Mpiga debe wa Kichina stendi ya Ubungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpiga debe wa Kichina stendi ya Ubungo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jafar, Feb 5, 2009.

 1. J

  Jafar JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Leo asubuhi nilikuwa nasindikiza wageni kuelekea bara (mkoani). Nikiwa ndani ya stendi ya mabasi ya Ubungo kiasi cha saa 11:15 (kumi na moja na robo alfajiri) nilikumbana na mpiga debe wa kichina akiniaambia 'lipo basi la Obama hapa linakwenda Mbeya hadi Tunduma" (lafudhi ya kihuuhii). Sikuamini ilibidi nisimame nihakikishe anayoyasema. Baada ya kudadisi nikaambia hao wachina (walikuwa watatu) unaowaona wanamiliki hilo basi (pembeni yetu) lenye rangi za bendera ya USA linalofanya safari zake Dar-Tunduma.

  Jamani, hivi kweli mchina ananunua basi na anaajiri mpiga debe mchina, mkata tiketi mchina, vibari vya kufanya uhuni huu wanapata wapi?

  Kweli mtanzania unaweza kwenda nchi za watu ukafanya hivi?
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,237
  Trophy Points: 280
  Wale Wachina wamiliki maduka Kariakoo, wanasukuma wenyewe mikokoteni ya bidhaa zao. Moja kubwa kuhusu Wachina, wanafanya mpaka biashara ya maching ila ni bidhaa zao.
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sheria, kanuni na taratibu zetu zinaruhusu haya? kama ndiyo, no problem....!
   
 4. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2009
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,591
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  Tatizo liko wapi?, kwanza kabla ya kushangaa ingebidi ujiulize kwamba huyo ni mtanzania au siyo?, maana Mtanzania siyo lazima awe na ngozi nyeusi!.

  well , huyo jamaa kama siyo Mtanzania je yupo nchini kihalali?, je hajavunja sheria zetu kuhusiana na kazi na biashara kwa wageni?. Kama hajazivunja nadhani hamna tatizo, hii dunia imekuwa kijiji. Mbona Watanzania kibao wapo ulaya na marekani wanagombania kazi na wenye nchi zao?. hapa kinachotakiwa ni sisi kuchapa kazi, tukilemaa hizo kazi zitakombwa na wageni halafu tutaendelea kulia foul, wakati kumbe tukipewa kazi zenyewe wala hatuzifanyi kiufanisi, au wakati mwingine siyo wabunifu
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Sasa kama sisi Watz tumelala- je wao wafanyeje?
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Hao ni wafanyabiashara halali office zao ziko pale shekilango mbele ya kituo cha mafuta na wanayo mabasi mengi sio hilo tu
   
 7. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Halafu sijui lipi la ajabu hapa.Wabongo wengi tu wanafanya biashara China. Tofauti ni kwamba wananunua China wanazituma Bongo , nyingi zikiwa feki.Wachina wameamua kurahisisha wanaleta wenyewe na wanauza wenyewe . Siju kama nazo hizi ni feki.
   
 8. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  let them chinese ni**az work, ukweli ni kuwa tumelala kwa kwenda mbele, hata sisi mbona tunajaribu biashara kwao china na Hong Kong, mbona hawatusumbui ki-hivyo, Acheni roho za korosho at least 2jifunze!

  I'm outta here! Peace
   
 9. B

  Baba Lao Member

  #9
  Feb 5, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  We Jafar si wapenda mteremko,wacha wazee kwa kazi wajitume maana inawezekana wanaona wabongo longo longo kibao na watu wa kupenda mteremko
   
 10. C

  Chief JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2009
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Basi hilo ni zuri sana. Nilipanda kwenda Mbeya majuzi. Ni fully airconditioned (inafanya kazi), reclining seats (2X2) na toilet ndani.
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Naomba kutofautiana na wachangiaji wanao support wachina kufanyakazi za upigadebe hapa Tanzania.Ningependa wachina waje kwa wingi hapa Tanzania kufanyakazi za kitaalamu kama ujenzi,utengenezaji wa mitambo na kazi nyingine zinazohusiana na utaalamu.Leo kama tunashangilia wachina kufanyakazi za wapiga debe nadhani tunatakiwa kujiangalia na kujipanga vyema kwasababu hizi kazi za wapiga debe tunazipiga vita si kwa wachina tu bali hata kwa watanzania wazawa sasa iweje leo tunashabikia wachina kufanyakazi ambazo hata watanzania tunawakaza.
  Idara yetu ya uhamiaji inatakiwa kuimarishwa ili kukabiliana na wimbi la wageni wa aina zote kufanyakazi ambazo watanzania wangeweza kuzifanya au kazi zisizohitaji mtaji mkubwa kuzianzisha.EAC inakuja muda si mrefu kama uhamiaji itashindwa kuwadhibiti wageni kuto nchi za mbali kama China sijui itakuwaje kwa wageni wanchitulizopakana nazo.
   
 12. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Soma vizuri, hawa si wapigadebe ni wawekezaji. Wanachofanya ni kuvutia watu wapande mabasi yao. Tofauti na wapiga sebe wao hawana mabasi ila wanauzia wenye mabasi abiria. Umeona tofauti hapo?. Kama wanalipa kodi hicho ndiyo muhimu. Ajira wanaitoa kwa madereva wa kitanzania wanaoendesha mabasi yao. Kazi ya marketing ya kuvutia abiria wanaifanya wenyewe japo mnawaita wapiga debe.

  Cha kujiuliza hapa ni je wabongo hawatawahujumu?, maana kama huduma yao ni nzuri ukweli ni kuwa kila abiria ataipenda huduma yao na kuongeza ushindani wa huduma bora katika usafirishaji. Mi nawafagilia sana hawa jamaa. Sisi kazi yetu kupiga domo tu oooh mchina oooh anapiga debe wakati jamaa wanaendeleza kampuni yao. Tuache shutuma zisizo na msingi na kuwa wabunifu zaidi vinginevyo tutakuwa tunaishia kwa waganga wa jadi tu kuvutia abiria na kuchinja ng'ombe na kuua watu wasio na hatia kwa kutaka short cut, wakati wenzetu mganga wao ni kutoa huduma bora.
   
  Last edited: Feb 5, 2009
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Hofstede nimekupata vizuri lakini uwekezaji wa aina hii ambao ajira zote zinabaki kwa wachina wewe unalionaje.Nini faida ya kuvutia wawekezaji kama ajira hata za kupiga debe wanazichukua wao.
   
 14. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #14
  Feb 5, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chief naomba utufahamishe yafuatayo maana wewe umesha onja hiyo huduma yao:--
  1. Nauli (kutoka DAR -MBY-TND) ukilinganisha na mabasi mengine (ya kiswahili - aka wazawa)
  2. Mwendo wa Mabasi haya (ya wachina - aka wawekezaji)
  3. Huduma (kuanzia, kupiga debe, kukata ticket, ndani ya basi, mizigo, kusimamisha abiria nk nk)
  4. Vp yakifika kwenye mizani kuna abiria wanashushwa?
  5. Je wanafuata ratiba waliyopangiwa ya kusafiri? (mda uliopangwa DAR-TDM unatumika vilivyo)
  6. Vp kuhusu wateja....wanapata au wanapelaka basi tupu?  Baada ya kuyafahamu hayo basi tufanye kulinganisha na huduma za mabasi ya wawekezaji wazawa ambayo tunayajua vizuri. Baada ya hapo sasa tuendelee na kudiscuss je uwepo wao una manufaa?

  Asante.
   
 15. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Hata kama zinaruhusu hazitufai, ni za kijinga na hatari kwa maendeleo yetu!
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,481
  Likes Received: 81,772
  Trophy Points: 280
  Only in Tanzania!!. Nchi nyingine kuna kazi na biashara ambazo wageni hawaruhusiwi kabisa kuzifanya lakini kwetu wageni tena wengine wanaishi kiharamu kila wanachotaka kufanya wanafanya tu ...:(
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu unataka maendeleo kwa kupiga debe!. Hivi wewe kama unabiashara yako unaitangaza kuna ubaya?, kama ndiyo basi promotion zote unaziona za Zain, TiGo n.k hazitufai kwa maendeleo yetu.kama mtazamo wako ni huo.

  Hakuna mzawa aliyetaka kuanzisha biashara akanyimwa kwa sababu tayari wachina wanazifanya. Tatizo la sisi wabongo porojo nyingi sana, akija mtu na idea yake nzuri yaani basi lake na kuvutia abiria anavutia yeye mwenyewe tayari mnaanza kulalamika. Tuache longolongo kama tunataka maendeleo na si kuwa na hasira na hawa jamaa ambao hawana hata haki ya kuchagua viongozi ambao tunawarudisha madarakani kila uchaguzi.
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kama kawaida yako tayali umesharusha shutuma, hakuna hata mmoja ambae amethibitisha kama hao wachina wanakaa isivyo halali, inawezekana wana uraia wa Tz vilevile, aidha ukisoma mabandiko yaliyotangulia, ni kwamba sio wapiga debe bali wanafanya marketing kwa basi lao.
   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  Feb 5, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hebu huyo aliyepanda atuambie je na dereva wa mabasi hayo ni wachina?, kama jibu ni ndiyo nakubaliana na wewe kabisa kuwa hii si sawa na inatakiwa kujua. Ila hebu tuangalie jambo jingine je hawa wachina hawajapata uraia?, kama ni raia hakuna haja ya kuwaonea. Mbona mabasi mengi sana ni ya waarabu na wahindi? hatusemi au utasema ni watanzania kama ni hivyo basi hata hawa wachina wanastahiki haki sawa kwani biashara ni ushindani na ili ufanikiwe boresha huduma.

  Mi ninawapenda hawa kwani sasa ndiyo maendeleo yatakuja kama basi lina huduma nzuri litawafanya na wale wanaoamini bishara ni kafara waache imani hizo na kufikiria kuboresha huduma. Mi niliwahi fanya kazi kwa muhindi mmoja longtime alikuwa na magari ya mizigo kila mwaka anachinja ng'ombe yard wakati magari mabovu. Sasa hizi imani zinapaswa ziishe. Hayo ndiyo maendeleo
   
 20. w

  wajinga Senior Member

  #20
  Feb 5, 2009
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona watanzania wemejaa nchi nyingi wanafagia kwani kuni ubaya gani.
   
Loading...