JoJiPoJi
JF-Expert Member
- Aug 8, 2009
- 2,920
- 3,309
Mzee Francis Kanyasu aliyechora Nembo ya Taifa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye matibabu Muhimbili Hospital
======
Mzee Francis Kanyasu maarufu kama Ngosha alisikika kwa nguvu mara ya kwanza alipoibuliwa na chombo cha habari cha ITV baada ya kukutwa anaishi maisha duni eneo la Buguruni kwenye kibanda kilichoonekana cha hovyo sana na tangu hapo akawa ajenda kiasi cha kuonekana na mamlaka husika.
REJEA: Mbunifu wa Nembo ya Taifa anaishi maisha duni sana
Siku chache zilizofata, serikali ilitoa taarifa rasmi ya kumpeleka mzee Ngosha hospitali ya Muhimbili na kumhudumia. Pia alitembelewa na naibu waziri wa afya, Hamis Kigwangala na kusema wamelazima kumuhamishia hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina kisha kutibiwa.
Naibu waziri alisistiza azma ya serikali kumpatia matunzo bora ikiwemo tiba na malezi katika kuthamini mchango wa wazee wasisi wa taifa. Kwa upande wake mzee Ngosha
Baadae ikajitokeza familia na kudai mzee huyo sie aliechora nembo hiyo bali ni mzee wao na alishatangulia mbele ya haki na walipoulizwa kuhusu ushahidi, walisema “Ushahidi ambao tunao ni wale watu wa rika lake ndiyo walikuwa wanashuhudia kwamba yeye ndiye aliyechora.”
Mei 28, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr. John Magufuli akiwa na mkewe walitembelea wagonjwa hospitali ya Muhimbili akiwemo mzee Kanyasu na Rais aliwashukuru madaktari wote wa Muhimbili kwa kazi wanayoifanya.
REJEA: Rais Magufuli na Mkewe watembelea Muhimbili, amtembelea Mzee Ngosha