Sasa kama sisi Watz tumelala- je wao wafanyeje?
Naomba kutofautiana na wachangiaji wanao support wachina kufanyakazi za upigadebe hapa Tanzania.Ningependa wachina waje kwa wingi hapa Tanzania kufanyakazi za kitaalamu kama ujenzi,utengenezaji wa mitambo na kazi nyingine zinazohusiana na utaalamu.Leo kama tunashangilia wachina kufanyakazi za wapiga debe nadhani tunatakiwa kujiangalia na kujipanga vyema kwasababu hizi kazi za wapiga debe tunazipiga vita si kwa wachina tu bali hata kwa watanzania wazawa sasa iweje leo tunashabikia wachina kufanyakazi ambazo hata watanzania tunawakaza.Idara yetu ya uhamiaji inatakiwa kuimarishwa ili kukabiliana na wimbi la wageni wa aina zote kufanyakazi ambazo watanzania wangeweza kuzifanya au kazi zisizohitaji mtaji mkubwa kuzianzisha.EAC inakuja muda si mrefu kama uhamiaji itashindwa kuwadhibiti wageni kuto nchi za mbali kama China sijui itakuwaje kwa wageni wanchitulizopakana nazo.
Soma vizuri, hawa si wapigadebe ni wawekezaji. Wanachofanya ni kuvutia watu wapande mabasi yao. Tofauti na wapiga sebe wao hawana mabasi ila wanauzia wenye mabasi abiria. Umeona tofauti hapo?. Kama wanalipa kodi hicho ndiyo muhimu. Ajira wanaitoa kwa madereva wa kitanzania wanaoendesha mabasi yao. Kazi ya marketing ya kuvutia abiria wanaifanya wenyewe japo mnawaita wapiga debe.
Cha kujiuliza hapa ni je wabongo hawatawahujumu?, maana kama huduma yao ni nzuri ukweli ni kuwa kila abiria ataipenda huduma yao na kuongeza ushindani wa huduma bora katika usafirishaji. Mi nawafagilia sana hawa jamaa. Sisi kazi yetu kupiga domo tu oooh mchina oooh anapiga debe wakati jamaa wanaendeleza kampuni yao. Tuache shutuma zisizo na msingi na kuwa wabunifu zaidi vinginevyo tutakuwa tunaishia kwa waganga wa jadi tu kuvutia abiria na kuchinja ng'ombe wakati wenzetu mganga wao ni kutoa huduma bora.
Basi hilo ni zuri sana. Nilipanda kwenda Mbeya majuzi. Ni fully airconditioned (inafanya kazi), reclining seats (2X2) na toilet ndani.
Sheria, kanuni na taratibu zetu zinaruhusu haya? kama ndiyo, no problem....!
Leo asubuhi nilikuwa nasindikiza wageni kuelekea bara (mkoani). Nikiwa ndani ya stendi ya mabasi ya Ubungo kiasi cha saa 11:15 (kumi na moja na robo alfajiri) nilikumbana na mpiga debe wa kichina akiniaambia 'lipo basi la Obama hapa linakwenda Mbeya hadi Tunduma" (lafudhi ya kihuuhii). Sikuamini ilibidi nisimame nihakikishe anayoyasema. Baada ya kudadisi nikaambia hao wachina (walikuwa watatu) unaowaona wanamiliki hilo basi (pembeni yetu) lenye rangi za bendera ya USA linalofanya safari zake Dar-Tunduma.
Jamani, hivi kweli mchina ananunua basi na anaajiri mpiga debe mchina, mkata tiketi mchina, vibari vya kufanya uhuni huu wanapata wapi?
Kweli mtanzania unaweza kwenda nchi za watu ukafanya hivi?
Hata kama zinaruhusu hazitufai, ni za kijinga na hatari kwa maendeleo yetu!
Kama kawaida yako tayali umesharusha shutuma, hakuna hata mmoja ambae amethibitisha kama hao wachina wanakaa isivyo halali, inawezekana wana uraia wa Tz vilevile, aidha ukisoma mabandiko yaliyotangulia, ni kwamba sio wapiga debe bali wanafanya marketing kwa basi lao.Only in Tanzania!!. Nchi nyingine kuna kazi na biashara ambazo wageni hawaruhusiwi kabisa kuzifanya lakini kwetu wageni tena wengine wanaishi kiharamu kila wanachotaka kufanya wanafanya tu ...🙁
Mkuu Hofstede nimekupata vizuri lakini uwekezaji wa aina hii ambao ajira zote zinabaki kwa wachina wewe unalionaje.Nini faida ya kuvutia wawekezaji kama ajira hata za kupiga debe wanazichukua wao.