Hakuna namna tumpe maua yake. Unapokuta watu uliowadhania ni wapinzani wanageuka na kujiunga na CCM wakati wa uchaguzi ni lazima ujiulize kama walikuwa wapinzani kweli au walikuwa wanatafuta pa kuhemea tu.
Ati leo Joshua Nassari yuko CCM..
Ati leo Wenje yuko CCM
Ati leo Peter Msigwa yuko CCM...
Kazi kwelikweli
Sasa hapa kwenye mada hii kuna jipya lipi mkuu ' Mwanakijiji"? Au kwa vile umezungumzia hao wachache tu toka CHADEMA, ambao wote walijulikana toka zamani?
Tunao wakongwe, akina Lipumba, Cheyo; akina Qeen Sendeka (hata sijui kama jina ni sahihi), na wengi wengine; lakini kutomtaja Mbowe kutanifanya nisiwe mkweli kwa kiasi kikubwa
Ndio, akina Mzee wa Kiracha (?) hao walikuwa ni wapinzani wa dhamira ya mioyo yao, au walikuwa ni wachimba dhahabu?
Yule nani yule, Mtikila, alikuwa ni mpinzani, kwa sababu alisimamia jambo ambalo halikuwa na lengo la kumletea manufaa yeye binafsi.
J.J. Mnyika, ni 'principled, mbali kabisa na hizi takataka za akina Wenje, Yericko na wengi wengine waliokuwa wamejazana ndasni ya chama hicho kabla ya ujio wa uongozi mpya.
N.B., Sitakuwa mkweli pia kama siwezi kumtambua binti Halima Mdee aliye "kengeushwa". Huyu ni mpinzani wa kweli.