Mpwa wangu anatafuta mume wa kuzaa naye!

Mpwa wangu anatafuta mume wa kuzaa naye!

Mkuu mbegu ya aina yoyote, anachohitaji ni mtoto
Kwahiyo hata zeru zeru ni sawa sababu anahitaji mtoto? jamani na alikua wapi mpaka umri umekwenda? na sioni kama nisawa apate mtoto bila kulewa huyo mtoto akimuliza mama baba mlikutana wapi anasemaje? aliletewa kutoka JF?
wala sio tamu anayosababu yakukata kuolewa ebu ongeeninae tena.umesema ni msiri sana sasa nadhani mengine hakukwambia.
 
mjomba una mambo weye, upendwe kuitwa babu wewe umlazimishe mwenzio azae khaa
 
hapa naona huyu mama atakuwa na matatizo ya kisaikolojia maana haingii akilini kwa msomi kama yeye aliyeajiliwa bado anakaa kwa wazazi. kunauwezekano alipokuwa nasoma alikumbana na matatizo ya kimapenzi na yakahalibu fikra zake ndio maana hawazi sana. ni ajabu kwa mtu kama yeye kutokuwa na msisimko wa kuzaa na akaona ni sawa tu. kwa wanaume ni sawa ila kwa yeye may be anajua anatatizo gani katika maumbile yake pengine alishatoa kizazi kutokana nautoiaji wa mimba kuna maswali mengi kwa ujumla wewe mtumie mama yake anajua A to Z za mtoto wake.
 
binafsi kwa hapa kwetu iyo njia sina halkika sana nayo(ivf). lakin dada huyo mpwao huwa ni mtu wa kaujichanganya? huwa anatoka toka out,au hata yuko katika hii mitandao ya kijamii? mwambie hivi aingie humu jf halafu atulize kichwa chake kwenye kuchangia nakuhakikishia atavuna wachumba balaa tena wa umri wake nakuhakikishia.

:doh: hivi eee????
 
Mh, huyo lazima atakuwa na tatizo! 40 years? Nadhani huyo hana shida ya kuolewa, kwanza kwa umri wake kuzaa ni issue! Kwa nini asifanye kazi ya kumtumikia Mungu tu? Awe sister kama ni mkatoliki.
 
Tegelezeni pole sana kwa ajili ya mpwa wetu na kwako pia kukosa uhondo wa kucheza na wajukuu. Sitapenda kushauri mpwa huyo kukimbilia IVF ikiwa hajashindwa kupata mtoto kwa njia ya kawaida kwanza. Inavyoonekana ana matatizo ya kisaikolojia ama homoni, kwani kwa umri alionao mwili wake lazima ungekuwa ukimsumbua kutokana na mhemko hasa ktk kipindi chake cha joto.

Nashauri kwanza mtafutie washauri wa kisaikolojia pia nyumbani hapo ahame maadamu ana uwezo wa kujitegemea najua aliamua kuwa nyumbani hapo kulingana na mila na desturi zetu za kiafriaka binti hawezi kwenda kuishi peke yake kama hajaolewa bila sababu ya msingi angeonekana ni malaya.

Kama uko naye karibu jitahidi jioni baada ya kazi na siku za weekend uwe unamtoa kwa kumchanganya na jinsia tofauti ili aweze kuzoea wanaume, haijalishi hata kama alitendwa huko nyuma lazima ataanza kubalika, kuliko kumtafutia mtu ambaye hatampenda kwa dhati ila kutokana na shinikizo la kujiona kuwa sasa amekuwa na anatakiwa awe na familia yake.
 
Last edited by a moderator:
Ni mtoto wa kaka yangu, na amezaliwa na kukulia Dar, mimi sikuwa karibu naye na ni msiri sana. Nimekuwa nikizungumza naye mara kwa mara lakini sio muwazi na hiyo ilitokana na yeye kujiwekea mipaka.

Amesoma hapa nchini na nje ya nchi katika moja ya nchi za Scandinavia na sasa ni mwajiriwa serikalini. Sina uhakika sana umri wake lakini naamini ana zaidi ya miaka 40. Hivi karibuni nilishikwa na udadisi na katika mazungumzo na shemeji yangu,(mama yake) alinijulisha kwamba hata yeye na kaka yangu wanashangaa binti yao kutoolewa au hata kupata mtoto. Anakiri kwamba hawajawahi kumuona na mwanaume na hana mashoga wanaofika hapo nyumbani.

Nilimdadisi iwapo waliwahi kumuuliza kuhusu kuolewa, shemeji akanijibu kwamba waliwahi kumuuliza na akajibu kwa kifupi kwamba hajapata mume na kipata atawajulisha. Lakini tangu siku hiyo akawa hana raha na akawaambia wadogo zake kwamba wazazi wamememchoka na sasa wanamnyanyasa. (anao wadogo zake wawili wa kike ambao wameshaolewa na kuzaa)

Nilitoa wazo kwamba wamshauri japo apate mtoto, ushauri ambao aliukubali kwa mikono miwili, lakini ni nani wa kuzaa naye?

Nimeshauri hatua ya kwanza ahame hapo nyumbani akapange mbali na nyumbani ili awe huru na hapo atakuwa na fursa ya kupata mwanaume japo wa kuzaa naye. Amekubali na sasa anatafuta nyumba ya kupanga.

Lakini yuko worried kama atapata mwanaume mwaminifu ambaye sio mume wa mtu japo wa kuzaa naye tu basi. Ila swali lake aliuliza iwapo hapa nchini kuna uwezekano wa kufanyiwa IFV badala ya njia ya kujamiiana. Hilo sina uhakika nalo na ndio maana nimekuja hapa kutafuta ushauri..
King'asti , BADILI TABIA , gfsonwin , Yummy , nyumba kubwa , Nehondo , MwanajamiiOne , marrykate , AshaDii , NATA , FirstLady1 , TaiJike , na wengineo ambao sijawataja, naomba msaada wenu ili nimsaidie mpwa wangu

Mpendwa Tegelezeni, kwanza pole kwa hili linalokuumiza kichwa mpaka umeamua kutuletea hapa. Kwanza wewe umeoa?kama una mke unaonaje ukimchukua mkeo na mpwa wako muende sehemu ambayo ina mchanganyiko wa watu mkae mpige story halafu ujaribu kumuuliza maswali ya msingi(nna uhakika unayajua) ndio upate mwanga wa nini hasa anachokitaka. Inawezekana kabisa sio kwamba anaipenda hiyo hali lakini kutokana na mambo flani flani aliyowahi kuyapitia akaamua ni bora asiwe na mahusiano na mwanaume yoyote.
Swala la kwamba wazazi hawajawahi kumuona na mtu ni maamuzi ya mtu sio lazma akiwa na mtu aonyeshe wazazi. Inawezekana alishawahi kubakwa labda ndio maana hataki tendo la kujamiiana,kuna vitu vingi sana vinachangia kaka yangu, cha msingi kaa nae muongee kwa undani. Hata huyo mwanaume wa kumpa mtoto hawezi kukurupuka tu.....swala la kupima siku hizi ni muhimu sana sidhani kama hilo lina mjadala.
 
Last edited by a moderator:
ukishamtafutia na mie shemeji yangu anatafuta naomba naye umtafutie.

Jf kwa kuzunguka na C/o
 
Tegelezeni pole sana kwa ajili ya mpwa wetu na kwako pia kukosa uhondo wa kucheza na wajukuu. Sitapenda kushauri mpwa huyo kukimbilia IVF ikiwa hajashindwa kupata mtoto kwa njia ya kawaida kwanza. Inavyoonekana ana matatizo ya kisaikolojia ama homoni, kwani kwa umri alionao mwili wake lazima ungekuwa ukimsumbua kutokana na mhemko hasa ktk kipindi chake cha joto.

Nashauri kwanza mtafutie washauri wa kisaikolojia pia nyumbani hapo ahame maadamu ana uwezo wa kujitegemea najua aliamua kuwa nyumbani hapo kulingana na mila na desturi zetu za kiafriaka binti hawezi kwenda kuishi peke yake kama hajaolewa bila sababu ya msingi angeonekana ni malaya.

Kama uko naye karibu jitahidi jioni baada ya kazi na siku za weekend uwe unamtoa kwa kumchanganya na jinsia tofauti ili aweze kuzoea wanaume, haijalishi hata kama alitendwa huko nyuma lazima ataanza kubalika, kuliko kumtafutia mtu ambaye hatampenda kwa dhati ila kutokana na shinikizo la kujiona kuwa sasa amekuwa na anatakiwa awe na familia yake.

Si mchezoooo.......hii ndio JF bana kila kukicha kuna mambo tunajifunza! TaiJike sababu za msingi ni zipi ambazo ukiwa nazo hutaonekana malaya???!!! Nielimishe ndugu yangu maana mimi nilihama kwa wazazi kabla sijaolewa nikawa najitegemea, sikujua kama nilikua naonekana malaya kwenye jamii.
 
Last edited by a moderator:
Mh jamani kwa kweli nampa pole sana, But kama anataka kupandikiza, Hospital ipo masaki nadhani awe na kiasi cha dola 3000 tu ili apandikizwe mbegu na apate mtoto . Kuhusu mbegu sijui kama wanazo pale au unaenda na mwanaume wa mbegu.
 
Si mchezoooo.......hii ndio JF bana kila kukicha kuna mambo tunajifunza! TaiJike sababu za msingi ni zipi ambazo ukiwa nazo hutaonekana malaya???!!! Nielimishe ndugu yangu maana mimi nilihama kwa wazazi kabla sijaolewa nikawa najitegemea, sikujua kama nilikua naonekana malaya kwenye jamii.
Yummy sababu mojawapo ni kama ajira na iko mbali na nyumbani ni wazi utalazimika kuhama.
 
Last edited by a moderator:
lecturer wangu mmoja katika chuo kimojawapo hapa nchini alikuwa na tabia hizo, alikuwa neighbour na sista mmoja lecturer mlliosoma political science mnamjua! i used to go there na dad coz dad ni lecturer engineering til todate, sasa yule lecturer alimwambia sista amuombee sana, coz hajui kama anataka kuwa mwanaume zaidi, au mwanamke zaidi, coz anavyo viwili na vyote active vibaya mno, especialy cha kiume! alikuwa hapendi kutoka wala kujichanganya, hebu ongea na mpwao vizuri, au mkeo aseme naye, ukute ana tatizo hili!
 
Jamani niko tayari tena mbegu zangu n safi kabisa nitapima hata mafua m huwaga sibahatishi mara 1tu nacheka na nyavu.
 
Naona anajiweka katika kona ya hatari sana.
Hata hivyo mpe habari za jf, ajiunge, mwambie habari za love connect, apost kule atapata tu!
 
Mkuu over 40 years aendelee kusubiri tu!

hapo nilipo-bold am worried kama hajagonga kitu ya meno-pause ambako hata mayai hayazalishwi tena...na kwa nchi kama hii yangu ya tz ni kaaaazi kwelikweli kupata wataalamu wa kumzalisha kwa maabara...uliulizia IFV CLINIC???..yap ipo moja tuu tanzania pale opposite na jengo la clouds mitaa ya mikocheni mlalakuwa njia ya kwenda coca cola wameweka kibao mlangoni na namba zao za simu....

mie naweza kumpa mbegu ila lazma nimuone na nijue hatimiliki za mwanetu na mie pia inakuwaje maana ndio nitakuwa biological poor-dady...ahahahaha...OVER 40...bado analipa kweli???..weka picha yake PM kwangu watu wajilipuwe vizuri.,
 
Back
Top Bottom