MPYA: Liyumba akwama tena Mahakamani

tafadhali fafanua kwa kiswahili kwanza unamaana gani hapo...!

Nafikiri alimaanisha 'without reasonable doubt' si unajua tena this is not our mother tongue. Unajua kila kesi na merits zake. Hapa hatujui Liyumba aliplay role gani kwenye ujenzi huu. Tunajuaje inawezekana ma-QS, consultants etc walimpa ushauri alikataa. Mnakumbuka issue ya richmond, TANESCO lawama ziliwakwepa kwa kuwa wao walitoa ushauri uliokataliwa? Kwa nini kutokueleweka kwa kesi hii kunatazamwa tu kwa jicho la 'hapa kuna mkono wa mtu?' Pia sijaona connection ya Shaidi kuwa Jaji akitokea kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka na kesi ya Liyumba. Walikuwa na ugomvi naye? Kama sivyo then connection ni ipi?
 
Mseminari Liyumba si moja kati ya wana mtandao.

Liyumba aliajiliwa na BOT katika nafasi aliyokuwa nayo. Ujenzi wa majengo hayo pacha haukuchukua wiki mbili ama mwezi mmoja, bali umechukua miaka na kwa misingi hiyo ilikuwa rahisi kujua mapema kabisa kwamba gharama za ujenzi si halali, na ujenzi ungesimama kwanza kufanya uchunguzi wa gharama hizo. Hapa pana kasoro.

Kwani thamani halisi ya majengo hayo pacha ni kiasi gani?, nani alifanya tathmini hiyo?, na ni lini ilifanyika?.

Hii sheria inayotumika kwa liyumba kwanini isitumike kwa watu wengine waliotutia hasara?, kwa mfano Yona, Mramba, Mgonja na wahusika wa EPA?.
Nashindwa kuelewa kabisa kwamba ndani ya nchi moja kuna sheria mbili kuhusu kitu kimoja.

kinachonitia hasira zaidi ni kwamba hata kama Liyumba aliiba lakini majengo yenye hadhi na heshima ya kimataifa yanaonekana, sasa wahusika wa EPA na akina Mramba & Co wamefanyia nini mapesa yetu?. Pesa za Kagoda mpaka sasa hakuna aliyekamatwa na wala haliongelewi tena. Sasa kwanini huyu Liyumba aandamwe hivi?

Kuna mtu kama Chenge ambaye kaua kwa uzembe wa wazi kabisa, lakini mbona yuko mitaani. Kuna watu hawaguswi na sheria ndani ya Tanzania?. Inanisikitisha sana.
 
Back
Top Bottom