wanajua kuwa AFCON imebaki mwaka mmoja tu kuanza? Mnategemea mwekezaji ajenge hotel ya hadhi ya kimataifa ndani ya miezi sita?
* Nani anakwamisha maono haya? Rais Samia aliahidi kwa dhati kujenga mji huu wa kisasa (AFCON City), lakini watendaji wa chini mkoani na wizarani wanaonekana kulegalega.
* Mmeona maandalizi ya wenzetu wa Morocco (AFCON 2025)? Miji yao imeshanyooka, miundombinu iko tayari. Sisi kwanini kila kitu kiwe "zimamoto"?
Tunawaomba viongozi wawajibike. Hatuwezi kuwa na uwanja wa bilioni 300 katikati ya pori lisilopitika. Arusha ni jiji la kitalii, na hili ni eneo la kimkakati. Nani katuloga?
#AFCON2027 #ArushaCity #WizaraYaArdhi #SamiaSuluhuStadium #Tanzania
 
Hakuna cha afcon wala dada yake na afcon,Rwanda ajiandae kuhost kama mbadala wa Tanzania.

Mmepigwa na utapeli wa serikali ya muuaji
 
Back
Top Bottom