MPs warned over documents

???
Sasa ndugu usipoweka hata kamstari kamoja kuelezea yanayojiri utakuwa umetuhabarisha?
Lazaro yupi? Anaumbuliwa nini?
 
Anasema sio sawa kuleek nyaraka za serikali kma za EPA,etc.

Anarudia zile hadithi za pesa za EPA zilizorudi zimetumika kuwainua wakulima, Slaa kakosea angambana hapo. Ila TPC nao transmission yao ovyo, mjadala hauko free flowing.
 
TBC wanachemsha wanamkatisha Lazaro, live transmission hawajazoea.
 
Duh...kaaaazi kweli kweli!!Mbona habari haijitoshelezi.Hata kufanya gap-filling inakuwa ngumu,naamini watakaokuwa wameshuhudia mahojiano hayo watakuja na more info ili pawe na fair and sober discussion.
 
"Kuna watu wa aina mbili duniani, kuna watu ambao hata mungu akishuka duniani akaleta mabadiliko wao watalaumu" -lazaro

"Kuna correction nyingi za standard of living kati ya mkulima na mfanyabiashara wa mjini, kama kodi, ndo maana tumefuta KODI YA KICHWA, kitu ambacho wapinzani hawakutaka." -lazaro

Slaa anacheka.
 
"hata mkichukua mishahara yote ya wabunge ukawapa askari haitaleta mabadiliko"

Oya! Nazitype hizi ninayozisikia! So of coz kutakua kuna tofauti, lakini ni yale yale!
 
TBC1 wana matatizo makubwa. Kwa muda sasa binafsi napata shida kuwapata hewani. Kwa hili suala la kukutanisha wabunge wa CCM na wale wa upinzani wakati mwingine huwa linaonesha jinsi tulivyo matatizo makubwa hasa kwa wabunge wa CCM, kujifanya wao ni sehemu ya serikali badala ya watetezi wa wananchi. Baadhi ya wabunge wa CCM hawana uwezo wa kuongea wazi baadhi ya vitu ambavyo wanavijua na vina maslahi kwa umma. Na ndio maana siku moja Selukamba alionekana kituko kwenye TV. Laiti kama wananchi wangekuwa na uwezo wa kuwaadhibu, huu ujinga wa kutetea kila jambo ungefikia ukomo.
 
Lazaro anatafuta chep publicity.....hana lolote arudishe pesa zetu za summer camp.
 
Lazaro anatafuta chep publicity.....hana lolote arudishe pesa zetu za summer camp.
Nimefanikiwa kupata kujua alichoongea Lazaro...

Kimsingi walitoka nje ya mada. Mada yenyewe ilikuwa inaongelea vinasaba vya DNA lakini wakajikuta wanafikia huko kwenye issue ya mishahara ya wabunge, suala la nyaraka za serikali etc.

Ninachoweza kusema ni hivi: Lazaro alivyoongea alionekana anaongea kwa dharau sana as if anawa-under estimate watanzania wanaoangalia. Halafu alionekana kuwa mtu wa kuamini upinzani ni sawa na u-mbumbumbu.

Binafsi nafurahishwa na uwepo wa upinzani na najua hilo tunaweza kutofautiana na Lazaro. Madai kuwa wapinzani wanakumbatia issue ya EPA na BoT kuwa yao na kudai ni ya CCM naona ni kuendekeza siasa badala ya kuangalia maslahi ya taifa.

Endapo wapinzani ni kweli wanakumbatia mambo haya na kudai ni yao basi nao watakuwa wameishiwa, kinachotakiwa katika suala hili ni kukubaliana kuwa tumefanikiwa kuwajua wabaya wetu ingawa wengine wameendelea kubebwa 'live'. Ukweli ni kwamba iwe ni CAG, CCM au Upinzani ndio uliibua issues hizi bado inabakia kuwa zile zilihesabika kuwa nyaraka za serikali na haikuwa rahisi nyaraka hizo kuwekwa hadharani na uwezekano wa reports hizo kufanyiwa kazi ulikuwa mdogo! Alichoongea Dr. Slaa katika hili yuko sahihi, waliofichua uozo huu wanastahili kupongezwa badala ya kuwabana au kuanza kutafuta sheria za kuwabana kuhakikisha wanaharibiwa maisha!

Suala la mishahara ya wabunge naona Lazaro bado alikuwa katika kitu kilekile ninachopingana nacho, kudai kuwa Dr. Slaa anatafuta umaarufu kwa kuwachochea wananchi bure.

Alichoongea Lazaro kuwa ndiyo mipango ya serikali katika kuwaokoa watanzania ni hadithi za siku nyingi ambazo bila kelele za watu kama Dr. Slaa and the like tutaendelea kuzisikia hadithi hizo.

Nasikitika kuwa Dr. Slaa huenda alielemewa maana inaelekea hata watangazaji wenyewe wako biased sana.

Tumeandika humu, yameandikwa magazetini na kwingine kwingi... Tanzania imezidi kuwa na matabaka, tuchukieni kwa kusema hivi lakini hatuwezi kuukwepa ukweli huu. Alichokisema Dr. Slaa kina ukweli mkubwa ingawa kama alivyoonekana kutahadharisha Lazaro inawezekana kabisa mtu kutumia kauli kama hizo kuufanya umma uione serikali kuwa haiufikirii na hivyo jamii ya chini kuamua kufanya kitu ambacho kinaweza kupelekea serikali iliyo madarakani kupoteza fursa hiyo!

Ukweli unabakia palepale kuwa Dr. Slaa na Lazaro wanaishi katika Jamii ambayo ina matumizi sawa na wao... Vyakula mnavyokula ni vya aina moja tu japo manjonjo ya makaangizo yanaweza kuwatofautisha, barabara mnazotumia ni zilezile, mafuta kwenye magari mnaweka sawa na raia wa kawaida, hata vituo vya televisheni mnavyoangalia ni vilevile! Haina sababu ya kuendelea kuangalia hii hali ikiendelea, kelele zitapigwa, iwe zinaonekana za vyura ama za wenye uchu wa madaraka lakini hazitaisha katika hili. Mtanzania anateseka sana ndani ya nchi yake!

Katika suala la nyaraka napenda kumfahamisha Lazaro kuwa sisi watanzania tuna mapenzi na taifa letu! Tunalipenda kiasi ambacho hatuko tayari kuona linaaibishwa kwa namna yoyote ile. Namhakikishia hata akiitembelea JF (au kama ni member) anaweza kuthibitisha kuwa mara zote tunawapa tahadhari juu ya mambo ambayo yanaelekea yanahatarisha usalama wa taifa letu. Nawashukuru policy makers wa Tanzania ambao walionelea ni vema wakimtambulisha mtu wao hapa JF na kuwa anatufahamisha pale anapoona kuna sehemu inalivua nguo taifa tukachukua hatua, hawa wanaangalia taifa na si chama!

Lazaro, unaweza kuwa sahihi katika mengi lakini katika mengi pia hauko sahihi!

Invisible
 
Nampongeza Mwiba kwa uchambuzi wake mzuri. Ninapenda tuingie kwa ndani zaidi tujiulize kwanini huyo mheshimiwa akaamua kumuuliza huyo waziri hilo swali at this particular moment? Why not last year? Naona jibu ni kuwa muonja asali haonji mara moja. Lazima atarudia tu. Wale mafisadi hawajakubali mambo yaishie hapo. Sasa wanawatumia hawa wabunge(njaa?) ili kutafuta namna ya serikali kutumia sheria kandamizi kuziba kwa namna yeyote ufisadi wao usifichuliwe. Dont be carried away by there present silence. They are silently planning there come back. They will stop at nothing to achieve this. Ndiyo maana wanawatumia vibaraka wao kuanza kusafisha njia. They should have been put under lock but this was not done. Mjomba, inauma sana! Anyway, that is the hole we are in and we happen to be silent while it was being dug. How do we get out? That is the crucial question we are facing now. Let us face it head on and find way out. ANY SUGESTION? Tusione ajabu tukasikia mengine bungeni ya aina hiyo.
 
"hata mkichukua mishahara yote ya wabunge ukawapa askari haitaleta mabadiliko"

Oya! Nazitype hizi ninayozisikia! So of coz kutakua kuna tofauti, lakini ni yale yale!


Inamaana (minority) wachache waneemeke while majority tunaumia sio? issue sio askari walipwe vizuri ila ni mgawanyiko mzuri wa mapato yetu as country, why on earth tunainvest na kuempower politics? haitusaidii kitu. Serious hata huyo Nyarandu nduguze wanateseka huko Singida while yeye anakula good time, hatutaki watulishe na wake zetu bali they have to make sure tukiumwa hatuishii kwa waganga wa jadi, hospitals ziwe na madawa na madaktari, shule walimu na vitabu, mabarabara mazuri those are our rights sio favour.

Ngoja niishie hapo nisije nikaanza kulaani bure. Mungu anisamehe!
 
huo mdahalo wa muda mfupi hata mie nimeuona...kwa kweli kwa wabunge aina ya kina lazaro tanzania inahitaji takribani karne kama tano kupiga hatua moja tu ya maendeleo..na hasa ya kidemokrasia. kijana Lazaro nahisi hata kijijini kwao na kwa wapiga kura wake hajui wanaishije...masikini wa kutupwa...anatetea maslahi wanayopata wabunge wetu in-comparison na wabunge wa nchi nyingine duniani...anashau pia kuwa slaa anachosema ni sahihi kuwa hili gap la kipato cha mbunge na mwanachi mwingine ni baya na halifai kwavile hata nyanya na mchele tunanunua soko moja la tandale au hata hapo kariakoo...haiwezekani mbunge kwa mwaka afunge karibu tshs 7m wakati mwalimu/askari/daktari hawafungi hata laki 5 kwa mwezi. Kijana Lazaro anasema kuwa hata mabilioni ya wabunge yakipelekwa kwa wananchi hayana impact yoyote wataendelea kuwa masikini...ok and very fine...kwanini yasipelekwe ili watanzania wote including wabunge tu-share kwa pamoja sifa yetu kuu duniani ya kuishi chini ya 1usd??LAZARO ...wadau nahisi amejisahau..kama nimekosea..huyu jamaa si ndio mme wa ki-miss flan hapa nchini???.....wataalamu wa saikolojia naomba tumchunguze mbunge lazaro kisaikolojia zaidi....KWA KWELI NIMEJISIKIA VIBAYA SANA KUONA BWANA MDOGO LAZARO ANAPINGA HOJA NZITO ZA MZEE SLAA KWA MAJIBU YA KITOTO-TOTO TUUU. Hajengi hoja za msingi achilia mbali kulinda maslahi ya wabunge -wezi badala ya kutetea maslahi ya WANACHI MASIKINI WA TANZANIA.....mungu ibariki TANZANIA YA NYERERE
 
Back
Top Bottom