Mpunga wote umenyauka

Mpunga wote umenyauka

Na Serikali haijaleta ukame wala jua
Ila mimi nalia na hawa mabwana shamba na TMA...wako wapi?.

Jamaa yangu Arusha alihadaika na ile mvua akakimbilia kupanda mahindi...saa hizi yamechomoza yanasubiri wakati ukiwadia yafe...maana jua linawaka....kama angepata taarifa kuwa zile mvua sio za kutumaini asingepoteza nguvu zake bure.
 
Hali mbaya sana kila kona ya nchi.

Pamoja na yote lakini hii ni shule inabidi tujifunze kilimo na ufugaji wa kisasa wa kutokutegeme mvua.

Lakini hii ni kwa sisi tunao jua dunia inaendaje.

Poleni sana kwa hayo yote Mungu awape wepesi.
 
Baada ya kufika shambani nimehuzunika sana, mpunga niliopandikiza umenyauka. Ukame huu twafa!
Wanasema msiba wa wengi harusi. Lakini kwa hili sio kweli. Nyanya zangu zimekauka zote. Hapa nilipo nasubiri kitunguu na namwomba Mungu kisikutane na mvua.
 
acha uchonganishi, kuna ukijani kila kona ya nchi hata mtukufu Rais alisema
 
Uko serious mkuu

Morogoro vijijini wafugaji wana ondolewa Na polisi kuepusha mfarakano Na wakulima Kwahiyo Ng'ombe wanakamatwa wakionekana Na ukipeleka Ng'ombe Au kutoa taarifa za mfufaji ambaye bado hajaondoka unalipwa. Kwahiyo wafugaji wameamua kuwauzia Ng'ombe Kwa bei rahisi Na hata wale walio kamatwa Na polisi wanauzwa Kwa bei sawa Na bure. Ila wengi Hawana afya
 
  • Thanks
Reactions: etb
aisee hali ni mbaya inabidi kumwomba Mungu alete mvua maana mazao yanakauka hali imekuwa si hali
 
Pole sana mkuu lakini kwa sasa mvua zimeanza kunyesha tena katika maeneo mengi ya nchi
 
Back
Top Bottom