MPYA: Liyumba akwama tena Mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MPYA: Liyumba akwama tena Mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Jun 15, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba, amekwaa kisiki tena mahakamani baada ya serikali kushinda rufani dhidi ya uamuzi wa Hakimu Nyigulila Mwaseba aliyelegeza masharti ya dhamana.

  Hakimu huyo pia sasa hataendelea tena kusikiliza kesi hiyo.

  Jaji Godfrey Shaid alisema kifungu cha 148 (5) cha mwenendo wa makosa ya kijai (CPA) hakielezei kosa la wizi na kusababisha hasara tu hivyo masharti nafuu ya dhamana yaliyotolewa kwa Liyumba yalitolewa kwasababu kifungu hicho kilitafsiriwa vibaya.
   
 2. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  Jamani hata kama mtu anatuhumiwa ufisadi, dhamana ni haki yake! inaonekana kweli kuna mkono wa mtu nyuma ya kesi hii...Yaani dhamana ya mabilioni ya shilingi!! Ukomaliaji huu wa serikali ungekuwa unafanywa pia kwa kina Rostam nadhani mambo yangekuwa safi sana!
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hata kama ana matatizo yake mengine, lakini dhamana ni haki yake, mbona kama kuna kitu kinafichwa hapo.
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Afadhali yeye bado anaishi, kuna watoto na wanawake ambao wanakufa shauri ya kukosa dawa. Laiti mabilioni waliyokuwa wanajichotea yangetumika ipasavyo nchi yetu isingelikuwa hapo ilipo.

  Japo yeye ni dagaa tu katika nchi ya Manyangumi na Mapapa lakini za mwizi ni arobaini ya yakikukuta usilalamike.
   
 5. H

  Heri JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2009
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ningependa kuuliza , hivi imeshawahi kutokea kwa mahakimu kutolewa/kuondoka katika kusikiliza kesi zaidi ya mara moja within a period of meizi sita?
  Hawa mahakimu wanaodoka kwa shinikizo au rushwa au kutokubali pressures kutoka juu?
  Kwa maoni yangu binafsi PCCB/DPP hawakuwa makini wakati wakifungua hii kesi. Wana jaribu kuonyesha kana kwamba Liyumba anapata dhamana kwa njia isiyo halali.
  Wampe hiyo dhamana na waendeshe hiyo kesi haraka na ufanisi na waprove within reasonable doubt kama Liyumba ni guility.
  Tutaanza kusikia kuwa uchunguzi haujakamilika!
   
 6. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mahakama kuu ya TZ leo imefutilia mbali masharti ya dhamana ya Amatus Liyumba wa BOT iliyokuwa imetolewa na mahakama ya hakimu mkazi wa Kisutu na kuweka masharti mapya pia kuamuru kesi hiyo ipangiwe hakimu mwingine.


  Sasa Liyumba pamoja na masharti mengine atatakiwa kuweka dhamana ya nusu ya hasara ya kiwango cha pesa anazotuhumiwa kuisababishia serikali ambayo ni Bilioni 221, HIVYO DHAMANA YAKE NI ZAIDI YA BILIONI 110,
   
 7. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,809
  Likes Received: 2,514
  Trophy Points: 280
  kazi kwelikweli shemeji!!!!!!!!!!!!!!
   
 8. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  That law is impractical and essentially unfair..
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
 10. c

  cesc Senior Member

  #10
  Jun 15, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  tuache mkono wa sheria ufanye kazi yake...sisi ni watazamaji tu na mashabiki...
  mwisho wa yote lazima UKWELI UJULIKANE ...LAZIMA..AWE AMESHINDA YEYE AU AMESHINDWA...JUST WAIT..SOONER RATHER THAN LATER MAJIBU YATATOKA...
   
 11. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  This is unfair

  law society inabidi iliangalie hili

  inaonekana kuwa hii kesi inaendeshwa kisiasa zaidi ya kisheria

  naamini kuna mkono wa mtu kwenye hili...i dont know what huyo bwana is trying to prove lakini nina wasi wasi hii itakuja kuleta massive embarassment kwa serikali

  as time goes by inaonekana kuwa kuna kila sababu wanataka kumkomoa Liyumba lakini huko tunakoelekea siko kabisa.

  Somehing is not right hapa na mwisho wa yote haya huyu jamaa atakuja kuachiwa huru then atakuja kucounter sue then watakaokuja kumlipa fidia na gharama zote ni walipa kodi kisa? serikali inaendesha kesi kishabiki shabiki
   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Hii itafanya watu waanze kuiquestion serikali and this is the last thing watu wanakitaka huko serikalini

  hapa itaonekana kuwa kuna vendetta na who knows media wataanza kugeuza kibao na mwishowe sidhani kama utakuwa ni mzuri

  something fishy is going on hapa
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  whatever happened to presumption of innocence?

  my exact sentiments

  Tanzanian law is a joke! lakini sijui wanatumia vifungu gani kujustify haya wanayoyafanya

  sasa hakuna mahakama iliyoprove kuwa ameitia hasara BILIONI 221 sasa iweje leo anaambiwa alipe bilioni zaidi ya 100 kama dhamana?

  its abot time Liyumba akabadilisha lawyers amchukue SHIVJI maana serikali haiko serious na inachokifanya  hapa hakuna mkono wa sheria unaofanya kazi hapa ni wazi kuna kono wa Vendettas uko kazini na inasikitisha sana. Yes jamaa ametuhumiwa lakini hakuna mahakama iliyomhukumu sasa mbona anakuwa treated as GUILTY person

  Makes you question kama Liyumba yuko treated namna hii hao wengine wenye kesi za kubambikiwa na polisi wanakuwa treated vipi?
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mbona akina Mramba walilegezewa na wanapeta uswazi?
  Akina Jeetu Patel walilegezewa na wengineo wapo uswazi huyu Liyumba naona kuna kamkono ka mtu kamekaza pale....tuseme yeye peke yake ndo kaitia hasara serikali kwenye majengo hayo? Mbona Bodi nzima wapo uswazi wanapeta tu?
   
 15. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mkuu GT na wengine,

  Hii ya Liyumba ni moja tu ya matatizo mengi ya maamuzi ya aina hiyo. Kwa ujumla ni kweli kuna watu wenye matatizo kam Liyumba, Mramba, Mgonja, Yona, Mahalu, Maranda, Jeetu Patel na wengineo, na kuna wanaotafutwa (japo wana matatizo) kama vile Warioba na kundi lake, lakini je, ni hao tu katika matatizo luluki ya nchi hii?

  Je, Mgonja, Mramba na Yona walistahili kusota rumande bila dhamana kwa muda wote ule? Je, ni kesi walizoshitakiwa nazo zina mashiko?

  Majibu ni tata katika kila swali na kwa taarifa (si rasmi) kuna kesi itafutwa ifikapo Julai, 2009 na tutakumbushana na kama kuna namna ya kuweka alarm ikifika Julai, 09 tufuatilie ni sawa maana kama alivyosema GT ni kodi zetu zitakazolipa fidia serikali ikishindwa hizi kesi mahakamani. Hata zile za EPA, wale wenye kesi za kughushi ambazo ziko wazi, wanaachiwa, eti wamelipa!!!!?? upuuzi gani huo kwani Mahalu hata kwa kuchanga changa hawezi kulipa 2bn?

  Mtashangaa, maana hata wanasheria na wapelelezi wameshagundua sanaa, wamenuna
   
 16. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  ndio hapo!
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu ndo hapo napo choka na serikali yetu hii wanahubiri kila siku utawala bora kumbe ni vinyonga tu sijui wanamdanganya nani kama sio wanajidanganya wao wenyewe.
   
 18. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  LIYUMBA amchukue SHIVJI sidhani kama hii kesi itakaa zaidi ya miezi 2 mahakamani

  this is ridiculous utamwambiaje mtu aweke dhamana nusu ya pesa aliyoitia hasara serikali wakati hakuna mahakama iliyomtia hatiani kwatuhuma za huo wizi in the first place?

  mwanzo i thought hawa jamaa wanafanya DOUBLE JEOPARDY lakini i was wrong what we see here ni close to it

  mimi niko ok na watuhumiwa kushitakiwa na no matter how much nitakuwa nina tofauti na watuhumiwa i still believe they deserve to have equal treatment under the law

  what we see here is LAW OF THE JUNGLE at play

  hakuna zaidi jamaa wanataka kuprove a point ambayo haipo na kuendesha kesi based on feelings ni wrong
   
 19. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  I'm not sure what you mean! In my case I just think that to demand someone to post a bail of 110 billion is unfair considering the obvious, that is maybe 5 people in the whole of Tanzania can claim to have that much money! So in cases of 'causing loss' this rule which was designed for theft cases.. should not apply as it is blind and unjust (not in relation to Liyumba alone but just in general) It is rubbish, especially considering the slow pace of litigation and the massive hold up of cases. Someone might be in jail for a few years and then acquitted of the crime.. How can the law fix the unjust nature of such a thing..! This rule should be scrapped..
   
 20. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  hivi huyu Liyumba kashitakiwa kwa sheria ipi na ni ipi ambayo imetumika kumwambia aweke bond kubwa namna hiyo?
   
Loading...