juve2012
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 3,343
- 2,040
Pesa na tacticians wanaharibu the beautiful game, juzi nilikua namsikiliza kocha wa Reading aliyetimuliwa, anasema kwenye championship wanacheza open games, they pass the ball and players express their skills lakini ukiwa EPL ukijaribu kucheza hivyo jiandae kushuka daraja, kama huamin waulize Blackpool ya kina Charlie Adams, sasa imagine kwa ligi kama EPL inayoangaliwa zaidi duniani ili usurvive inabidi ucheze hovyohovyo, ukienda Spain ni ligi ya team mbili tu cku hzi na hiyo inatokana na pesa za mikopo walizonazo hizi team kubwa mbili na ndio clubs zenye madeni makubwa kati ya club kubwa za Ulaya.
Na kwa sababu pesa imekua too much kwenye club level mpaka inafikia kuua vipaji vya wachezaji wazuri kwa sababu ya ukwasi walionao (sihitaji kuwataja coz mnawajua) ndio maana soka la kimataifa limekosa ladha kabisaa. FIFA rushwa na siasa vimetawala. Tuombe uzima lakini cjui miaka 10 ijayo tutaona mpira wa aina gani kwa hii dunia ya sasa ambayo mungu wake ni pesa!
kwetu sie wa kitambo ndio tunaiona hii tofauti lakini wenyewe wa kizazi cha leo wanaona kumekucha!hamuwezi amini mechi za jana na leo sijatazama,na matokeo yamekuwa vile vile watu walivyohisi.zamani ukienda juve unakuta watu,ukienda man u watu,arsenal watu,Marseille,deportivo,valencia ya akina Mendieta,barca,Munich,leverkusen,Ajax.sasa leo watu wote wako madrid,barca,na hawa wanakopa bank huku wewe juve kwenu mikopo marufuku,viwanja ndio tunapata ruhusa ya kujenga miaka hii,timu zimefilisika,sio serie a ile huku napoli maradona,kule juve baggio,hapa milan van bastern,kule inter de lima,hapo fiorentina batigol,huku lazio Crespo,kule parma buffon,Nakata..hapo hujaja la liga ukamchungulia Rivaldo,Hiero na wenzao,hujaenda kwa Lars Ricken,effenburg na wenzao Bundesliga,hujarudi kwa Pele,Papin,Duggary,karembeu na wenzao pale league one,hujarudi kwa Davids mjini amsterdam,yaani nazunguka tu sijaingia Epl hapo mtanisaidia wenyewe,labda nimtaje jamaa yule wa Newcastle alikuwa ananirusha roho sana..Faustinoo..(Chomba malizia).ukienda Galatasaray unamkuta Hagi na yule jamaa anapiga mashuti ya vichwa Mario Jardel.hujarudi coppa libertadores uwakute river plate,flamengo na magoli ya hatari kabisa!yaani unashika remote unazunguuka tuu hujui utazame wapi!tangu 1990(nakumbuka mwaka huu nilitandikwa bakora shule kwa kuchafua daftari na picha za akina Biyick,Mfede,Milla,higuita,Cannigia,Donadoni) hadi 2002 ni rusha roho tuu!leo hii umtazame nani serie a,league one,holland?utaishia spain umtazame cr7 na messi wee hadi usinzie!