Mradi unaodhaminiwa na China waibua maisha mapya katika Hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai nchini Tanzania

Mradi unaodhaminiwa na China waibua maisha mapya katika Hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai nchini Tanzania

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,242
Reaction score
1,212
1747033730407.png


Kwenye ukingo wa Bonde la Ngorongoro nchini Tanzania, ukungu unaonekana kutanda kwenye uwanda huku makundi ya nyumbu na pundamilia wakirandaranda chini. Kutoka kwenye jukwaa jipya la kuangalia wanyama, wageni kutoka duniani kote sasa wanapata fursa ya kutazama kwa kina pamoja huku pembeni kukiwa na vibao vilivyoandikwa kwa Kiswahili, Kiingereza, na Kichina, ishara inayoonesha mabadiliko ya taratibu lakini yenye nguvu.

Hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai (Geopark) inayotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambayo hapo awali ilikuwa kwenye hatihati ya kupoteza hadhi yake kwa UNESCO, sasa inafufuliwa kupitia mradi wa kwanza wa Hifadhi ya jiolojia kupitia msaada wa kigeni wa China.

Mradi huu ulizinduliwa Juni 2023 baada ya hifadhi hiyo kupokea onyo la kadi ya njano kutoka UNESCO mwaka 2022. Matatizo yaliyoiandama hifadhi hiyo yalikuwa ni miundombinu duni kwa wageni na maudhui yasiyotosheleza ya kisayansi.

Juhudi hizo ni pamoja na uungaji mkono wa kisayansi na kuboresha miundombinu ili kurejesha hadhi ya hifadhi hiyo kimataifa huku ikiimarisha uhifadhi, elimu na utalii. China kupitia Kituo cha Tianjin, cha Utafiti wa Jiolojia wa China na miundombinu kinachoshughulikiwa na Kampuni ya Reli ya China, iliitikia kwa kutoa usaidizi wa kiufundi.

"Ilikuwa uzoefu mpya kwa kila mmoja wetu, ilitubidi kufanya kazi kwa karibu na washirika wetu wa Tanzania kutatua changamoto za vifaa, kukabiliana na msimu wa mvua, na kufanya kila hatua kuwa sawa." alisema Xu Jiangbo, kiongozi wa kiufundi wa mradi wa miundombinu kwenye eneo la hifadhi.

Xu alibainisha kuwa kazi nyingi zimekamilika, akiongeza kuwa jumba la makumbusho, lililosanifiwa kama jengo la kihistoria la Jiopaki, linatarajiwa kufunguliwa Juni mwaka huu, na maonesho ya digitali, hadithi za kina, na maonesho ya kisayansi yatawaelezea wageni mageuzi ya Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, shughuli za kihistoria za mlipuko wa volcano ya Ol Doinyo Lengai, na alama za nyayo za Laet.

Msaada wa kiufundi utakamilika ifikapo Novemba, ambao utakuwa ni uchunguzi wa urithi wa kijiolojia, muundo wa maonesho ya makumbusho, na mafunzo ya wafanyakazi wazawa.

Simon Moses, fundi uashi mwenye umri wa miaka 48, aliongoza kikundi cha ujenzi katika eneo la makumbusho. "Nimejifunza mbinu nyingi mpya. Msimamizi wangu wa Kichina anaelezea kila kitu kwa uwazi," alisema.

Moses aliongea akiwa kifua mbele huku akionesha jumba la makumbusho, ambalo linachanganya mitindo ya kikabila ya Afrika, muundo wa Hekalu la Mbinguni la China na usanifu wa makazi ya Tulou Fujian. Jengo hilo pia lina teknolojia za kijani kama vile paneli za jua.

Chini kabisa kwenye mteremko, Elisante Hando, fundi msaidizi mwenye umri wa miaka 31, alikuwa akifunga taa kwenye jumba la makumbusho. “Nilijiunga miezi minane iliyopita ila sikujua kama ningejifunza mambo mengi hivi,” alisema. "Sasa, najua kutumia zana na mbinu mpya. Nahisi niko tayari kwa mradi wowote ule utakaokuja baada ya huu."

Maneno yake yalionesha faida kubwa ya kuwajengea uwezo vijana wazawa. "Mradi huu sio tu wa kujenga vitu; bali ni wa kujenga watu pia," Elisante alisema.

Neema Mollel, mwenye umri wa miaka 52 ambaye ni mmiliki wa hoteli na muongozaji mstaafu wa watalii, ameona umuhimu mkubwa zaidi katika mradi huo. Kama mwanachama wa jamii ya Wamasai, alishukuru kwa namna mradi unavyohifadhi urithi wa wenyeji.

"Mila zetu zimefungamana na ardhi hii. Sasa watalii hawataona wanyama tu, bali pia wataelewa hadithi zetu," alisema, akiongeza kuwa kwa uwepo wa alama bora, barabara, na vituo vya wageni, watalii wanakaa kwa muda mrefu, na kuongeza biashara zaidi kwa mahoteli na maduka yao.

Kitoi Mbise, mwalimu wa jiografia kutoka Arusha, aliuita mradi huo kuwa ni wa kubadilisha elimu. "Hifadhi hii inaibua uhai wa darasa langu. Sasa ninapofundisha kuhusu volkano au utalii endelevu, ninaweza kuonesha mahali halisi ambapo inafanyika."

Mbise alisema atatumia hifadhi hiyo kuelezea uhifadhi, kuonesha namna utalii unavyoweza kuinua uchumi, na kuwaelezea wanafunzi fani za sayansi ya mazingira na ramani ya kidijitali.

Kwa Anna Keller, mtalii wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 65, mabadiliko yanaonekana waziwazi. "Vituo ni safi, alama ziko wazi, na utamaduni unaoneshwa kwa heshima. Inafanya tuwe na uzoefu mzuri zaidi," alisema wakati alipotembelea eneo hilo na mumewe.

Sun Kai, naibu mkurugenzi wa Kituo cha Ushirikiano wa Sayansi ya Jiolojia Kusini mwa Afrika cha Kituo cha Tianjin, Utafiti wa Jiolojia wa China, alielezea imani yake kuwa mradi huo ni zaidi ya msaada.

"Ni mchango wa utaalamu wa China katika ulinzi wa kimataifa wa urithi wa kijiolojia. Na inaonesha ushirikiano wa maana unavyoweza kuonekana," alisema.

Wakati msimu wa utalii unapokaribia, Hifadhi ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai (Geopark) imejiandaa zaidi kuliko hapo awali. Volkeno zake za kuvutia, alama za nyayo za kale, na wanyamapori wanaopita huku na kule sasa wanaonekana wakiwa na hadithi mpya, hadithi za ushirikiano, kujifunza na heshima.
 
Back
Top Bottom