Mpwa wangu anatafuta mume wa kuzaa naye!

Tegelezeni

JF-Expert Member
Dec 31, 2009
268
124
Ni mtoto wa kaka yangu, na amezaliwa na kukulia Dar, mimi sikuwa karibu naye na ni msiri sana. Nimekuwa nikizungumza naye mara kwa mara lakini sio muwazi na hiyo ilitokana na yeye kujiwekea mipaka.

Amesoma hapa nchini na nje ya nchi katika moja ya nchi za Scandinavia na sasa ni mwajiriwa serikalini. Sina uhakika sana umri wake lakini naamini ana zaidi ya miaka 40. Hivi karibuni nilishikwa na udadisi na katika mazungumzo na shemeji yangu,(mama yake) alinijulisha kwamba hata yeye na kaka yangu wanashangaa binti yao kutoolewa au hata kupata mtoto. Anakiri kwamba hawajawahi kumuona na mwanaume na hana mashoga wanaofika hapo nyumbani.

Nilimdadisi iwapo waliwahi kumuuliza kuhusu kuolewa, shemeji akanijibu kwamba waliwahi kumuuliza na akajibu kwa kifupi kwamba hajapata mume na kipata atawajulisha. Lakini tangu siku hiyo akawa hana raha na akawaambia wadogo zake kwamba wazazi wamememchoka na sasa wanamnyanyasa. (anao wadogo zake wawili wa kike ambao wameshaolewa na kuzaa)

Nilitoa wazo kwamba wamshauri japo apate mtoto, ushauri ambao aliukubali kwa mikono miwili, lakini ni nani wa kuzaa naye?

Nimeshauri hatua ya kwanza ahame hapo nyumbani akapange mbali na nyumbani ili awe huru na hapo atakuwa na fursa ya kupata mwanaume japo wa kuzaa naye. Amekubali na sasa anatafuta nyumba ya kupanga.

Lakini yuko worried kama atapata mwanaume mwaminifu ambaye sio mume wa mtu japo wa kuzaa naye tu basi. Ila swali lake aliuliza iwapo hapa nchini kuna uwezekano wa kufanyiwa IFV badala ya njia ya kujamiiana. Hilo sina uhakika nalo na ndio maana nimekuja hapa kutafuta ushauri..
King'asti , BADILI TABIA , gfsonwin , Yummy , nyumba kubwa , Nehondo , MwanajamiiOne , marrykate , AshaDii , NATA , FirstLady1 , TaiJike , na wengineo ambao sijawataja, naomba msaada wenu ili nimsaidie mpwa wangu
 
Last edited by a moderator:
{kwamba wazazi wamemchoka na sasa wanamnyanyasa} msemo uhu wadada weng aged ambao awajaolewa wanaupenda sana sorry 4her bt azd subri bahati yake
 
{kwamba wazazi wamemchoka na sasa wanamnyanyasa} msemo uhu wadada weng aged ambao awajaolewa wanaupenda sana sorry 4her bt azd subri bahati yake

Huyu mwanamama aliye na zaidi ya miaka 40, aliyesoma mpaka nje kwenye nchi za Scandinavia bado anakaa na wazazi? Au "wazazi wamemchoka" kwa maana ya kumchoka kusema suala la ndoa?
 
Ohhh!..hivyo anatafuta sperms donors enhh?....Ok,nenda kamuulize tena anataka mbegu za aina gani? then kuja hapa tena kwa maelekezo zaidi......nahisi naweza kupata deal la kutoka mitaa hii.
 
Huyu mwanamama aliye na zaidi ya miaka 40, aliyesoma mpaka nje kwenye nchi za Scandinavia bado anakaa na wazazi? Au "wazazi wamemchoka" kwa maana ya kumchoka kusema suala la ndoa?
Yeah ni kama bado anakaa na wazazi kwani kuna anaishi kwenye apartment ambayo iko in the same compound na anawasaidia wazazi kazi za nyumbani kwa kuwa wako aged

Mimi simuelewi lakini anaonekana kutokuwa na ukaribu na wanaume, hata mimi ilinichukuwa muda sana kumzoea, in fact nimejuana naye ukubwani, mimi nimekulia mikoani na ninakuja DAR kikazi na huwa nafikia kwa wazazi wake.
 
Mi niko tayari kama issue ni mtoto tu, hata akitaka wawili.
Ila mambo ya kuoana ntakua namdanganya kwa kweli!!
sawa lakini kwa njia gani, ya kujamiiana au ya IVF?
Je uko tayari kupima? (UKIMWI)
Je una umri gani?
Niko serious mkuu
 
binafsi kwa hapa kwetu iyo njia sina halkika sana nayo(ivf). lakin dada huyo mpwao huwa ni mtu wa kaujichanganya? huwa anatoka toka out,au hata yuko katika hii mitandao ya kijamii? mwambie hivi aingie humu jf halafu atulize kichwa chake kwenye kuchangia nakuhakikishia atavuna wachumba balaa tena wa umri wake nakuhakikishia.
 
Ohhh!..hivyo anatafuta sperms donors enhh?....Ok,nenda kamuulize tena anataka mbegu za aina gani? then kuja hapa tena kwa maelekezo zaidi......nahisi naweza kupata deal la kutoka mitaa hii.
Mkuu mbegu ya aina yoyote, anachohitaji ni mtoto
 
Yeah ni kama bado anakaa na wazazi kwani kuna anaishi kwenye apartment ambayo iko in the same compound na anawasaidia wazazi kazi za nyumbani kwa kuwa wako aged

Mimi simuelewi lakini anaonekana kutokuwa na ukaribu na wanaume, hata mimi ilinichukuwa muda sana kumzoea, in fact nimejuana naye ukubwani, mimi nimekulia mikoani na ninakuja DAR kikazi na huwa nafikia kwa wazazi wake.

Kwani ni lazima kila mwanamke kuwa na ukaribu na wanaume? Wengine wito wao ulikuwa utawa ila wamekosea njia tu, wengine wana upungufu na homoni za kutaka kuwa na wanaume, wengine wametendwa siku nyingi hawataki hata mwanamme, wengine wasagaji wanataka wanawake wenzao.

Mwacheni aishi maisha yake.

Mkimletea bugudha ataoa kwa ajili ya pressure mwioshowe atawaletea bwana mapepe mtamshangaa tena hapa kaona nini huyu? Kumbe makosa yenu kumshurutisha.

Kashakaa na wazungu wa Scandinavia huyu, anajua hata akiamua kukaa na mbwa wake tu poa, kuna watu wanaishi hivyo.

Kumtaka mtu mwingine aishi kama unavyoona wewe maisha yanavyotakiwa ni kutaka mtu aishi kitumwa.

Usikute hata hizo habari za IVF anakubali kwa sababu ya pressure, kesho keshokutwa mtoto atakua kuulizia baba, mama atasema mie sikutaka hata kuwa na mtoto, ndugu zangu ndio walionipa pressure.
 
binafsi kwa hapa kwetu iyo njia sina halkika sana nayo(ivf). lakin dada huyo mpwao huwa ni mtu wa kaujichanganya? huwa anatoka toka out,au hata yuko katika hii mitandao ya kijamii? mwambie hivi aingie humu jf halafu atulize kichwa chake kwenye kuchangia nakuhakikishia atavuna wachumba balaa tena wa umri wake nakuhakikishia.
Sio mtu wa kujichanganya kabisa, yaani sijui ni malezi, maana wazazi wake ni watu wa dini na wamewalea watoto wao kwa maadili ya hali ya juu sana. Kuna siku nilimuomba tutoke out, duh! alipinga sana na toka siku hiyo akawa hapendi kuongea na mimi kama zamani. mama yake kanishauri nimsaidie na nilimshauri ajiunge na JF akasema hana muda ila anapenda sana kusomamagazeti ya nje maana hata mimi namletea magazeti kama Hello, Woman Weekly, OK nk
 
Kwani ni lazima kila mwanamke kuwa na ukaribu na wanaume? Wengine wito wao ulikuwa utawa ila wamekosea njia tu, wengine wana upungufu na homoni za kutaka kuwa na wanaume, wengine wametendwa siku nyingi hawataki hata mwanamme, wengine wasagaji wanataka wanawake wenzao.

Mwacheni aishi maisha yake.

Mkimletea bugudha ataoa kwa ajili ya pressure mwioshowe atawaletea bwana mapepe mtamshangaa tena hapa kaona nini huyu? Kumbe makosa yenu kumshurutisha.

Kashakaa na wazungu wa Scandinavia huyu, anajua hata akiamua kukaa na mbwa wake tu poa, kuna watu wanaishi hivyo.

Kumtaka mtu mwingine aishi kama unavyoona wewe maisha yanavyotakiwa ni kutaka mtu aishi kitumwa.

Usikute hata hizo habari za IVF anakubali kwa sababu ya pressure, kesho keshokutwa mtoto atakua kuulizia baba, mama atasema mie sikutaka hata kuwa na mtoto, ndugu zangu ndio walionipa pressure.
Mkuu hata yeye ameonekana kuridhia wazo la kupata mtoto, na mwezi uliopita nilikuja nDAR kikazi na mke wangu na alizungumza naye kwam kirefu akamweleza kwamba anapenda sana apete mtoto lakini wanaume wanamuogopa, sijui kwa sababu ya umri!
 
mwambie hivi aingie humu jf halafu atulize kichwa chake kwenye kuchangia nakuhakikishia atavuna wachumba balaa tena wa umri wake nakuhakikishia.
mhh wakubwa wanafahdi umeongea kwa kujiamin mbona awa ninaohc ni age yangu waliopo umu watukutu sana kama smile utazanan k yake imeng'olewa bana
 
Ok!..yupo tayari kuchukua hizo mbegu kwa njia gani?....I mean ile ya Sperms to Eggs kupitia baiolojia zetu au Sperms to eggs kupitia In Vitro Fertilization....ya kwanza we can walk the talk kama tutaridhiana maana lazima tuonane,ya pili cna haja ya kumuona ataje offer yake then its a deal.
 
hajawahi hata kuwa na b/f katika maisha yake? huyo atakuwa ni freak, na probably hata kitobo utelezi hana..
 
Ok!..yupo tayari kuchukua hizo mbegu kwa njia gani?....I mean ile ya Sperms to Eggs kupitia baiolojia zetu au Sperms to eggs kupitia In Vitro Fertilization....ya kwanza we can walk the talk kama tutaridhiana maana lazima tuonane,ya pili cna haja ya kumuona ataje offer yake then its a deal.
hana hela bana mbona unafanya biashara sasa....... hata hiyo ya njia za asili yukom pouwa lakini kupima ukimwi ni lazima
 
Back
Top Bottom