MPs warned over documents

Watu humu ndani mkishidwa kuwa realistic and fair then everything else that we do here kitakuwa ridiculed tuu.. The Government, infact no government, could ever sanction unlawful dissemination of material that is under the stamp of 'top secret'.. its just wrong! no matter the motive.. simple as..
 
Watu humu ndani mkishidwa kuwa realistic and fair then everything else that we do here kitakuwa ridiculed tuu.. The Government, infact no government, could ever sanction unlawful dissemination of material that is under the stamp of 'top secret'.. its just wrong! no matter the motive.. simple as..

Top secret ya kuuza nchi na kukwiba?? give me a break!
 
Watu humu ndani mkishidwa kuwa realistic and fair then everything else that we do here kitakuwa ridiculed tuu.. The Government, infact no government, could ever sanction unlawful dissemination of material that is under the stamp of 'top secret'.. its just wrong! no matter the motive.. simple as..

Is it fair watu kutumia forged documents kuiba billions from the central bank?

Is it fair watu kuingia mikataba kuuza rasilimali zetu for a song ili wao wapocket billions in kickbacks?

Is it fair watu kuingia highly inflated bogus procurement deals (rada/Richmond/Dowans) and pocket billions in bribes at tax-payers expense?

If all those above are regarded as "top secret" by the government and should not be divulged, what hope is there for the common mwananchi?

Is that in your best interest? Is that what you would like to remain top secret?
 
Watu humu ndani mkishidwa kuwa realistic and fair then everything else that we do here kitakuwa ridiculed tuu.. The Government, infact no government, could ever sanction unlawful dissemination of material that is under the stamp of 'top secret'.. its just wrong! no matter the motive.. simple as..

Kinyambiss.. tunaelewa sana suala la "nyaraka za siri". Ukifikiria kwa karibu utaona kuwa hakuna nyaraka yoyote ambayo imetumiwa hadi leo kufichua ufisadi inaweza kuangukia kwenye nyaraka za siri. Ghasia na genge lake wanachojaribu kuzuia ni nyaraka zinazotoa siri za ufisadi. Hizi kwao ndiyo nyaraka za siri.

Hakuna nyaraka za maafisa wetu wa intelligencia ziko hadharani; hakuna Nyaraka za matumizi yetu ya kijeshi au vifaa vya kijeshi vinavyoingia na mbinu za kivita (don't believe what you see on Wikipedia!). Ni top secret.

Kina Ghasia hawana tatizo na nyaraka za siri proper, tatizo lao ni kuwa nyaraka zinazofichua ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za wananchi. Wao hawataki hayo yajulikane. Wanachotaka ni kurudisha nidhamu ya woga na utawala wa hofu.

Siri anazozingumzia siyo zile zenye kulind maslahi ya taifa bali ya matumbo ya wenye taifa.
 
Date::4/22/2009
Wananchi wadai sheria ya nyaraka ni kuficha wizi

Na Salim Said

Mwananchi

SIKU moja baada ya serikali kutoa onyo kwa wabunge wanaotumia nyaraka za siri za serikali, baadhi ya wanasiasa na wananchi wamepinga kauli hiyo na kusisitiza kuwa kuzilinda nyaraka zinazoelezea ufisadi ndani ya serikali ni wizi wa mali za umma.

Juzi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti na Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia aliliambia Bunge mjini Dodoma kuwa, mbunge yeyote atakayebainika kutumia nyaraka za siri za serikali, hatua kali za kisheria zitachukuliwa bila ya kujali nafasi yake.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana, baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa vyama vya siasa na wananchi walisema, hawakubaliani na kauli hiyo kwani inatishia udadisi wa mali za wananchi.

Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Samuwel Ruhuza alisema, kauli hiyo ni ya kisiasa zaidi, kwa kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeona kuwa ufisadi mkubwa umewekwa hadharani katika miezi michache iliyopita.

Alisema, hizo zinazoitwa nyaraka za siri za serikali, siri kubwa iliyomo ni wizi tu wa rasilimali za umma, lakini hakuna siri kama invyohubiriwa na Waziri Ghasia.

“Unajua ndugu mwandishi, leo hii ukienda kuulizia mkataba wa Kiwira kwa mfano, utaambiwa ni siri, lakini siri hiyo ni wizi ambao umefanywa na waziri aliyesaini mkataba huo. Kwa hiyo nyaraka zote hizo zinaficha wizi tu” alisema Ruhuza na kuongeza:

“Katika nchi hii kuna wazalendo na wasiokuwa wazalendo, ambao ndio huibia nchi kwa kusaini mikataba tata, lakini wazalendo ndio wanaotupatia mikataba hiyo na kufichua wizi uliomo”.

Aliwataka wazalendo kuendelea kuiba nyaraka hizo na kuwapatia viongozi wa upinzani, ili kuweka hadharani wizi unaofanywa na viongozi wa serikali.

“Tunawaomba wazalendo waendelee kuzisaka na kutupatia nyaraka hizo, na sisi pia tutaendelea kuzisaka na kuzitumia,” alisema Ruhuza.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alisema, kauli hiyo inathibitisha udhaifu wa serikali katika kufanya kazi zake.

“Ulimwengu huu ni wa uadilifu, ukweli na uwazi, sasa unaficha nini cha ajabu kama wewe ni muadilifu kwa wananchi wako unaowaongoza, kama si wizi ni nini?” alihoji profesa Lipumba.

Alisema wanaotumia nyaraka hizo wanajaribu kuwaeleza wananchi kile kinachofanywa na serikali yao, kwa hiyo kuwaficha wananchi kujua mwenendo wa serikali yao ni kuwaumiza”.


Alisema, kinachosababisha hayo ni wizi, ujambazi na ufisadi wa baadhi ya viongozi walioaminiwa na wananchi, lakini wamekosa uaminifu na kuanza kupora mali za umma.

“Tunapinga kwa nguvu zote kauli hiyo, kwa kuwa inadidimiza demokrasia, uhuru wa habari nchini kwa kuwaficha wananchi kujua waharibifu na waporaji wa mali na kodi zao” alisema profesa Lipumba.

“Katika kipindi hiki tunahitaji ukweli na uwazi wa shughuli za serikali na sio usiri kwa sababu usiri unadumaza demokrasia na unarudisha nyuma maendeleo ya jamii” alisema.

Kwa upande wake Abdulwaheed mkazi wa mjini Unguja alilalamikia kitendo cha viongozi wa serikali kutumia sheria kujilinda na kuficha maovu yao.

“Kauli hii ya Ghasia inaonyesha wazi matumizi mabaya ya sheria, ambapo waziri anajaribu kutumia sheria kujilinda yeye na wenzake ambao wanafanya ufisadi ndani ya serikali” alisema Abdulwaheed na kuongeza:

“Hii ni katika jitihada za serikali kuwafumba midomo wabunge wa upinzani kutupatia taarifa muhimu, lakini sidhani kama watatishika na tunawaomba wasitishike kwa sababu tuko pamoja nao”.

Alifafanua kuwa, kauli hiyo inaweza kusababisha kukua kwa ufisadi kwa sababu maofisa wa serikali ambao walikuwa na uzalendo na ujasiri wa kuvujisha nyaraka hizo kwa wabunge kuogopa.

“Hii inaweza kusababisha kukua kwa ufisadi badala ya kupungua na pia ni pigo kwa vyombo vya habari hasa katika kuandika habari za uchunguzi” alisema.


Miaka miwili iliyopita viongozi wa vyama vya wapinzani hasa wabunge wameibuwa ufisadi mkubwa katika mikataba mbalimbali ya serikali ikiwa ni pamoja na Richmond na Malipo ya Akaunti za Madeni ya Nje (EPA).
 
Back
Top Bottom