Mpoto atumbuize kwenye vikao vya CCM badala ya Komba

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,855
8,253
Ndugu zanguni naomba kuwasilisha hoja ,kwa maoni yangu ningependa Mpoto apewe nafasi ya kutumbuiza kabla ya kuanza vikao vya CCM badala ya TOT ya Komba naamini mashairi ya Mpoto huenda yakawakumbusha waheshimiwa hali halisi ya Mtanzania wa kawaida kuliko hizo kwaya za mhe Komba kwani hakuna kipya katika tungo zake zaidi ya kuimba kwa kujikomba kwa wakulu,uwezo wake umefikia mwisho hana jipya ni sawa na Maximo na Taifa Stars(?) .
 
asiende kabisa ccm. watamchafua. huwezi ukacheza kwenye tope usipakae matope
 
Ni wazo zuri sana, lakini implementation kama hiyo inawezekana kwa mawazo yako?..."Tazama wamama wajawazito walivyolala mzunguwanne kule Amana, wakingoja mgomo wa madaktari uishe"....Unadhani maneno kama hayo utaimba mbele ya Makamba na lile tumbo lake?
 
CCM wanapenda kusifiwa tu hata kama wanafanya madudu. Mpoto pale hatafanya kazi wanaweza kumfurusha kama sio wa CCM wakamtungia nyimbo za kuimba. acha waendelee na huyo huyo Komba na yeye ni kama wao so wana-match!!
 
Jamani msisahau kuna kijana wa bongo flava kaimba wimbo unaitwa 'Mr. President' anaitwa Muro (mtanisahisha jina la mwimbaji kama nimekosea). Wimbo umeanza kupigwa katika baadhi ya radio station hapa mjini. Binafsi nimeusikia karibu mara 4 radio clouds fm na magic fm.

Huu wimbo ni mkuki mchungu sana kwa Rais Kikwete na wanamtandao wote. Mtunzi ajaficha kitu, kauchambua utawala wa JK na matukio yote kuanzia nukuu za mwalimu Nyerere. kampeni za JK za mwaka 2005 na performance yake to date.

Though sijausikia for a week now, si ajabu ukawa umepigwa marufuku (banned) na watawala. Naamini mheshimiwa akipata bahati/nafasi ya kuusikia wimbo huu na kuuelewa, basi magogoni 'patachimbika'!!
 
Hehehe
Wanajamii nimeshawatungia WIMBO nasubiri siku tukianza vikao vyetu nitawachania mistari au vipi YO YO?
 
Back
Top Bottom