Mpigapicha TBC apigwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpigapicha TBC apigwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 6, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Mpigapicha TBC apigwa

  Imeandikwa na Hellen Mlacky; Tarehe: 5th January 2011 @ 23:53

  MPIGAPICHA wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Josias Charanga ameshambuliwa na kuporwa kamera yake na Ofisa Usalama wa Taifa wakati akipiga picha maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU).

  Wanafunzi hao zaidi ya 200 waliandamana jana hadi Ofisi ya Waziri Mkuu wakitaka msaada kwa madai kwamba wamedanganywa kwamba chuo hicho kimesajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) hali ambayo si kweli.

  Katika maandamano hayo, walikuwamo waandishi wa habari wakifanya kazi yao akiwamo mpigapicha huyo wa TBC ambaye alipigwa na kunyang’anywa kamera yake.

  Kabla ya kipigo hicho, ofisa huyo alimfuata mpigapicha wa Mwananchi na kumwuliza sababu za kumpiga picha na kuchukua kamera aliyokuwanayo na kumwamuru afute picha alizopiga.

  Baada ya hapo, alimfuata mpigapicha wa TBC na kamera yake na kumkwida shati na kisha kumwingiza Mapokezi na kumpiga vibao kwa madai kwamba alimpiga picha wakati akiwatuliza wanafunzi hao.

  “Usinipige picha, nitachukua kamera yako,” alisema ofisa huyo, maneno ambayo yalifuatiwa na kipigo na kunyang’anywa kamera mpigapicha huyo wa Kituo cha Televisheni cha Serikali.

  Mapema wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanafunzi hao walidai kuwa wamekuwa wakikosa haki za msingi sawa na vyuo vingine, kutokana na kudanganywa kuwa wamesajiliwa na TCU, hali ambayo si kweli kwa sababu chuo hicho ni cha masomo ya Posta, kwa kuwa kiko Kampala na huku ni tawi tu.

  Walidai kuwa kama wangeambiwa mapema kuwa chuo hicho hakijasajiliwa, wasingejiunga, kwa sababu wapo wenye vigezo vyote vya kuingia vyuo vingine vilivyosajiliwa na TCU tofauti na hicho.

  Tatizo lingine wanafunzi hao walidai kuwa ni ada kubwa wanayotozwa ya Sh milioni 2.7 ambapo pia walisema wamekuwa wakitozwa Sh 70,000 kwa kila mwanafunzi anayetakiwa kurudia mtihani baada ya kutofanya vizuri kitendo ambacho walidai si sawa.

  Walisema kuwa wameshalalamika mara nyingi na kufikisha malalamiko yao mpaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, lakini mpaka sasa wamekuwa wakiambulia ahadi na kuamua kuandamana hadi kwa Waziri Mkuu ili kufikisha kilio chao.

  Hata hivyo, baadaye wanafunzi hao walitakiwa kutoa wawakilishi watano waingie ndani kuwasilisha hoja zao na baadaye mmoja wa wanafunzi aliyeingia ndani aliwatangazia wenzake kuwa watapewa majibu leo saa 5 asubuhi.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  JK has just unleashed a police state upon us...........How sad..........What a legacy to bequeath his populace.................
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Goshhhh!!!!!!!!!!!!
   
 4. n

  ngoko JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii ndiyo njia ya kutunza amani na utulivu tuliojijengea ( ndani yake kuna hayo machungu)
   
 5. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #5
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  It's a chain reaction..who to intervene?
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yani ni uonevu wa hali ya juu!
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,107
  Likes Received: 5,563
  Trophy Points: 280
  unajau maana ya kupigwa??
  akaulize yule aliekimbilia magereza kesi za ATC
  amwonyeshe kovu huyo hata Damu ajamwaga anasema kapigwa nexty tym mpigen kweli
  pole
  Kaka Josias
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mbona jk anatangaza uhuru kwa vyombo vya habari ndio huu ss
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  TUCTA nao waongezee chachandu pls kaombeni kibali cha maandamano moto wa mapambano umeanza
   
 10. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mimi naona ni sawa tu kwani jamaa alishamalert kuwa asimpige picha atachukua kamera yake sasa kwa kuwa waandishi wengi wa habari tunasahau kazi yetu ya msingi tumeingia kwenye uanaharakati na kuwa na kiburi cha hicho kiproganda kinachoitwa haki za binadamu to fullfill someones interest, bora mtu apigwe akumbushwe shule.
   
 11. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  safi tena safi sana...huyo aliyetoa kichapo anipe namba yake nimrushie vocha ya shilingi 2,000 tu kama asante kwa watu wasiofuata taratibu......!
  Isitoshe na hao wanafunzi hawajui kuwa ile ni KAMPALA?....si wasome tu kwa njia yao ya posta? kuna ubaya gani....? wakati wanafanya taratibu za kujiunga si walijuwa kuwa ada ni 2.sth milion......sasa wanaandamana nini?
   
Loading...