MPs warned over documents | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MPs warned over documents

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 21, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,429
  Trophy Points: 280
  MPs warned over documents

  LEONARD MWAKALEBELA in Dodoma, 21st April 2009 @ 11:53,

  DAILY NEWS

  The government has warned Members of Parliament that their privileges and immunities that go with their offices do not cover them against holding classified government documents. Minister in the President’s Office, Public Service Management, Mrs Hawa Ghasia said that using such documents for political motives was inherently unlawful, and that anyone holding such documents was liable to prosecution – because there is no immunity for such MPs.

  She was responding to supplementary questions by Mr Siraju Juma Kaboyonga (Tabora Urban-CCM) and Ms Rosemary Kasimbi Kirigini (Special Seats-CCM). Mr Kaboyonga wanted to know if privileges and powers enjoyed by MPs also gave them immunity against prosecution for possessing government classified documents.

  On her part, Ms Kirigini wanted to know what measures had been taken against some MPs who were allegedly in possession of the documents and using them to pursue political interests. The minister said the government knew that some MPs had these papers in their possession for political reasons – but warned that the law would soon take its course against them.

  She added that her office had since ‘discovered’ that some MPs were forking out huge sums of money to get such documents. “We’re investigating to establish (both) their sources and the motives behind,” the minister said. Answering the basic question raised by Kheri Khatib Ameir (Matemwe-CCM), Mrs Ghasia admitted that many classified documents had fallen into unauthorized hands recently – mostly individuals seeking political capital. “This situation cannot be ignored … it must be addressed thoroughly in order to contain the abuse of such documents.

  Possession of such documents is liable to criminal prosecution according to the laws of the land,” the minister insisted. She cited the relevant laws against possession of classified documents by individuals as the National Security Act no. 3 of 1970, National Archives and Records Act no. 3 of 2002, Public Service Act no. 8 of 2002 and Standing Regulations of the public service. “These laws stipulate division of responsibilities among state organs and give powers to arrest and prosecute suspected thieves of the classified documents,” Mrs Ghasia explained.

  She said her office would work with other state organs in investigating the spate of leakages. Mr Ameir had asked for details of the people so far arrested for the crime during the past one year -- and what disciplinary and legal measures had been taken against them.

  He also wanted to know what efforts the government was making to contain leakage of its sensitive documents, describing the leakages as a ‘threat to national security.’ However, Mrs Ghasia said no such arrests had been made so far – but only acknowledged that ‘some suspects’ had been removed from their offices -- or transferred to others. The minister also cautioned the general public against abuse of such documents following increased use of information and communication technology (ICT).
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Vitisho hivyo vinapenyezwa na Sultani CCM akiwatumia wafuasi wake watiifu ,sasa sijui ni doc zipi ambazo zitakuwa classified ,ni hizi wanazogawa akina Slaa na wenziwe au kuna zingine ,zinazoonekana hapa JF zikiwa na mihuri ya siri au serikali.

  Ila huku ni kuumbuka maana nyaraka zote zinaoonekana si za mambo mema ni mambo maovu tu ambayo yanaonyesha wizi ndani ya Serikali ya Sultani CCM ,kwa nilivyofahamu kwa wanavyotaka wao mambo haya yawe ni siri kubwa ili wazidi kuficha na kuwaficha wananchi kwa yale yanayotokea nyuma ya maneno yao matamu wawapo mikutanoni na kuwalaghai wananchi watafanya hiki na kutekeleza kile kumbe ni kingi wanachokwiba kuliko wanachotumia.

  Kwa dunia ya leo kila uovu utadhihirika tu kwani si waote waliomo ndani ya utawala wa CCM wanaridhika na jinsi nchi inavyooendeshwa kienyeji ,wanaofaidika ni wachache na sio madhumuni ya kudai uhuru kuwa faida ipatikane kwa wachache tu na wengine waendelee kuwa watumwa chini ya Chama Tawala hilo halikubaliki na lina mwisho wake.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,429
  Trophy Points: 280
  Hapa wanayemtarget ili kuendelea kuficha udhalimu na ufisadi uliokithiri ndani ya serikali ni shujaa wetu Watanzania na huyo si mwingine bali ni Dr W. Slaa. Naona sasa wanataka kuvuka mpaka ili kuhakikisha maovu yao yanaendelea kubaki siri nzito. Watanzania inabidi tupinge hili kwa nguvu zetu zote, vinginevyo ufisadi ndiyo utazidi kushamiri. Kwa maoni yangu Dr Slaa si mtu wa kufunguliwa mashataka kwa maovu mbali mbali mbali aliyoyaanika kadharani bali ni wa kupongezwa na umma wote wa Watanzania wanaopenda maendeleo ya nchi yetu.
   
 4. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Umesema vyema Mwiba, classified document inapokuwa ni nyaraka ya wizi wa mali ya umma, haina hadhi ya kuwa confidential.Kwa mtaji huo neno hilo linaweza kutumika vibaya, labda watunge sheria ya kuwabana wanaofichua siri za serikali kuboronga. So far hakuna document nzuri ambayo ni confidential imetoka hadharani, nadhani jukumu lao la kwanza ni kuacha kutumia sheria ya confidential kulinda ufisadi wao.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa watu wanaumwa?
   
 6. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Haswaaa!!! Nadhani tukawapime akili kwanza kabla ya kutafuta ugonjwa mwingine!
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nadhani wamepagawa akili.
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Bila shaka hawatapata kigugumizi katika kutaja hizo wanazoita nyaraka za siri. Utamu utakuja pale tutakapoweza kuwaweka kiti moto waweze kutueleza kwa nini waraka wa kiufisadi uliitwa wa siri. Hapo pia tutaweza kupata tafsiri nzuri tu ya kisheria kuhusu kinachofaa kuitwa hivyo na kwa manufaa ya nani na wajibu wa mzalendo ambaye anajikuta uso kwa uso na waraka huo afanye nini.
   
 9. 911

  911 Platinum Member

  #9
  Apr 21, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Yaani hawa wauliza maswali+waziri anayejibu wote ni vioja tu.Muda mwingine huwa najiuliza kuwa hivi Bunge linatutendea 'haki' wananchi,hasa kama mambo wanayokaa kujadili ndio haya ya kuhalalisha ukwapuaji kwa mgongo wa 'CLASSIFIED Docs'??Mhimili huu una tatizo kubwa kuliko ni/tunavyofikiri.Poor MPs,shame on you.
   
 10. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NDIO MAANA NASEMA HAKUNA KUTOKA CCM ANAEFAA KUTUONGOZA Kama lazima CCM basi na amalize muda wake huyo aliopo. Hivyo mijibaba mizima inakaa kwenye Bunge na kuanza kumfisadi mtu anaetetea maslahi ya Taifa. Haya yote yanakuja baada ya DR Slaa kuanika wazi Wabunge wanavyotunyonya. Wanafikiri akikamatwa ndio watamuweza kwani kwa uchaguzi hawamuwezi.
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Ndivyo tulivyo!

  Wakumbushe wasisahau kuwashitaki Google kwa kuwa na picha za kila kona ya kunakoitwa "Restricted".

  Dawa ya matatizo haya ni kuwa msafi, kwisha khabari yake!
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,429
  Trophy Points: 280
  Inabidi watupe definition ya hizo nyaraka za siri. Je, muhusika kama akianika nyaraka za siri hadharani ili kutetea maslahi ya Watanzania bado huyo muhusika atafunguliwa kesi ambayo kwa maoni yangu itakuwa ni kupoteza pesa za walipa kodi na muda pia katika kumshtaki yule ambaye hastahili kushtakiwa.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Whaat?..

  Jamani hivi hawa viongozi wetu wazima kweli?

  Hivi hawa ni wasomi kweli au wanatumia Siasa pia kufikia maamuzi ya aina hii..
  Hizi Documents haziwezi kuwa Government classified ikiwa zinahusiana na UFISADI..
  Hivi hawafahamu yaliyomkuta Nixon na Watergate? hawakumbuki Yalimkuta Carter na Iran Contra..

  Haiwezekani hata siku moja nyaraka zinazovunja sheria (someone's madudu) kuwa government classifed document...kisha mtu azipeleke Bungeni mahala ambapo sheria za ammendiments za sheria zetu hufanyika..

  Kisha huwezi kusema zinatumika kwa Political motives ikiwa viongozi wanaopingana na matumizi mabaya ya wadhifa yanatoka vyama vyote vilivyopo Bungeni isipokuwa nyaraka hizi humlenga mtu mmoja au kundi la watu wahisika.. Itakuwaje swala la Richmond liwe Politcal motivated - EPA, Rada, Kagoda na kadhalika yawe Political wakati kuna wabunge wa CCM na baadhi Mawaziri wa serikali hawafahamu kilichotokea hata nyaraka hizo zikapita kufunga mikataba mibaya kwa taifa letu.

  Hivi kweli mipango ya UFISADI baina na viongozi kwa usiri wao inaweza kuitwa Government Classified Documents?
   
 14. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #14
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Umeshtuka sana naona, utakuwa una nyaraka za serikali si bure!
   
 15. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #15
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Iko hivi,

  BoT (EPA, Twin Tower etc) scandals zimetokana na ku-leak kwa nyaraka za siri za serikali.

  Changa la macho la Richmond a.k.a Dowans limebumbuluka kutokana na nyaraka kadhaa za serikali.

  DECI nayo itabumbuluka soon endapo nyaraka za serikali walizo nazo watu flani wakiziweka bayana hivyo kupelekea machafuko (kwa madai yao) kwa taifa.

  Radar, Buzwagi and the like vimetokana na nyaraka za serikali kuanikwa!

  Huu ni wakati mbaya kwa taifa! Wanaoanika nyaraka hizi au kutembea nazo wamesababisha aibu kubwa kwa taifa, tunalazimika kuonekana kama tunashitaki watu na kujikuta tukiwa katika wakati mgumu mbele ya mataifa rafiki. Hali si nzuri kabisa! Wanatakiwa kukamatwa ama kumalizwa taratibu watu hawa (watakapofahamika). Hatuwezi kuwaacha hivi hivi.

  Pata ujumbe
   
 16. A

  August JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Je inamanisha Kikwete, Pinda na Serikali ya CCM wameunga Mkono waraka huu Au ni Maneno ya waziri husika Pekee yake, maana siamini kama CCM wote ni wajinga kama huyu waziri husika.
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  August,
  Mkuu maneno hayo yaliyotangulia ujumbe wote ni maneno (vitisho) ambayo yanatakiwa kuchukuliwa kuwa yanatoka - Serikali ya Kikwete na Pinda...
  Unapotumia neno The government has warned MP's hapa mkuu wangu ndipo unajua kwamba sasa tumefika mahala pabaya sana..
  Na kama kweli aliyosema Invinsible ndio hoja yao kubwa basi wametumia mbinu mbaya sana kuliko zote na naomba Mungu kesho waanze zoezi hilo kwa sababu ukisikia mtu anapata sifa za Kisiasa basi ni kutokana na reactions kama hizi..
  Kumbuka tu kwamba Karamagi amepoteza Uwaziri na sifa zake kutokana na Buzwagi na kwa bahati mbaya au nzuri, sifa alozipata Zitto ni kutokana na Bunge kumfungia (reaction) na swala la Buzwagi kuwa heading ya mazungumzo yote mitaani. hakuna mwananchji aliyejali tena hizo nyaraka wala kufahamu kilichoandikwa isipokuwa utovu wa sheria na usiri uliopo ndicho kilichowafumbua wananchi macho!
  Leo hii Karamagi yupo wapi nasikia hata mkewe Mrusi kamwacha mataani!.Zitto sii mwenzake tena na pengine ni mmoja kati ya Wabunge wachache waheshimiwa..
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,429
  Trophy Points: 280
  Serikali yapiga mkwara mabomu ya Dkt. Slaa
  Tuesday, 21 April 2009 17:00

  .Mwenyewe aahidi kuendeleza vita
  .Hatua hiyo ni kulinda ufisadi

  Na John Daniel, Dodoma

  Majira

  KATIKA hali inayoonesha kuchoshwa na tuhuma nzito dhidi yake zinazoibuliwa na baadhi ya wabunge wakiwa na ushahidi wa nyaraka muhimu za kiutendaji, Serikali imetoa onyo kwao kuacha mara moja kuiba nyaraka hizo vinginevyo wataangukiwa na mkono wa sheria.

  Hatua hiyo inayotafsiriwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa ni Serikali kujihami na kutaka kuwaziba midomo wabunge machachari wanaokesha kusaka nyaraka hizo huku kukiwa na mgawanyiko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu jinsi ya kuwashughulikia mafisadi.

  Akitoa onyo hilo Bungeni jana, Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Hawa Ghasia alisema licha ya Serikali kuwatambua wanaoiba nyaraka hizo imekuwa ikiwaacha kwa madai walikuwa wakijitafutia umaarufu wa kisiasa na tuhuma wanazotoa hazina madhara makubwa lakini si halali kufanya hivyo.

  Bi. Ghasia aliyekuwa amebanwa na Wabunge watatu wa CCM; Bw. Kheri Ameir (Matemwe), Bw. Siraju Kaboyonga (Tabora Mjini) na Bi. Rosemary Kirigini (Viti Maalum), alisema wanaohusika na wizi wa nyaraka hizo wamo bungeni na sasa wamesikia onyo, hivyo wakome kufanya hivyo.

  "Sheria iliyopo ya kinga ya mbunge haimkingi kuiba nyaraka za Serikali. Hatukuwakamata wabunge hao kwa kuwa wanajitafutia umaarufu wa kisiasa," alisema Bi. Ghasia wakati akijibu swali la nyongeza la Bw. Kaboyonga aliyetaka kujua kinga ya Mbunge akiiba nyaraka za Serikali.

  Bi. Ghasia alisema: "Mheshimiwa Spika tunawataka wabunge hao wasiendelee, wakiendelea tutawakamata kwa kuwa wamo humu na wanatusikia, wakiendelea sheria itachukua mkondo wake."

  Kuhusu swali la msingi la Bw. Ameir iliyetaka Serikali kueleza ni watu wangapi wamekamatwa kuhusika na tuhuma za kuiba au kutoa nyaraka hizo kati ya Januari na Desemba mwaka jana, hatua zilizochukuliwa dhidi yao na jitihada zinazofanywa kukomesha tabia hiyo.

  Bi. Ghasia alisema tayari Serikali ina majina ya watumishi kadhaa wanaodaiwa kuhusika katika tuhuma hizo lakini hakuna aliyekamatwa rasmi kwa kuwa uchunguzi wa kina unafanyika ili kupata ushahidi.

  Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa namba tatu ya mwaka 1970 na Sheria ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa namba tatu ya mwaka 2002 na Sheria ya Utumishi wa Umma namba nane ya mwaka 2002 na kanuni za kudumu katika Utumishi wa Umma toleo la mwaka 1994 ni kosa la jinai kuwa na nyaraka za Serikali.

  Hata hivyo Wabunge ambao wameonekana kuwa vinara katika kuibua hoja nzito za ufisadi wakiwa na nyaraka muhimu za Serikali ni Mbunge wa Karatu Dkt. Wilbrod Slaa (CHADEMA) ambaye baadhi ya hoja zake zimekuwa mwiba kwa baadhi ya watendaji ambao si waaminifu.

  Akitoa maoni yake kuhusu onyo hilo, Dkt. Slaa alisema: "Nadhani hii ni dalili ya Serikali kukosa uelekeo na kushindwa. Ni wazi Serikali haiwezi kuendelea kupambana na vitendo vya kifisadi kwa kufanya hivyo."

  Alisema Watanzania wakumbuke kuwa alilazimika kuchomoa hoja yake Bungeni baada ya kupata barua kutoka idara nyeti ya Serikali kwenda kwa Waziri Mkuu ikitaka Serikali isikubali kupeleka hoja yake bungeni kwa sababu haina majibu juu ya hoja hiyo.

  "Naishangaa sana Serikali inasahahu hivi karibuni tu iliwasilisha hoja
  bungeni kuongeza sh. bilioni 53 zilizorudishwa kutokana na kuibuliwa kwa ufisadi ili zitumike kwa masuala ya maendeleo, leo inatishia watu kwamba wasiendelee kuibua masuala hayo?" Alihoji Dkt. Slaa kwa masikitiko.

  Kuhusu umaarufu, mwanasiasa huyo alisema: "Kama wanasema mimi natafuta umaarufu sawa nakubali, lakini umaarufu unatokana na kazi kubwa na kufanikiwa katika kufanya utafiti juu ya jambo fulani. Sasa kama mimi knilitafuta umaarufu wa kufanya kazi kubwa ya kuibua ufisadi na kuwasaidia Watanzania basi kweli ninastahili umaarufu maana ni matokeo ya kazi kubwa na si ya bure."

  Aliahidi kuwa vitisho hivyo haviwezi kukwamisha moto uliowaka wa mapambano yao dhidi ya ufisadi na kwamba aliwahi kutumiwa ujumbe wa vitisho na hatimaye kuwekewa vinasa sauti chumbani lakini hawezi kuogopa kwa kuwa anayestahili kuogopwa ni Mungu tu.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Unapowatuhumu Wabunge KUIBA ni bora uwe na ushahidi wa kutosha kwamba watu hawa ni wezi.. Binafsi nafikiri Bi Hawa Ghasia ni lazima awajibishwe kama atashindwa kuwataja na kuleta ushahidi wa wazi kwa sababu ametumia neno zito kuwa Wabunge wezi wapo ktk bunge letu...Hakuna sheria yoyote inayoruhusu mwizi kuachiwa kwa sababu yoyote ile..
  AWATAJE wezi hao, wananchi tupate kuwafahamu.Hatuwezi kuendelea kuwakilishwa na Wabunge wezi..
   
 20. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,118
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Lazaro pumba kinoma!
   
Loading...