Mpoto: Mzee Ngosha wa Nembo ya Taifa alikuja kwangu kama 'chizi', tukafanya kazi, akatutoroka..

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Msanii Mrisho Mpoto ameshtushwa na msiba wa Mzee Ngosha kwa aina yake!

Kwanza hakujua kama ni mtu aliyewahi kufanya naye kazi. Pia hakujua kama alikuwa mzima kichwani au la! Amekuja kugundua baada ya taarifa za kifo chake..

Anakumbuka ushauri wake uliosindikizwa na ujumbe "Yachukulie maneno haya ni ya chizi kaongea''.

Kwa ufupi, kisa ni cha kusikitisha na kufunza.

Tazama dakika ya 2 sekunde ya 22 (huyo mzee mwenye kofia nyekundu).

IMG_7218.jpg




Well, msomeni Mpoto;
------------
"Hii ni taarifa ya kunisikitisha sana kwenye maisha yangu ya Muziki naomba niwashirikishe ndugu zangu.

Nakumbuka kabla ya kutoa wimbo wa [HASHTAG]#SIZONJE[/HASHTAG] Nyuma yake nilitoa "NJOOUICHUKUE" huyu mzee alikuja ofisini kwangu kuniambia maneno mzito sana kwamba anapenda kazi yangu na alinitabiria mambo mengi mazuri kwenye safari yangu ya Maisha nanukuu "YACHUKULIE MANENO HAYA NI YA CHIZI KAONGEA".

Ombi lake lilikua moja tu alitamani kufanya kazi na Mimi, ofisi nzima ikamchukulia kama mzee aliyechanganyikiwa wakataka kumfukuza, mlinzi wetu Wa ofisi akasema msimpuuze mpeni nafasi.

Tulipompa nafasi ndiyo akatoa wazo la video ya wimbo Wa [HASHTAG]#njoouichukue[/HASHTAG] iweje, na akasema yule mzee Mshuba kikongwe Muuza Bangi ataigiza yeye mwenyewe. Tulicheka Sana maana wazo lake lilikua zuri na liliungwa mkono na Director Adamu Juma.

Sasa leo baada ya kuangalia kwa makini kumbe ndiyo Yule mzee aliyefariki leo Mchora Nembo ya Taifa. Natamani siku zirudi nyuma niongee nae Tena, roho imeniuma sana kwa kweli sijui hata nifanye nini.

Kibaya zaidi baada ya shooting alitutoroka hata hatukujua tutampataje!

Ndugu wa marehemu tafadhalini mtujulishe kuhusu mazishi yake! ".
-------------

Ni hayo tu!
 
Alikuwa "shushushu"
Zamani wakiitwa hivyo.

Wenzao nowadays wana wa waa wanak wan wanakaaa!!!
(sorry nimepatwa kigugumizi ukubwani) ntarudi baadae
This makes sense.. Maana alivyowatoroka ni character za mshushushu!
 
Hii kiki ya bajaji kabisa. Huyo mzee anatakribani wiki mbili anazungumzwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, inamaana alikuwa hajajua, mpaka alivyoaga duniani ndio anatoa maneno?
 
Kick tu....yaani ni kusema hata front page za magazeti hakumuona siku alipookotwa huko Buguruni,Mpoto huwa haangalii hata taarifa za habari?aliogopa akianza kusema uwongo wake huu kwamba huyo mzee alimtoroka kipindi akiwa hai angepinga kwa ukweli kwamba alimpigisha kazi kwa malipo kiduchu au hakumlipa kabisa ila kwa sasa kwa7bu amenyamaza kimya maisha yote kaona aibuke akatafute wingi wa likes Fb na Inst.hapo umesisitiza kujulishwa mipango ya mazishi badala ya kuuliza njia gani ya kutoa rambirambi mpoto acha unafiq siku yako na wewe inakuja.
 
Hii kiki ya bajaji kabisa. Huyo mzee anatakribani wiki mbili anazungumzwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, inamaana alikuwa hajajua, mpaka alivyoaga duniani ndio anatoa maneno?
Ameielewa sura ya marehemu
 
Back
Top Bottom